Mwanamke aliyeasi dini Sudan aponea KIFO!

Mwanamke aliyeasi dini Sudan aponea KIFO!

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
ImageUploadedByJamiiForums1403547793.140300.jpg Mwanamke aliyehukumiwa kifo nchini Sudan kwa kuasi dini ameachiliwa huru.
Wakili wake Elshareef Ali, ameambia BBC kuwa mwanamke huyo aliyekiuka dini kwa kuolewa na mwanamume mkristo aliachiliwa huru Jumatatu

Hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya Meriam Ibrahim,ilibatilishwa na mahakama ya rufaa, kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan Suna.

Meriam ameolewa na mwanamume mkristo na alihukumiwa kifo na mahakama ya kiisilamu kwa kosa la kuasi dini, baada ya kukata kukana kuwa yeye ni mkristo.

Hukumu dhidi yake ilichochea viongozi wa kimataifa walioilaani wakisema inakiuka haki za binadamu.
 
Vita yako na nani?

Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho 'Waefeso 6: 12'
 
Back
Top Bottom