Mwanamke kutokuwa na uwezo wa kuzaa!

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
6,603
9,380
Ndugu zangu wanaJF, jamii imekuwa na unyanyapaa wa aina ya kipekee dhidi ya wanawake au wanaume wasio na uwezo wa kupata mtoto. Wamekuwa wanyonge na hata imekuwa tishio katika kudumu ndoa zao. Jamii imechukulia kila binadamu anazaa na asipoweza basi anaonekana kama hafai.
Najiuliza swali, kwani mwanamke kutokuwa na uwezo wa kuzaa inamfanya asiwe mwanamke? Je kuzaa pekee ndio uanamke?
Nimejaribu kuangalia nimegundua wanawake wengi ndio wa kwanza kuwanyanyapaa wale wasio na uwezo wa kupa a mtoto, kwa mfano, madada, mama yako mzazi, hata bibi wa mwanaume aliyeoa mwanamke mwenye matatizo ya uzazi.
Tumekuwa tunawaweka katika kundi la jinsia tofauti na wanawake wengine wakati kila kitu ni mwanamke just kutokuzaa. Nikajiuliza sana kwa nini mtu hajapata mtoto kwa miaka kadhaa anatengwa wakati nae anatamani mtoto ila uwezo hana, ila akipata ndio wanajamii wanajikomba kwake!
Ndugu zangu, mwanamke kutokuzaa haimfanyi yeye kutokuwa mwanamka kwani hata wale wenye uwezo wa kuzaa sio wote ni wakamilifu kwa kila sekta ya uanamke.
Nawasilisha hoja, nawaombeni tuchangie kwa ustaarabu.
 
Mi napita tu, ngoja wenyewe waje watachangia kiustaarabu
 
Mi napita tu, ngoja wenyewe waje watachangia kiustaarabu

Karibu mkuu, lakini katika hao unaowaita wenyewe na wewe upo! Kwani wewe ni member wa JF. Otherwise ulikuwa unamaanisha wenyewe wasiopata mtoto au wanaonyanyapaa?
 
Adui wa mwanamke ni mwanamke. Ukiwa wewe huzai wa kwanza kukunyanyasa ni wifi au mamamke na mwengine ni yule anayeshabikia kuwa nyumba ndogo.

Wote hao ni wanawake, yaleiti wangeweza kuweka nafsi zao kwenye machungu apitiayo mwanamke mgumba wasingethubutu.
 
Nimeliona hili, kwa mfano mwanamke asiye na uwezo wa kuzaa, akiolewa, watu wa kwanza kuulizia mtoto au ujauzito ni dada, mama, shangazi au bibi wa mwanaume, sijajua ni kwa nini, na wao huwa wa kwanza kumpatia ndugu yao kabinti eti huyu ni rafiki au mtoto wa rafiki amemaliza chuo flani. Sasa hata huyo nae anaeingilia ndoa ya watu ni mwanamke nadhani kuna shida sana ila as we know wanawake wana power hata ya ushawishi sasa wakishawishi vibaya matokeo yake ndio haya kwa jamii. Tunahitaji kubadilika!
 
Akiwa na kazi nzuri na analisha familia hata kama hazai ataonekana wa maana. Bro wangu kaoa wa design hiyo ma wifi zake wanampiga mizinga tu na kumsifia mke mwenye roho safi na anapenda ndugu. Absence ya mtoto miaka yote haionekani. Nafikiri angekuwa hazai alafu mama wa nyumbani it would have been a different story all together.
 
Ndugu zangu wanaJF, jamii imekuwa na unyanyapaa wa aina ya kipekee dhidi ya wanawake au wanaume wasio na uwezo wa kupata mtoto. Wamekuwa wanyonge na hata imekuwa tishio katika kudumu ndoa zao. Jamii imechukulia kila binadamu anazaa na asipoweza basi anaonekana kama hafai.
Najiuliza swali, kwani mwanamke kutokuwa na uwezo wa kuzaa inamfanya asiwe mwanamke? Je kuzaa pekee ndio uanamke?
Nimejaribu kuangalia nimegundua wanawake wengi ndio wa kwanza kuwanyanyapaa wale wasio na uwezo wa kupa a mtoto, kwa mfano, madada, mama yako mzazi, hata bibi wa mwanaume aliyeoa mwanamke mwenye matatizo ya uzazi.
Tumekuwa tunawaweka katika kundi la jinsia tofauti na wanawake wengine wakati kila kitu ni mwanamke just kutokuzaa. Nikajiuliza sana kwa nini mtu hajapata mtoto kwa miaka kadhaa anatengwa wakati nae anatamani mtoto ila uwezo hana, ila akipata ndio wanajamii wanajikomba kwake!
Ndugu zangu, mwanamke kutokuzaa haimfanyi yeye kutokuwa mwanamka kwani hata wale wenye uwezo wa kuzaa sio wote ni wakamilifu kwa kila sekta ya uanamke.
Nawasilisha hoja, nawaombeni tuchangie kwa ustaarabu.

Mzizi wa kunyanyaswa mtu asiyeweza kuzaa ni jamii zinazochukulia watoto kama mali. Aghalabu jamii za kikulima zinazotegemea ukulima wa jembe la mkono ulio wa kizamani. Kwa jamii hizi, kuzaa watoto wengi maana yake ni kupata wafanyakazi wengi katika shamba la familia na kuongeza uzalishaji.

Kwa hiyo kimsingi jamii kama hizi, mwanamke akiolewa na mwanamme halafu wasiweze kupata mtoto. Mara nyingi ndugu wa mwanamke (mara nyingine hata ndugu wa mwanamme) bila hata kujua sababu au nani ana "tatizo", kitu cha kwanza kitakuwa ni kumsema mwanamke. Kashindwa kuwaongezea nguvukazi ati, na hata "kuendeleza jina". Hapa tunaona unyanyapaa na mfumodume.

Jamii zilizoendelea na kutatua matatizo ya msingi kama chakula, malazi elimu na maradhi, zimeona kuzaa sana kama tatizo. Na si tu kwamba watu wasioweza kuzaa hawabaguliwi, kuna watu wengine wenye uwezo wa kuzaa lakini kwa sababu wana imani zao kuhusu idadi ya watu kuongezeka duniani, wanaamua kuacha kutafuta kupata mtoto.

Kwa hiyo ukiangalia sana utaona unyanyapaa huu unatokana na umasikini, ukosefu wa elimu na kuishi kwa kufikiri kwamba "kila mtoto anakuja na riziki yake". Kimsingi kupenda watoto ni kitu kizuri, kwa sababu kama watu wangekwenda upande mwingine kwa sana, watu tungekwisha duniani. Lakini kunyanyasa mtu asiyeweza kuzaa ni kutoelewa kuwa maana ya ndoa na mapenzi si kuzaa, ni kupendana.

Kwa hiyo mie kama nikimuoa mtu ninayempenda na ikatokea hatujapata mtoto wala sitaona tatizo.

Rafiki yangu mmoja ambaye ana mtoto alisema kitu kimoja sarcastic lakini kinaonyesha madhara ya "western education" kwake. Miaka ya kwanza akihofia sana jinsi mtoto wake atakavyoparamia vitu vyake, hususan alitaja speakers zake za bei mbaya za "Bang and Olufsen". Terrible.

Mnaijeria mmoja alipobanwa kuhusu watu wa dunia ya tatu kupenda kuzaana sana aliwalaumu watu wa magharibi kwa kuwa wabinafsi sana na kutaka raha zao kwa sana bila kufikiria wenzao, ingawa kuna chembe za ukweli katika hili, bado alikuwa anawajumuisha wote visivyo kwa maoni yangu.

Huyo rafiki yangu na huyo Mnaijeria wote walikuwa wanakosea kwa sababu walikuwa na extemes. Hatutakiwi kuwa wabinasi sana kiasi cha kuogopa watoto kwa sababu tunahofia wataharibu vitu vyetu (na vitu vinajumuisha mapaka mambo ambayo yanaweza kuheshimika kama mazingira, kwa hiyo anayekataa kuzaa kwa sababu anaogopa "Bang and Olufsen" itaharibika na anayekataa kuzaa kwa sababu anaogopa ozone layer itatoweka wako katika kundi moja, who is to say utakayezaa hatakuwa ndiye wa kutengeneza next level technology ya kuongezea "Bang & Olufsen" au kuondoa hofu kuhusu Ozone layer?)

Mie naona balance nzuri ni kwenda na George Carlin alichoki-popularize kama "replacement value". Kila mtu azae mmoja wa kuji replace. In a lifetime, more or less the population will not rise too much, but also will not fall too much.

Lakini nimebadilisha habari kutoka habari ya kunyanyaswa wasioweza kuzaa kwenda tatizo la population. Tukirudi kwenye habari ya mwanzo, kama nilivyosema, tatizo ni umasikini na elimu. Ndiyo maana analaumiwa mwanamke tu mara nyingi. Watu wanaangalia kwa macho, wanaona mwanamke anabeba mimba na kuzaa, kwa hiyo kama hawezi kuzaa tatizo ni yeye. Hawajui mwanamke hawezi kuzaa peke yake, na kama hawezi kuzaa peke yake, kukiwa na tatizo kwa mwanamme mwanamke hazai.

Umasikini na elimu vinafungamana, kama hujaweza kuutatua umasikini huwezi kuelimika, na kama hujaweza kuanza kuelimika hata kidogo umasikini huutatui. kwa hiyo vyote vinaenda pamoja. Na kama hatujatatua matatizo ya umasikini na elimu, haya mengine ya unyanyapaa ni lazima yawepo tu.

Mtu anayeamini kwamba mwanamke anaweza kurogwa asizae, au juwa mchawi ambaye sharti lake moja la kuendelea kuwa mchawi ni kutokuzaa, utawezaje kumwambia kwamba kubagua wasiozaa ni unyanyapaa?
 
Akiwa na kazi nzuri na analisha familia hata kama hazai ataonekana wa maana. Bro wangu kaoa wa design hiyo ma wifi zake wanampiga mizinga tu na kumsifia mke mwenye roho safi na anapenda ndugu. Absence ya mtoto miaka yote haionekani. Nafikiri angekuwa hazai alafu mama wa nyumbani it would have been a different story all together.

Hapa unazidi kuonyesha kwamba kuna habari ya uchumi inayohusika katika hili.

Inakuwa kama vile usipozaa unaharibu matumaini ya watu kwamba huenda "ukawatoa", watu familia hazina madaktari na wanasheria halafu wewe huzai?

Lakini kama wewe tayari mwanasheria au daktari au una mkwanja fresh unaweza kufadhili mambo vizuri, nani wa kukutaka uzae ili utoe mwingine? Hususan kama yeye mwenyewe hana?

Aibu!
 
Yalinikuta hayo. Wala sina hamu hata chembe. Na ubaya tatizo lilikuwa wala si kwangu bali ni kwa yeye. Lakini mineno na kashfa. Pamoja na kutunza familia lakini maneno toka kila kona.
Nilipochoka, nikajiondokea, na huko 'mtaani' nikapata mtoto wangu. Wanaogopa hata kutoa hongera!
Choka miye!
Ila humu duniani kuna stress jamani! Hata ukijifanya hujali lakini saa nyingine zinapenya kushinda hata pai (22/7), Lol
 
Back
Top Bottom