Mwanamke Kuchuchumaa - Marufuku

Mwanamke Kuchuchumaa - Marufuku

Sikonge

Platinum Member
Joined
Jan 19, 2008
Posts
11,635
Reaction score
6,238
Mbunge wa SIKONGE, Juma Nkumba ambaye anasifika kwa kuwa na vindevu kama Adolf Hitler au Bobby Mugabe, ameamua kuonyesha makucha yake jana jioni kwenye Mkutano wa Sungusungu hapa SIKONGE kwa kupiga marufuku akina Mama kujisaidia haja ndogo wakiwa Wamechuchumaa au Kuchutama.

Hili Swala limesababisha shida kubwa sana kwa akina Mama wa Sikonge na wakuja ambao hawana uwezo wa kuwa na vyoo vya kisasa vya kukaa kama vile vya watu wa majuu au mijini.

Jitihada kubwa zinafanywa kwa sasa ili kuwasiliana na KIKUNGU wa JF ili aweze kusaidia mambo ya kisheria yanasemaje na Mtetezi wa haki za akina Mama wa SIKONGE ambaye pia ni member wa JF aitwaye Kaunga akishirikiana na kiranja wa zamani wa Shule ya Msingi Chabutwa ambaye sasa amekuwa Mkulima kwa mara ya pili na yeye pia akiwa Member wa JF kwa jina la @ELNINO , wamesema watahakikisha hili jambo linafikishwa hadi kwa Jaji Mkuu na Mwanamuziki wa Rock wa Band ya U2 aitwaye BONO ili kutangaza Sikonge kama Kivutio kikubwa cha Utalii duniani kwa kuona Wanyama Mbugani na akina mama wakifanya vitu vyao bila kuvunja sheria ya Mbunge.

Pichani, Mama akiachia Maji bila kuvunja AMRI ya Nkumba.

14917_10151199287790793_2078481178_n.jpg


Jeuri ya Nkumba inaletwa zaidi na Pesa ndefu aliyonayo ambayo kwa sasa hadi amefungua Chuo Kikuu chake hapa SIKONGE chenye jina lake. Chuo hicho chenye hadhi ya juu, kimemfanya awe anaabudiwa hapa Sikonge.

Nkumba-bus.jpg
Saidi+Juma+Nkumba-Sikonge.jpg


Pichani ni BUS la Chuo cha Nkumba na kulia ni Nkumba mwenyewe.

Hii habari imeandikwa leo 01/04/2013.
 
Kabla hajamaliza Mkutano huo hapo jioni, ameonya tabia ya akina Baba kunywa Pombe, kulewa na mwisho kuangusha Magari yao wakiwa Mguu upande kuwa ni hatari kwa afya zao..... Mbwa wanaweza kukufanisha na ikawa shida.

65958_03_d_20110804090436.jpg

POMBE.jpg
554598_10151177720285568_649961656_n.jpg
 
Nadhani hayo ni maoni yake tu, hiyo kauli haina athari yoyote kwa kuwa haijatoka kwa kiongozi wa serikali. Angeitoa rais, waziri au RC na DC kwenye mamlaka zao kidogo ingetikisa, sasa mbunge hana nguvu yoyote kisheria ya kutoa amri. Usishangae kusikia yeye mwenyewe alikuwa amelewa wakati anaongea hayo!
 
wabunge siku hizi wana mamlaka ya kuamuru?

Pia anatumia nini kufikiri? anajua risk ya vyoo vya kukaa kwa wanawake?
 
Nadhani hayo ni maoni yake tu, hiyo kauli haina athari yoyote kwa kuwa haijatoka kwa kiongozi wa serikali. Angeitoa rais, waziri au RC na DC kwenye mamlaka zao kidogo ingetikisa, sasa mbunge hana nguvu yoyote kisheria ya kutoa amri. Usishangae kusikia yeye mwenyewe alikuwa amelewa wakati anaongea hayo!

Jabulani Happy fools day naona umeingizwa mkenge nawe umeingia!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom