Mwanamke ananitosa kila anapopata kazi

Mwanamke ananitosa kila anapopata kazi

Mi naona tatizo liko kwako mleta mada
Huyu binti kakusoma na kujua we ni mtu wa namna gani. Anajua unampenda sana na atakalotaka huwezi kufurukuta. Ila kukuchunia mara ya kwanza ilitosha kukupa somo. Kama ikitokea ukamrudia sasa hivi ujue umekwisha na utakuwa ujinga usio na mfano. Wasichana wapo wengi wanaoweza kukupenda ni kwanini mawazo yako yamefungwa unamuona huyo tu. Sikushauri kumrudia huyo msichana. Msalimie lakini wala usiombe game na wala kuonyesha interest ajue kuwa nawe umechoka mambo yake. La sivyo ukamrudia huyu binti tegemea kuendeshwa kama gari bovu.
 
sasa wewe unataka umsaidie kwa lip na unajua kabisa unapendwa akiwa hana....
 
Ndivyo walivyo ndugu yangu, msichana atakutafuta kipindi ana shida tu, akiwa hana shida na wewe hutomsikia tena, labda kama anakupenda walau unaweza ambulia hata SMS

Ndivyo walivyo hata usiwashangae, mfano mkiwa school kama una akili class msichana atakuganda mno full kukutumia SMS, ila mkienda likizo hakukumbuki hata robo mpaka uanze wewe tena anaweza asiwe na response nzuri
 
Habarini,

Hivi mwanamke anapokutosa kila apatapo kazi na kurudiana na wewe kila anapopigwa chini maana yake ni nini?
Maana yake wewe ni bwege au labda kakufananisha na bwege.

Nimeongea kwa lugha ya picha, kama ufafanuzi ukihitajika nitatoa.
 
Una roho ngumu, mtu unaona kabisa hakupendi we umekomaa nae tu
 
naona unauliza vitu ambavyo viko wazi kabisa.......af muda wote unaambulia kiss au.....we kweli sijui...haya ngoja watakushauri maanami naona kilakitu wazini akili yako kujiongeza
 
Back
Top Bottom