Mwanamke aliyeitawala nyumba

kibovu

JF-Expert Member
Apr 17, 2017
661
686
Ndugu wana Jamvi poleni na majukumu,

Napenda mmshauri rafiki yangu kwa haya yanayoendelea katika mahusiano yake.Rafiki yangu ni mtendaji aliekuja masomoni kujiendeleza jijini Dar es Salaam. Siku moja akiwa ameenda kwenye harusi alikutana na msichana wakaanzisha mahusiano.

Msichana huyo anasoma chuo nae hapa jijini Dar es Salaam. Walianzisha mahusiano yao na msichna alikuwa anaishi kapanga Kinondoni mwanaume anaishi hostel.

Baada ya miezi sita za mahusiano yao dada alimuomba amlipie kodi huyo mwanaume akapigana akalipa kodi kwa mazumuni ya wawili hao kuishi pamoja.
Walihamia Sinza chumba na sebule master walikuwa wanalipa laki 9 kwa miezi sita.

Katika maisha yao ya kuishi pamoja kunasiku huyo dada alikuwa akimueleza wanakuja rafiki zake wa kike na hivo arudi hostell mara moja kiukweli jamaa alikuwa akifanya hivo lakini ilifikia mwisho alimzibiti huyo dada na kuanza huyo dada kuwakwepa rafiki zake wanaotaka kuja kutembea geto kwake.

Huyu dada anapenda sana kuiserch simu ya mpenzi wake na akiona namba tu ya mwanamke ni razima aifute.Jamaa kwa upande wake hapendi kumfatilia hivo vitu. Siku tano zilizopita kuna dada mmoja anasoma nae alimpigia huyo jamaa ilikuwa mida ya saa nne usiku jamaa akiwa anaoga yule dada aliipokea ile simu na kusema unasemaje mshenzi.

Kiukweli jamaa hakuipenda ile tabia alimueleza mkewe but mkewe alimjibu kwa mwanamke yeyote atakae piga usiku nitapokea.

Huyu mwanaume akikutana na rafiki yake wa kike hata chuo akipiga nao picha mwanamke ataongea sana, yeye akipiga picha jamaa hanashida.

Tokea aanze mahusiano na jamaa anamuhudumia kila kitu japokuwa wazazi wake walifariki but anaishi na kaka yake pia ana dada zake wenye kazi alishamuambia kaka yake sintakutaka hela ya matumizi tena.

Kunasiku walikuwa katika mazungumzo huyo dada alimueleza mume wangu nikianza kazi itanibidi niwe natuma kila mwezi laki moja nyumbani kwa kaka inayobaki ndo tunapanga matumizi.

Tukio la Leo ambalo ndilo jamaa ananiomba ushauri nikaona niwashilikishe wazee wenzangu tumshauri ushauri uliotukuka.

Kuhusu mgegedo jamaaaa mpaka amuombe tena sana mara anyimwe kwa kukadilia hupewa kama mara nne. Wanachumba self but mwanamke anapenda kuchemshiwa maji na kupikiwa pamoja na kufuliwa nguo hayo mambo nimemshauli wiki mbili zilizopita sasa hivi hayafanyi.


Leo wameamka asubuhi kitandani mnamo saa moja asubuhi baada ya kuamka yule mke wake akamueleza kwa nini jana ulichukia nilipo zifuta namba za hao wasichana?

Jamaaa alimjibu kwa upole mke wangu nimekupa uhuru wa kushika simu yangu unapoona chochote kibaya niulize sio ufute tu mke wake kwa hasira akamuambia chukua namba zao hizi hapa nilikuwa nimezisave kwenye simu yangu.

Jamaa akazichukua baada ya kuzichukua mwanamke akaanza kulia jamaa akaanza kumbembeleza msichana akaamka akaenda akaosha vyombo akaoga jamaa akaenda kuangalia kama kunamaji ndani akakuta hamna akaenda bombani akachochota akaoga alipoanza kupaka mafuta mke wake akiwa sebuleni akasikia anamuambia naenda nyumbani jamaa hakumjibu.

Jamaaaa anaomba mumshauri je ampigie simu kumuuuliza chochote na anafaa kuwa mke.
 
Akikubali hiyo hali iendelee atajuta sana na itamfanya ashindwe kutimiza majukumu yake. The best way ni kuachana na huyo dada kwa sasa bila kupoteza muda maana atamuharibia mwelekeo wa maisha. Given kwamba hawajaoana na hawana mtoto mida wa kufanya maamuzi ni sasa maana akisubirj kimojawapo ya hivyo kitokee ni jambo linaloweza kimgharimu maisha yake yote.

Inavyoonekana huyo demu hampendi ila amemkubali ili aweza kutatua matatizo yake. Msaidoe mwenzio afunguke akili sasa hivi la sivyo atakuwa amechelewa. Atafuta mwanamke anayejielewa waanzishe mahusiano na siyo wa namna hiyo.
 
Duh mpe pole Sana lakn Kama nkweli hayo yote hapo jamaa atakuja kuteseka Sana mbeleni mwanamke ambaye anataka uwe chini yake hafai kabsaa
 
wakati nasoma kulikuwa na methali isemayo . mtoto umleavyo nduvyo akuavyo . sasa hoyu jamaa yako asubili mkewe akue ndo atajua nini afanye.
 
ndugu wana Jamvi poleni na majukumu. Napenda mmshauri rafiki yangu kwa haya yanayoendelea katika mahusiano yake.
Rafiki yangu ni mtendaji aliekuja masomoni kujiendeleza jijini dar és salaam. Siku moja akiwa ameenda kwenye harusi alikutana na msichana wakaanzisha mahusiano.

Msichana huyo anasoma chuo nae hapa jijini dar és salaam.
Walianzisha mahusiano Yao nã msichna alikuwa anaishi kapanga kinondoni mwanaume anaishi hostel.
Baada ya miezi sita za mahusiano yao dada alimuomba amlipie kodi huyo mwanaume akapigana akalipa kodi kwa mazumuni ya wawili hao kuishi pamoja.
Walihamia sinza chumba na sebule master walikuwa wanalipa laki 9 Kwa miezi sita.
Katika maisha Yao ya kuishi pamoja kunasiku huyo dada alikuwa akimueleza wanakuja rafiki zake wa kike na hivo arudi hostell mara moja kiukweli jamaa alikuwa akifanya hivo lakini ilifikia mwisho alimzibiti huyo dada na kuanza huyo dada kuwakwepa rafiki zake wanaotaka kuja kutembea geto kwake.

Huyu dada anapenda Sana kuiserch cm ya mpenzi wake na akiona namba tu ya mwanamke ni razima aifute.
Jamaa kwa upande wake hapendi kumfatilia hivo vitu.

Siku tano zilizopita kuna dada mmoja anasoma nae alimpigia huyo jamaa ilikuwa mida ya saa nne usiku jamaa akiwa anaoga yule dada aliipokea ile cm na kusema Unasemaje mshenzi .Kiukweli jamaa hakuipenda ile tabia alimueleza mkewe but mkewe alimjibu kwa mwanamke yyte atakae piga usiku Ntapokea.

Huyu mwanaume akikutana na rafiki yake wa kike hata chuo akipiga nao picha mwanamke ataongea Sana, Yeye akipiga picha jamaa hanashida.

Tokea aanze mahusiano na jamaa anamuhudumia kila kitu japokuwa wazazi wake walifariki but anaishi na kk yake pia ana dada zake wenye kazi alishamuambia kk yake sintakutaka hela ya matumizi tena

Kunasiku walikuwa ktk mazungumzo huyo dada alimueleza mume wangu nikianza kazi itanibidi niwe natuma kila mwezi laki moja nyumbani kwa kaka inayobaki ndo tunapanga matumizi.

Tukio lá Leo ambalo ndilo jamaa ananiomba ushauri nikaona niwashilikishe wazee wenzangu tumshauri ushauri uliotukuka. Kuhusu mgegedo jamaaaa mpaka amuombe tena Sana mara anyimwe kwa kukadilia hupewa kama mara nne. Wanachumba self but mwanamke anapenda kuchemshiwa maji na kupikiwa pamoja na kufuliwa nguo hayo mambo nimemshauli wiki mbili zilizopita sasa hivi hayafanyi


Leo wameamka asubuhi kitandani mnamo saa moja asubuhi Baada ya kuamka yule mke wake akamueleza kwa nini jana ulichukia nilipo zifuta namba za hão wasichana? jamaaa alimjibu kwa upole mke wangu nimekupa uhuru wa kushika cm yangu unapo ona chochote kibaya niulize sio ufute tu mke wake kwa hasira akamuambia chukua namba zao hizi apa nilikuwa nimezisave kwenye cm yangu jamaa akazichukua baada ya kuzichukua mwanamke akaanza kulia jamaa akaanza kumbembeleza dem akaamka akaenda akaosha vyombo akaoga jamaa akaenda kuangalia kama kunamaji ndani akakuta hamna akaenda bombani akachochota akaoga alipoanza kupaka mafuta mke wake akiwa seblem akasikia anamuambia e naenda nyumbani jamaa hakumjibu





Jamaaaa anaomba mmshauli je ampigie cm kumuuuliza chochote na anafaa kuwa mke.
Anapewa mara 4 kila baada ya muda Gan mkuu
 
Yan baada ya kunipa namba za watu aliowasave hlf anaanza kulia ningepiga makofi huyo mwanamke mpk angejuta kunifahamu
 
Mbona kama unapenda kutawaliwa ila ni vile marafiki zako wanakuingilia ktk maisha yako binafsi na mpenzi wako!!
Wewe kama unaridhika na kutawaliwa basi ni heri tu muendelee kuishi.

Kuhusu kukufaa wewe ndio unajua kama anakufaa au la,na kama haujui basi muda wako wa kuoa na kuitwa mume bado.
 
Kwanza kabisa amuacge aende zake pili atafute namna ahame hapo alipopanga na apange mbali na hapo,,asimuulize kitu Hugo demu,,demu akitaka kurudi amwambie asbiri atamwambia maana kuna wanafunzi wenzake wamekuja kumtembelea,,akimuuliza VP mbona amehama amwambie ameamua tuuu,,atajirekebisha mwenyewe,,
 
Kwanza haya majanga ni yako Mtoa Uzi wala usimsingizie nsela,pili mpige chini huyo demu sio mke mwema utakuja kujuta
 
Mleta uzi inabidi asikilize huo wimbo ndio ataelewa.

Kunguru wafananao upaa pamoja. Hizo ni hisia kali zinakuendesha ila si mke huyo
Hata hivyo mpaka sasa inaonekana huyo mwanaume ana udhaifu. Anataka kumuonyesha huyo mke wake wema ila hajui ndo anajitengenezea jeneza.

Pia inaonyesha anaweza kukumbwa na tatizo hilo hata akiingia kwenye mahusiano mengine. Wanawake ni kama watoto. Atajaribu kitu kidogo ukikubali wakati hupendi imejimaliza maana siku nyingine ukikataa hatakuelewa. Sasa leo anajaribu hiki na kesho kile na unakubali mwishowe yanakuwa mengi ambayo hutaweza kuyahimili. Mwishowe ndoa inakuwa utumwa sasa. Huyo jamaa asipolotambua hilo mahusiano yake yatamletea downfall siyo kwa huyu mpenzi wa sasa tu hata kwa wengine. Labda itokee apate mwanamke muelewa kitu ambacho hata hivyo ni nadra sana bila ya yeye kutambua nafasi yake.
 
Acha kuingilia mambo ya watu.... Kama mwenzako anaosheshwa vyombo na haoni shida. Usimshtue....!

Pambana na hali yako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom