Tangawizi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 7,846
- 8,484
[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] sio kivileUlivyokuwa unamwacha wiki mbili hkujua kuwa anahitaji mwanaume na yeye?
Post sent using JamiiForums mobile app
[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] sio kivileUlivyokuwa unamwacha wiki mbili hkujua kuwa anahitaji mwanaume na yeye?
Chapombe analeaje watoto?Waambie wahame yeye na mr range watoto wako utalea mwenyewe au ukubali kuwa houseboy wao iko siku watakwambiab usafishe range wao bado wamelala
Utaache mkeo na watoto? Kulikoni?
Post sent using JamiiForums mobile app
Haswaaaaa....Ndo ujifunze kabla ya kuingia kwenye mahusiano/ndoa
Kama ni dharau huyo mkeo amefikia pasipofikika na binadamu mwenye timamu hata kama ulifanya mangapi, na isitoshe hujawahi kumletea mwanamke humo ndani kwako hata siku moja. Hata hivyo nahisi huu Uzi umetunga kichwani hakuna reality. Maana kufikia kuuleta humu umechuja vya kutosha na kufikia hatua hii. Kwenye reality sitaki kuamini kama mwanaume utatendewa uchafu kama huo bado unaomba ushauri jinsi gani ufanye labda kama unaigiza unataka kupata hisia za wanaume wana react vipi
Sent from my PTM-Z-mini using JamiiForums mobile app
Unaonekana hauko serious pengine hizi ni drama za jfNataka mnipe ruksa ya kuuwa
Unaonekana hauko serious pengine hizi ni drama za jf
Sababu ya nyumba ndogo unakimbia watoto for weeks? Tunavuna tunayopanda. Ukijidanganya kulea mwenyewe hutawezaSijakuelewa
Sababu ya nyumba ndogo unakimbia watoto for weeks? Tunavuna tunayopanda. Ukijidanganya kulea mwenyewe hutaweza
Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
Rudi kwa Mungu wako ustadh au Kawaone wanasaikologia una tatizo kubwa sina ushauri,duh!Wana MMU leo mtashangaa sijaja nimelewa sana humu ndani, niko mtaratibu sana tofauti na siku nyingine. Ningelewa nadhani humu leo pasingekalika.
(Nilikua na mke) sijui kama bado ninae. Tangu siku naiacha familia yangu, kazi, heshima yangu mtaani na kazini, na ndani ya nyumba vimeporomoka kama ukuta wa tope ulionyeshewa mvua.
Mwaka 2016 mwezi wa tano nilianza kua na ukaribu na mfanyakazi mwenzangu kazini, ni binti huyo. Niliidanganya akili yangu kua sitoweza kuitelekeza family yangu kwa sababu yake lakini muda ukawa ni mwamuzi. Mahusiano yalianza na kushika kazi kiasi cha kuondoka nyumbani wiki 2 au tatu bila kutia mguu.
Huyu mwanamke nikiri aliichota akili yangu na ikachoteka. Alinijali sijpata kujaliwa na mke wangu kabla kama vile. Akanipa hadi na visivyotolewa. Family yangu muda huu ilishanililia vya kutosha, Ilikua ni swala la muda tu director wangu wa kazini kuanza kugundua madudu ya kazi zangu. Wafanyabiasha wako sensitive sana na kazi zao, baada ya miezi miwili tu "I was demoted at work".
Mshahara wangu uliporomoka zaidi ya nusu. Nyumbani ikawa siku nikirudi nataka wife anifanyie nilivyokua nafanyiwa na mwanamke yule (kunipa visivyopeka), Nakumbuka baada ya kama siku tatu mfululizo kunikatalia uchafu wangu nilimlazimisha nikambaka na kutimiza haja yangu na kutokomea kwa mchepuko.
Sauti ya kilio chako ule usiku haitokaa initoke akilini. Muda huo mapenzi na mdigo yalipungua zaidi ya punguzo la mshahara wangu. Nikawa simwelewi, anaweza kutoka usiku akaniacha nimelala akarudi asubuhi, nikiuliza anazua tafrani.
Kumbuka muda huo ni mwezi wa kumi niko na mdigo. Mapenzi na mdigo yalifika ukingoni nikaamua nirudi kwangu. Nikawa mtu wa mawazo sana kazini ndipo uchapombe ulipoanza. Hata kile kimshara kidogo nilichobakisha nakitumia kupiga ulabu. Nimepata sana ajali za pikipiki njiani usiku uso umejaa makovu. Muda si muda nikaona unyonge wa mama Yasi haupo tena na kapata ujasiri wa gafla, sikujali, nilichokua nawaza ni ulabu tu.
Siku moja nimelala chumbani kwangu usiku nimelewa ingawa akili yangu inafanya kazi nikasikia sauti ya kiume lounge ndani ya nyumba. Sikuweza kuamka nikafata yangu na tulishatengana na mama Yasi vyumba muda sana kumbuka. Asubuhi nikaamka kama kawaida kuelekea kazini natoka nje nakuta gari aina ya Range Vogue nje kwangu ndani ya geti langu. Nikapanda pikipiki yangu bila kufumbua mdomo wangu kuuliza aliyopo ndani. Jioni kama kawa piga ulabu rudi nyumbani nimejichokea hata kula sili.
Siku ya tatu leo naongea, nimeamka asubuhi nimeoga tayari chumbani kwangu natoka kuelekea kazini nakutana na jamaa kafunga taulo anaelekea bafu za public za familia ndani kwangu akitokea chumba analala mke. Simjui na sijawahi kumuona. Nikamwacha lakini niliamua walau niulize kinachoendelea kwa mama Yasi, niliingia bila hata kugonga chumbani mule na kumkuta akiwa kakaa kitandani. Kumuuliza kulikoni mwenzangu, nilichojibiwa ni kwamba.
"NIFUATE YANGU NIACHE KUFATILIA MAMBO YA WATU YATANITOKEA PUANI"
Nilipandwa na hasira nisijue cha kufanya, lakini baada ya kufikiri mawili matatu nikaamua niondoke nikaenda kujikomoa na ulabu sikwenda hata kazini. Jana na leo sijanywa hata tone la pombe natafakari cha kufanya.
Nimeona niwashirikishe wana MMU mnipe akili kwa sababu nahisi mwanamke kaondoka na akili zangu.
Pole baba Yasi Ushauri muombe mama yasi msamaha muendelee na life mpeane mauzoefu mliyoyapata katka michepuko
Nani?Somebody is spying me.