Mwanamke amlazimishia mwanaume ngono hadi kumtoa ulimi

rpg

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Posts
3,620
Reaction score
1,480

Kijana mmoja mkazi wa Kimandolu jijini Arusha, Paulo Simon (18) amelazwa hospitali ya mkoa Mount Meru, baada ya kubakwa na kisha kukatwa ulimi na mwanamke mmoja aliyekuwa akimtaka kimapenzi.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia Jumanne majira ya saa 6.30 katika eneo la Tindigani, Kimandolu, wakati mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina moja la mama Abuu alipofika katika baa hiyo kama mteja na baadae kumlazimisha mhudumu wa baa hiyo kufanya mapenzi bila ridhaa yake.

Simoni ambaye ni mfanyakazi katika baa hiyo, inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Mtaa, Joel Mbasha, alisema mnamo majira usiku alikuja mwanamke huyo na kuagiza kinywaji na kumuhudumia.

Alisema ilipotimu majira ya saa 6.30 wateja waliisha na kuamua kufunga baa, hata hivyo mwanamke huyo alieendelea kunywa pombe taratibu katika eneo la kaunta.

"Mimi sikuwa na mazoea kabisa na mwanamke huyo kwanza ukimwangalia ni kama mama yangu,wakati nikifunga baa na kujaribu kuondoka alinifuata na kuniambia anataka tukafanye mapenzi nilimkataa ndipo aliponishika kwa nguvu sehemu zangu za siri," alisema.

Alisema alipatwa na maumivu makali na kuanza kupiga kelele ,ambapo mwanamke huyo aliendelea kumng'anga'nia sehemu zake za siri huku akimziba mdomo kwa kutumia kinywa chake na baadae alifanikiwa kumng'ata ulimi na kuutema chini.

"Alipoona napiga kelele akaleta mdomo wake kwenye mdomo wangu akanishika kichwa na kuniingizia mdomo wake huku mkono wake mmoja ameshika sehemu zangu za siri nilikuwa nasikia maumivu makali sana wakati nalia ndipo alipofanikiwa kuning'ata ulimi na kuondoka nao kisha aliutema karibu na mlango wa baa," alisema.

Majeruhi huyo kwa sasa hali yake bado si nzuri kwani hawezi kuzungumza na muda mwingi anatokwa na damu nyingi hali iliyosababisha wauguzi katika hospitali anayotibiwa kumuwekea ndoo kutema damu.

Jeshi la polisi mkoani Arusha limethibitisha tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
 
Mwingine ni upungufu wa akili sio hisia za mapenzi. Sheria itafuata mkondo nadhan huyo mama akafungwe kwenye jela ya wanaume nadhan watamsaidia kumwondolea hamu
 
mbona kawaida sana... mwenzake ana genye afu yy anataka kuremba? angenyofolewa mdomo kabisa..
 
Mwingine ni upungufu wa akili sio hisia za mapenzi. Sheria itafuata mkondo nadhan huyo mama akafungwe kwenye jela ya wanaume nadhan watamsaidia kumwondolea hamu

Yaani wakamtupe kwenyesero yamasela tu mpuuzi sana huyo
 
Naona huyu kichwani mwake alihisi huyo mama ameathirika.. ndo maana akawa mgumu kukubali kubakwa.. Ila mhh katuangusha wanaume.. Mbinu zote za medani ameshindwa kulitegua bako..!
 
Kijana mmoja mkazi wa Kimandolu jijini Arusha, Paulo Simon (18) amelazwa hospitali ya mkoa Mount Meru, baada ya kubakwa na kisha kukatwa ulimi na mwanamke mmoja aliyekuwa akimtaka kimapenzi.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia Jumanne majira ya saa 6.30 katika eneo la Tindigani, Kimandolu, wakati mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina moja la mama Abuu alipofika katika baa hiyo kama mteja na baadae kumlazimisha mhudumu wa baa hiyo kufanya mapenzi bila ridhaa yake.

Simoni ambaye ni mfanyakazi katika baa hiyo, inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Mtaa, Joel Mbasha, alisema mnamo majira usiku alikuja mwanamke huyo na kuagiza kinywaji na kumuhudumia.

Alisema ilipotimu majira ya saa 6.30 wateja waliisha na kuamua kufunga baa, hata hivyo mwanamke huyo alieendelea kunywa pombe taratibu katika eneo la kaunta.

“Mimi sikuwa na mazoea kabisa na mwanamke huyo kwanza ukimwangalia ni kama mama yangu,wakati nikifunga baa na kujaribu kuondoka alinifuata na kuniambia anataka tukafanye mapenzi nilimkataa ndipo aliponishika kwa nguvu sehemu zangu za siri,” alisema.

Alisema alipatwa na maumivu makali na kuanza kupiga kelele ,ambapo mwanamke huyo aliendelea kumng’anga’nia sehemu zake za siri huku akimziba mdomo kwa kutumia kinywa chake na baadae alifanikiwa kumng’ata ulimi na kuutema chini.

“Alipoona napiga kelele akaleta mdomo wake kwenye mdomo wangu akanishika kichwa na kuniingizia mdomo wake huku mkono wake mmoja ameshika sehemu zangu za siri nilikuwa nasikia maumivu makali sana wakati nalia ndipo alipofanikiwa kuning’ata ulimi na kuondoka nao kisha aliutema karibu na mlango wa baa,” alisema.

Majeruhi huyo kwa sasa hali yake bado si nzuri kwani hawezi kuzungumza na muda mwingi anatokwa na damu nyingi hali iliyosababisha wauguzi katika hospitali anayotibiwa kumuwekea ndoo kutema damu.

Jeshi la polisi mkoani Arusha limethibitisha tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

We ndio muongo kabisa,,,,sasa bila ulimi itakuwaje sasa? Umepata nguvu ya kuingia hadi JF
 
Duuuu hatare huyo nae kwanini asingevaa ndomu akampa kitu basi yaishe qay ya bure imekuja analeta za kuleta.
 
Huyu jamaa aliyenyofolewa ulimi hakutumia akili kumkwepa huyu ji-mama. Mwanamke kama humtaki na amekubana kona, usitumie nguvu. Mimi ilishawahi kunitokea, kwanza nilimkubalia, wakati wa kujiandaa nikajifanya nakwenda uwani, ikawa kimoja.
 
kuna watu hapa wanatamani wabakwe wao na mijimama kila siku ila holaaa!!!!!!
 
Kijana mmoja mkazi wa Kimandolu jijini Arusha, Paulo Simon (18) amelazwa hospitali ya mkoa Mount Meru, baada ya kubakwa na kisha kukatwa ulimi na mwanamke mmoja aliyekuwa akimtaka kimapenzi.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia Jumanne majira ya saa 6.30 katika eneo la Tindigani, Kimandolu, wakati mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina moja la mama Abuu alipofika katika baa hiyo kama mteja na baadae kumlazimisha mhudumu wa baa hiyo kufanya mapenzi bila ridhaa yake.

Simoni ambaye ni mfanyakazi katika baa hiyo, inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Mtaa, Joel Mbasha, alisema mnamo majira usiku alikuja mwanamke huyo na kuagiza kinywaji na kumuhudumia.

Alisema ilipotimu majira ya saa 6.30 wateja waliisha na kuamua kufunga baa, hata hivyo mwanamke huyo alieendelea kunywa pombe taratibu katika eneo la kaunta.

“Mimi sikuwa na mazoea kabisa na mwanamke huyo kwanza ukimwangalia ni kama mama yangu,wakati nikifunga baa na kujaribu kuondoka alinifuata na kuniambia anataka tukafanye mapenzi nilimkataa ndipo aliponishika kwa nguvu sehemu zangu za siri,” alisema.

Alisema alipatwa na maumivu makali na kuanza kupiga kelele ,ambapo mwanamke huyo aliendelea kumng’anga’nia sehemu zake za siri huku akimziba mdomo kwa kutumia kinywa chake na baadae alifanikiwa kumng’ata ulimi na kuutema chini.

“Alipoona napiga kelele akaleta mdomo wake kwenye mdomo wangu akanishika kichwa na kuniingizia mdomo wake huku mkono wake mmoja ameshika sehemu zangu za siri nilikuwa nasikia maumivu makali sana wakati nalia ndipo alipofanikiwa kuning’ata ulimi na kuondoka nao kisha aliutema karibu na mlango wa baa,” alisema.

Majeruhi huyo kwa sasa hali yake bado si nzuri kwani hawezi kuzungumza na muda mwingi anatokwa na damu nyingi hali iliyosababisha wauguzi katika hospitali anayotibiwa kumuwekea ndoo kutema damu.

Jeshi la polisi mkoani Arusha limethibitisha tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

alikua amelala ama???? alishindwa kukidefend Kabisaaa yan??????
 
Back
Top Bottom