Mwanamke anayekupenda kweli

Mwanamke anayekupenda kweli

ogmhillu

Member
Joined
Jul 24, 2017
Posts
87
Reaction score
71
Sio kazi ngumu sana kuelewa mwanamke anaekupenda kiukweli mwanamke anaekupenda kweli hawezi kukuomba wewe kitu chochote bali atachohitaji kutoka kwako sana sana ni muda wako na 'attention' yako kwake.

Hayo mengine kuhusu pesa, outing, shopping na mengineyo unatakiwa kujiongeza wewe kama mwanaume na sio kubweteka na kupendwa, kwa sababu mwanamke wako anahitaji matunzo vilevile.

Anachohitaji mwanamke ni wewe tu na muda wako. Wanawake wameumbwa na moyo 'strong' lakini katika suala la mapenzi na hisia wako 'sensitive' sana. Wanahitaji kupendwa na wanahitaji kuona akijaliwa.

Mwanamke akikupenda kweli kutoka moyoni mwake atahitaji awe na wewe muda mwingi, atakutext mara kwa mara, atakupigia simu every time when she feels she wants to talk to you.

Atakuwa kama mtoto mdogo anayehitaji kupendwa, kukumbatiwa, kubebwa na kutizamwa kwa umakini.

Mpende sana mwanamke wa aina hiyo, muda mwingine aweza kuwa anakufuatilia sana mpaka unajiuliza nina 'date' na shushushu ama nini? Ila unapaswa kutambua kuwa anakupenda kwa dhati na anataka ajihakikishie kuwa yupo peke yake kwako.

Ukipata mwanamke wa aina hiyo tulia, usimuumize wachana na mitambo mingine, utazunguka bucha zote lakini nyama ni ile ile sana sana utamaliza nauli yako na nguvu zako za kuzunguka kila bucha.
 
Pamoja na hayo mkuu kuna ule usemi kwamba 'ukipenda sanaa siku mkiachana utaumia sana' so pamoja na hayo ulioandika bado unapaswa kuwa makini pia
 
Sio kazi ngumu sana kuelewa mwanamke anaekupenda kiukweli. Mwanamke anaekupenda kweli hawezi kukuomba wewe kitu chochote bali atachohitaji kutoka kwako sana sana ni muda wako na 'attention' yako kwake.

Hivyo hivyo kwa mwanaume pia...
 
Sio kazi ngumu sana kuelewa mwanamke anaekupenda kiukweli. Mwanamke anaekupenda kweli hawezi kukuomba wewe kitu chochote bali atachohitaji kutoka kwako sana sana ni muda wako na 'attention' yako kwake.
Aya mawazo sio yako...naomba umpe credit zake bwana gabo msanii wa bongo movie...maana naona umecopy na kupaste kutoka katika ukurasa wake wa fb umeweka apa bila kuonesha..kua umechukua kwake acha wizi wa idea za watu...mpe sifa yake kwani ungesema umekopy ungekuaje...
 
Back
Top Bottom