Mwanamke ajioa mwenyewe baada ya kukosa mume

Mwanamke ajioa mwenyewe baada ya kukosa mume

Dr Matola PhD

Platinum Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
62,589
Reaction score
112,309
Yasmin Eleby hakupata mchumba wa kumuoa mtu ambaye alitaka awe mume wake atakapofikisha miaka 40--kwa hivyo akafanya kitendo ambacho kimewashangaza wengi, aliamua kujioa mwenyewe.

Kwa mujibu wa mtandao wa My SanAntonio.com,Eleby aliahidi kwamba ikiwa hatapata mchumba wakati atakapokuwa ametimiza miaka 40, basi atafanya harusi ya mtu mmoja yaani atajioa ili kusherehekea miaka yake 40.

Duru zinasema kuwa mwanamke Eleby alifanya harusi yake mwenyewe katika makavazi ya Houston akiambatana na jamaa na familia yake na wageni wengine waalikwa.

Kwa sherehe hii, dadake Eleby ndiye aliendesha sherehe hio, kwani ni kinyume na sheria kwa mtu kujioa mwenyewe. Harusi ya kawaida ni kati ya watu wawili.

Katika picha za kanisani sherehe ilionekana kuwa ya kawaida bila ya mchumba.
Kulingana na John Guess Jr afisa mkuu wa makavazi hayo, sherehe hiyo ilionekana kuwa bila tashwishi na kuonekana kama jambo la kawaida kwani makavazi hayo huwakumbatia watu wa jinsia mbali mbali kuendesha harusi zao hapo.

Aliposikia kwamba Eleby, ambaye anaishi na kufanya kazi ugenini alikuwa anapanga kujioa mwenyewe, aliharakisha kwenda katika eneo hilo kujionea mwenyewe.

"Eleby alipofikisha umri wa miaka 40 bila ya kupata mpenzi na mtu mwenye nia ya kumuoa, aliamua angejioa mwenyewe,''alisema Guess Jr ambaye anasema harusi hiyo imewashangaza wengi na kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii.

Anasema anakubaliana na Eleby na mtazamo wake wa mapenzi kwamba mtu anaweza kujipenda na kujioa kwa kukosa wa kumuoa kwani cha muhimu ni mtu kujipenda kwanza kabla ya kupendwa.
"watu wengu huolewa bila ya kutafakari mara mbili kuhusu yule anayemuoa, '' Guess Jr alisema.

Anadhani kwamba pindi watu watakapomuona Eleby anavyojishughulikia mwenyewe, huenda akapata ushindani.
"ni mrembo, anafanya kazi kwa bidii na anasifika duniani na pia anaona uamuzi wake umewapa gumzo watu wengi. ''
 
Mkuu Matola nilipoiona hii nikabaki nacheka tu, kumbe kwa baadhi kuolewa ni muhimu. Mrembo kakosa wa kumuwowa kaamua kujiwowa mwenyewe. Kazi kweli kweli! Sasa kajiwowa mwenyewe ili iweje?
 
Last edited by a moderator:
Afu mkuu kama sijakupata vizuri vile!!!! ngoja nivae mawani yangu huenda nikaelewa.
 
Haina tofauti na sherehe ya kujifanyia birthday.

Wanawake huwa wanajikaza kama they
don't care kuhusu kuolewa lakini inawaumiza.
 
Hongera zake kwakufanya maamuzi magumu, kajipunguzia stress hahahaha.

pls nomba usiniquote
 
Mkuu Matola nilipoiona hii nikabaki nacheka tu, kumbe kwa baadhi kuolewa ni muhimu. Mrembo kakosa wa kumuwowa kaamua kujiwowa mwenyewe. Kazi kweli kweli! Sasa kajiwowa mwenyewe ili iweje?
Jibu lako msome hapa chini Viol
Haina tofauti na sherehe ya kujifanyia birthday.

Wanawake huwa wanajikaza kama they
don't care kuhusu kuolewa lakini inawaumiza.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo inapoitwa ndoa si sahii, huo ni uhuni sawa na ule ufanywao na watu wa jinsi moja.
Naamini tafsiri ya ndoa inaeleweka. Period
 
Hahahahaaaaaaa! Nisimtukanemamba mie bado mto sijauvuka.
 
Mkuu Matola nakumbuka tar 1 January, 2015 uliianza hii kampeni ya kuwahimiza dada zetu nikadhani ni utani, kumbe upo serious
 
picha wapi sasa

Mkuu Matola nakumbuka tar 1 January, 2015 uliianza hii kampeni ya kuwahimiza dada zetu nikadhani ni utani, kumbe upo serious
Mkuu hapa wala hakuna utani, wanaomsikiliza Mange kujitongozesha kwa Matajili arobaini yao iko njiani.

Anayetaka picha muhusika ni huyu hapa.
 

Attachments

  • 1422465379095.jpg
    1422465379095.jpg
    5.1 KB · Views: 1,083
Afu mkuu kama sijakupata vizuri vile!!!! ngoja nivae mawani yangu huenda nikaelewa.
HAHAAAA. MKUUU HADINAHUKUU HUÈLEWI HILI NI TATIZOKUBWA KWA MWL WAKO WA VIDUDU NILIJUA PDIDY SASA FUNGUA UFAHAMU NAANZAKUKUELEKEZAYAANIALIMAANISHA. KUNABINTIAMETAFUTA MUTUWAKUMUWOWWAAAA AMEKOSA KAAMUAAKUJIWOOOWAAAMWENYEWEEKAMAAWEEEMUTUWABUKOBAAAAUNAELEWAKULIKONINAEANDIKA,,,,SOFARBADONAJIUHURIZAAA ATJINANIIIMWENYEWEE?? MKUUMATOLA HIYOCHAMTOTONAONAMOJA KWENYENET JAMAQYAKEKALAKONA SIKUYAHARUDIDEMUKAENDACHURCH KATOKANAMAMAMETI WAKE WAKAEREKEAKWA PARTY WAKATIWAKEKIII AKAOMBAALISHWEENAMAMAYAKE THENN RANGIZA NYUMBAWALIWEKAKWENYEMABOMBA WAKAANZAKUMIMINIAAALOHANGENIONYESHABANKSTATEMENTYAKE NINGEHUDHURIAHATAKANISANITUGELESHA,,MKUUU USIOPOEREEAHAPA HIRIII NITATIZOLaMwalmkuu formfour akuwanakufwatiria revoyetu inaishiahapa kukuerekezazaid cc c Maasaidada(inrrlationship),faizerfoxy(not known) erisi njoo mrimani jioni nipm nikirekereze
 
Mkuu hapa wala hakuna utani, wanaomsikiliza Mange kujitongozesha kwa Matajili arobaini yao iko njiani.

Anayetaka picha muhusika ni huyu hapa.
Mpwahiikazi yawapii??alpha alpha sierra Rodger/
 
HAHAAAA. MKUUU HADINAHUKUU HUÈLEWI HILI NI TATIZOKUBWA KWA MWL WAKO WA VIDUDU NILIJUA PDIDY SASA FUNGUA UFAHAMU NAANZAKUKUELEKEZAYAANIALIMAANISHA. KUNABINTIAMETAFUTA MUTUWAKUMUWOWWAAAA AMEKOSA KAAMUAAKUJIWOOOWAAAMWENYEWEEKAMAAWEEEMUTUWABUKOBAAAAUNAELEWAKULIKONINAEANDIKA,,,,SOFARBADONAJIUHURIZAAA ATJINANIIIMWENYEWEE?? MKUUMATOLA HIYOCHAMTOTONAONAMOJA KWENYENET JAMAQYAKEKALAKONA SIKUYAHARUDIDEMUKAENDACHURCH KATOKANAMAMAMETI WAKE WAKAEREKEAKWA PARTY WAKATIWAKEKIII AKAOMBAALISHWEENAMAMAYAKE THENN RANGIZA NYUMBAWALIWEKAKWENYEMABOMBA WAKAANZAKUMIMINIAAALOHANGENIONYESHABANKSTATEMENTYAKE NINGEHUDHURIAHATAKANISANITUGELESHA,,MKUUU USIOPOEREEAHAPA HIRIII NITATIZOLaMwalmkuu formfour akuwanakufwatiria revoyetu inaishiahapa kukuerekezazaid cc c Maasaidada(inrrlationship),faizerfoxy(not known) erisi njoo mrimani jioni nipm nikirekereze

Cc: Heaven on Earth
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom