Mwanamke anayekupenda huwa hivi

Mwanamke anayekupenda huwa hivi

Kuna kale ka usemi kanasema"huwezi kujua thamani ya anayekupenda mpaka atakapoenda kumpenda mtu mwigine " hilo ndilo linalokukuta sasa pambana na hali yako
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Asante mkuu ngoja nipambane haswaa
 
Sio kazi ngumu sana kuelewa mwanamke anaekupenda kiukweli. Mwanamke anaekupenda kweli hawezi kukuomba wewe kitu chochote bali atachohitaji kutoka kwako sana sana ni muda wako na 'attention' yako kwake.

Hayo mengine kuhusu pesa, outing, shopping na mengineyo unatakiwa kujiongeza wewe kama mwanaume na sio kubweteka na kupendwa, kwa sababu mwanamke wako anahitaji matunzo vilevile.

Anachohitaji mwanamke ni wewe tu na muda wako. Wanawake wameumbwa na moyo 'strong' lakini katika suala la mapenzi na hisia wako 'sensitive' sana. Wanahitaji kupendwa na wanahitaji kuona akijaliwa.

Mwanamke akikupenda kweli kutoka moyoni mwake atahitaji awe na wewe muda mwingi, atakutext mara kwa mara, atakupigia simu every time when she feels she wants to talk to you.

Atakuwa kama mtoto mdogo anayehitaji kupendwa, kukumbatiwa, kubebwa na kutizamwa kwa umakini. Mpende sana mwanamke wa aina hiyo, muda mwingine aweza kuwa anakufuatilia sana mpaka unajiuliza nina 'date' na shushushu ama nini?

Ila unapaswa kutambua kuwa anakupenda kwa dhati na anataka ajihakikishie kuwa yupo peke yake kwako.

Ukipata mwanamke wa aina hiyo tulia, usimuumize wachana na mitambo mingine, utazunguka bucha zote lakini nyama ni ile ile sana sana utamaliza nauli yako na nguvu zako za kuzunguka kila bucha.
Unatumia kinywaji gani?
 
huu uzi mbona unarudiwa sana?? au ndo msisitizo kwa wanaume?
 
Jiongeze..we mwanaume..manake kamic dyudyu
hapana nipo nae ofisi moja na nime date nae kwa wiki mbili lakin hatu kusex, baadae akasema kuwa tuachane, lakini kila siku alikuwa ana text mwisho wa siku nikampa vikwazo kama Trump hivi kuwa sitaki kuchat nae maana hatuongei kitu cha maana kwangu, but nikawa nimenunua simu ya WhatsApp mkuu ndio akaanza kunitumia text kwa watsap na ila mi nikamwambia msimamo wangu kuwa sitaki kuchat na wewe. Maana sioni kitu cha maana tunachat but Jana kani text ila nimekula kimya.
kwa sasa mi nipo likizo kwahyo hatuonani
 
Yaani nipate mwanamke wa hivyo halafu niwe peke yangu,hakika ntalitunza hilo penzi lakini siyo ile nina mpenzi hayo yote ananionyesha lakini ana mwanaume mwingine pia,hakika nikigundua naondoa upendo wangu kwa kiasi kikubwa nakubaki nao wa kawaida au namtema kabisa,sintataka hata kusikia maneno ya watu kua ananipenda mimi sana kuliko flani,sasa kama ananipenda mimi sana kwanini awe nasisi badala ya mimi tu?
 
Hayo yote yanapatika baada ya kuwa na pesa usijiongopee bure... Kama huwajui hawa watu wanaweza kaa hata mwaka wanakufanyia yote hayo siku wakianza kujilipa tutakuonea huruma ndugu.
 
Sio kazi ngumu sana kuelewa mwanamke anaekupenda kiukweli. Mwanamke anaekupenda kweli hawezi kukuomba wewe kitu chochote bali atachohitaji kutoka kwako sana sana ni muda wako na 'attention' yako kwake.

Hayo mengine kuhusu pesa, outing, shopping na mengineyo unatakiwa kujiongeza wewe kama mwanaume na sio kubweteka na kupendwa, kwa sababu mwanamke wako anahitaji matunzo vilevile.

Anachohitaji mwanamke ni wewe tu na muda wako. Wanawake wameumbwa na moyo 'strong' lakini katika suala la mapenzi na hisia wako 'sensitive' sana. Wanahitaji kupendwa na wanahitaji kuona akijaliwa.

Mwanamke akikupenda kweli kutoka moyoni mwake atahitaji awe na wewe muda mwingi, atakutext mara kwa mara, atakupigia simu every time when she feels she wants to talk to you.

Atakuwa kama mtoto mdogo anayehitaji kupendwa, kukumbatiwa, kubebwa na kutizamwa kwa umakini. Mpende sana mwanamke wa aina hiyo, muda mwingine aweza kuwa anakufuatilia sana mpaka unajiuliza nina 'date' na shushushu ama nini?

Ila unapaswa kutambua kuwa anakupenda kwa dhati na anataka ajihakikishie kuwa yupo peke yake kwako.

Ukipata mwanamke wa aina hiyo tulia, usimuumize wachana na mitambo mingine, utazunguka bucha zote lakini nyama ni ile ile sana sana utamaliza nauli yako na nguvu zako za kuzunguka kila bucha.
Sweet manka miss Chaga toa neno hapa maana dunia imechafuka[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
daaarr ume ongea ki2 kuntu,,, itx strong poit dear,,, waeleze hao wasio jua umuhimu wa mwanamke jinsi anavyo penda,,, umenikoshaa sana,, nikimpata atakaye jali hisia zaNgu nitamganda kama ruba,, lakini nyie waanaume kwenye 200 wapo 9,,, daaarrr hongera sana kwa kulitambua hilo,, ckujua kuwa wapo wanaoume wanao lijua hilo ila ww ni mmoja wapo,,, Big Up my dear
Unaonesha ukipenda unakuwa deep sana eeh...Well jiangalie lakini mapenzi yakizidi kuna haya:
1.Unazidisha wivu wa kijinga na kumpangia ME masharti ya kuishi utaachwa tu.
2.Unaanza mashauzi ya kitoto km kuringa kupokea simu utaachwa tu.
3.Unapenda kujikweza na maigizo utaachwa tu.
4.Unapenda kuomba omba hela af mvivu utaachwa tu.

Kama katika hayo juu haupo basi njoo p.m kwa ushauri juu ya kuacha kuumizwa.
 
Yaani nipate mwanamke wa hivyo halafu niwe peke yangu,hakika ntalitunza hilo penzi lakini siyo ile nina mpenzi hayo yote ananionyesha lakini ana mwanaume mwingine pia,hakika nikigundua naondoa upendo wangu kwa kiasi kikubwa nakubaki nao wa kawaida au namtema kabisa,sintataka hata kusikia maneno ya watu kua ananipenda mimi sana kuliko flani,sasa kama ananipenda mimi sana kwanini awe nasisi badala ya mimi tu?
Hio ndio inanishindaga tu kwa hawa dada zetu, anaweza kawa anakupenda ila ndio mama huruma. Kila anaebisha hodi twende kazzz...
 
Back
Top Bottom