Mwanajeshi kortini madai mauaji ya askari mwenzake

Mwanajeshi kortini madai mauaji ya askari mwenzake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Praiveti Pascal Lipita (28), anayefanya kazi katika wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha 843 Nachingwea, mkoani Lindi, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.

Lipita (28) anatuhumiwa kumuua askari mwenzake, Praiveti Baserisa Ulaya kwa kile kinachodaiwa kuwa wivu wa kimapenzi.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa huo, Maria Batulaine, na kusomewa shtaka linalomkabili.

Mwanasheria wa Serikali, Abdulrahman Mohamed, alidai kuwa askari hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kwamba wivu ndio unaodaiwa kusababisha mauaji hayo.

Mwanasheria huyo wa serikali alidai kuwa mshtakiwa alifanya mauaji hayo Februari 10, mwaka huu, majira ya Saa 12;00 jioni wakiwa kambi ya Nang’ondo.

Alidai kuwa siku hiyo ya tukio, wakiwa kambini hapo, mshitakiwa akiwa na silaha, alimmiminia askari mwenzake risasi 19 kisha kuchakaza mwili wake na kumkatisha uhai.

“Baada ya kumpiga risasi moja na kuanguka chini, mshtakiwa aliendelea kummiminia zingine mwili wote na kumpotezea uhai wake,” alidai Mohamed.

Mwanasheria huyo alidai kuwa kutokana na kitendo hicho, mshtakiwa alifanya kosa chini ya kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 marejeo mwaka 2002.

Hata hivyo mshtakiwa hakutakiwa kukubali wala kukataa mashtaka yanayomkabili kwa kuwa mahakama hiyo kisheria haina mamlaka ya kusikiliza kesi zinazohusu mauaji.

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka hayo, alipelekwa rumande na atafikishwa tena mahakamani Machi 2, mwaka huu, kesi itakapotajwa.

Chanzo Nipashe
 
Madhara ya kupenda bila tahadhari. Unawezaje kuweka moyo wako kwa mwanadamu mwenzako na kusahau kwamba, binadamu huweza kubadilika muda wowote. Hata maandiko matakatifu yameonya juu ya kuweka tumaini kwa mwandamu.

Binadamu yoyote anapaswa kuweka tumaini lake kwa Mungu muumba wa mbingu na dunia na vyote vilivyomo, tofauti na hapo ni maumivu tu.
 
Mapenzi yana-run dunia aisee. Juzi kati nimeshikiwa kisu na mwanamke almanusura anitoe utumbo nje kwa kisu kama nisingekuwa nimepitia mafunzo ya kujihami. Niliwaza mno siku hiyo ikabidi niachane na mapenzi kabisa kwa sasa.

Tahadhari katika mahusiano ni suala muhimu sana.
 
Kupenda mwanamke ni sawa na.kupanda bodaboda na kuweka matumaini yako na uhai wako kwa muhuni
 
Wanaume wenzangu aka mabaharia epukeni kuweka silaha kama bastola, visu, mapanga, mashoka, bunduki, sime n.k vyumbani mwenu kwa kisingizio kuwa mwizi akiingia utamkabiri. Siku mkizinguana na mkeo silaha hizo hizo ndio zitatumika kutoana uhai na mwenzi wako. Bora muweke mlango wa dharula ukisikia wezi wanavunja unatoka unakimbia.

Kifo cha huyo dada mjeda kimesababishwa na silaha kuwa karibu yao
 
Ulivyoachana na Mapenzi sasa hivi unajishughulisha na nini?
Mapenzi yana-run dunia aisee. Juzi kati nimeshikiwa kisu na mwanamke almanusura anitoe utumbo nje kwa kisu kama nisingekuwa nimepitia mafunzo ya kujihami. Niliwaza mno siku hiyo ikabidi niachane na mapenzi kabisa kwa sasa.

Tahadhari katika mahusiano ni suala muhimu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuanzie hapa waliom-miminia Lissu lisasi 38 hawakuwa Ma soja.
Napita tu..
 
Back
Top Bottom