Mwanamke Avua Nguo Asikamatwe na DAWASCO

Mwanamke Avua Nguo Asikamatwe na DAWASCO

MaxShimba

Platinum Member
Joined
Apr 11, 2008
Posts
36,008
Reaction score
4,093
OPERESHENI ya kuwasaka wezi wa maji Dar es Salaam, juzi imechukua sura mpya baada ya mkazi wa Tandale Chama, wilayani Kinondoni ambaye ni mwanamke (jina tunalo), kuvua nguo zote.

Chanzo cha mwanamke huyo kuvua nguo ni baada ya kuuona msafara wa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Meck Sadiki na Maofisa
wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO), ambao walimkuta akiuza maji aliyojiunganishia kiholela.

Hata hivyo, Ofisa wa DAWASCO ambaye ni mwanamke alilazimika kumkamata na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi waliokuwa katika operesheni hiyo.

Operesheni hiyo ilifanyika kwenye eneo la Kagera, Tandale Chama, Mkwajuni na Bonde la Mkwajuni ambapo vifaa mbalimbali ambavyo vilikuwa vikitumika kuunganisha maji vilikamatwa.

Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Sadiki alisema operesheni hiyo imefichua mambo mengi yanayofanywa na wananchi aliowaita wahujumu uchumi kwa kujiunganishia maji kiholela bila kuyalipia.

Alisema asilimia 36 ya maji yamekuwa yakipotea kutokana na baadhi ya watu kujiunganishia kichume cha sheria.

“Leo kwa macho yangu nimeshudia wezi wawili katika oparesheni hii, nakuomba Mkuu wa Wilaya hii (Jordan Rugimbana), kesho mchana (leo), unikabidhi majina ya wezi wa DAWASCO .

“Wizi huu hauna tofauti na wauzaji dawa za kulevya hivyo
tuchukue hatua mapema kudhibiti hali hii,” alisema Bw. Sadiki na kuongeza kuwa, maji yanayopotea ni sawa na lita milioni 100.

Aliwagiza DAWASCO wajitazame upya kwa watendaji wake ambao wanalihujumu shirika hilo na kuweka mikakati ya kudhibiti tatizo hilo kwa kuunda chombo cha maadili ili watendaji wabovu wawajibishe.
 
Kuwa mwizi kweli kunahitaji uwe na guts!Mtu mzima na akili zake kuvua nguo hadharani sio mchezo!

Yaani mwanamama kadhania kwa kuchojoa nguo zote ndio serikali itaogopa laana yake na kuacha kumkamata? Sasa maungo yameonwa na kadamnasi na kesi ya wizi inamkabiri! Sote hela twaipenda ila kwa kuiba twaumiza wengine jamani!
 
ni maji yanapotea au mapato yanapotea ?sifikirii kuwa waliojiungia maji wame yaficha ndio maana kuna uhaba mkubwa wa maji-wajipange upya wafanye maji yapatikane kwa kila mtu tuone kama kutakuwa na 'opresheni kamata wizi wa maji'
 
wanakwepesha hoja ya mnyika kwa kuwasaka wezi.ccm kweli balaa.walikwepesha hoja ya mbatia kwa upande wa elimu kwa kuunda tume
 
Kesho kutwa Rais JK naye ataenda GOBA na UBUNGo kukamata wezi wa maji.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Wanamuone tu mwanamke mwenzangu lo kwani hawajui wahujumu uchumi wengi wapo sirikali kubwa sana?
 
big up but nashangaa mkuu wa mkoa kufanya hii kazi
badala ya polisi na dawasco.
kilichopo waboreshe miundombinu zaidi ya maji na sio kukamata wezi pekee
 
Hii operation bado inaendelea?
wale wenzangu na mie ambao mnakoishi hata hamjawahi kuona bomba la Dawasco mnapeta tu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
magembe akiwa na vazi la kuazima kwa Mwakyembe.
Ngoja tuone kama atamudu kushinda nalo!
 
OPERESHENI ya kuwasaka wezi wa maji Dar es Salaam, juzi imechukua sura mpya baada ya mkazi wa Tandale Chama, wilayani Kinondoni ambaye ni mwanamke (jina tunalo), kuvua nguo zote.

Chanzo cha mwanamke huyo kuvua nguo ni baada ya kuuona msafara wa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Meck Sadiki na Maofisa
wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO), ambao walimkuta akiuza maji aliyojiunganishia kiholela.

Hata hivyo, Ofisa wa DAWASCO ambaye ni mwanamke alilazimika kumkamata na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi waliokuwa katika operesheni hiyo.

Operesheni hiyo ilifanyika kwenye eneo la Kagera, Tandale Chama, Mkwajuni na Bonde la Mkwajuni ambapo vifaa mbalimbali ambavyo vilikuwa vikitumika kuunganisha maji vilikamatwa.

Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Sadiki alisema operesheni hiyo imefichua mambo mengi yanayofanywa na wananchi aliowaita wahujumu uchumi kwa kujiunganishia maji kiholela bila kuyalipia.

Alisema asilimia 36 ya maji yamekuwa yakipotea kutokana na baadhi ya watu kujiunganishia kichume cha sheria.

“Leo kwa macho yangu nimeshudia wezi wawili katika oparesheni hii, nakuomba Mkuu wa Wilaya hii (Jordan Rugimbana), kesho mchana (leo), unikabidhi majina ya wezi wa DAWASCO .

“Wizi huu hauna tofauti na wauzaji dawa za kulevya hivyo
tuchukue hatua mapema kudhibiti hali hii,” alisema Bw. Sadiki na kuongeza kuwa, maji yanayopotea ni sawa na lita milioni 100.

Aliwagiza DAWASCO wajitazame upya kwa watendaji wake ambao wanalihujumu shirika hilo na kuweka mikakati ya kudhibiti tatizo hilo kwa kuunda chombo cha maadili ili watendaji wabovu wawajibishe.

masikini mama wa watu!

hivi.....wale drug barons ambao hata JK alisema anawafahamu, wameishia wapi?
 
Je wale waliounganishwa na DAWASCO lakini wana Pump za umeme ambazo hujaza maji kwenye Simtank za lt hadi 10000 kwa siku, kwenye mtaa na kuuzia wenzao mtaani nao ni watu gani? kuna watu maeneo ya mwananyamala hospital wametajirika kwa kuwauzia wenzao maji ya DAWASCO wanayovuta kwa Pump. mtaa mzima wenye kaya zaidi ya 50 maji yanatoka nyumba moja tu kwa nini? Maji ya DAWASCO mtaani yanauzwa na hao wenye pump sh 200 hadi 100.
 
Wanaokamata wezi unatarajia nini mbaya na mafundi waliowaunganishia wako hapo lwenye msafara
 
Nonesense. Mkuu wa mkoa na ukidampa wa DAWASCO wapi na wapi?
 
Back
Top Bottom