Mwanajeshi kortini madai mauaji ya askari mwenzake

Mwanajeshi kortini madai mauaji ya askari mwenzake

Kupenda mwanamke ni sawa na.kupanda bodaboda na kuweka matumaini yako na uhai wako kwa muhuni
Ndio mtupende kwa akili tena muwe na akili za ziada sio za kushikiliwa.... Tatizo mnatupenda kumoyo...... Moyo kazi yake kusukuma Damu.....
 
Madhara ya kupenda bila tahadhari. Unawezaje kuweka moyo wako kwa mwanadamu mwenzako na kusahau kwamba, binadamu huweza kubadilika muda wowote. Hata maandiko matakatifu yameonya juu ya kuweka tumaini kwa mwandamu. Binadamu yoyote anapaswa kuweka tumaini lake kwa Mungu muumba wa mbingu na dunia na vyote vilivyomo, tofauti na hapo ni maumivu tu.
Jamaa lofa kweli. Utauaje mpenzi kama mapenzi hayapo kwako?
 
Askari wa JWTZ Wilayani Nachingwea, Lindi Pascal Lipita(28), amefikishwa Mahakamani akituhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi Askari mwenzake ambaye ni Mpenzi wake Baserisa Ulaya, chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa huo Maria Butulaine, Pascal anadaiwa kummiminia risasi 19 Mpenzi wake huyo na kumsababishia kifo wakiwa kwenye kambi ya Nang’ondo,Nachingwea.

Mshtakiwa amerejeshwa rumande na atarudi tena Makamani March 02, 2020 kesi itakapotajwa.

mapenzi mabayaa...mapenzi mabayaaaa...
 
Mapenzi yana-run dunia aisee. Juzi kati nimeshikiwa kisu na mwanamke almanusura anitoe utumbo nje kwa kisu kama nisingekuwa nimepitia mafunzo ya kujihami. Niliwaza mno siku hiyo ikabidi niachane na mapenzi kabisa kwa sasa.

Tahadhari katika mahusiano ni suala muhimu sana.
Ulifanyeje hadi ukashikiwa kisu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaume wenzangu aka mabaharia epukeni kuweka silaha kama bastola, visu, mapanga, mashoka, bunduki, sime n.k vyumbani mwenu kwa kisingizio kuwa mwizi akiingia utamkabiri. Siku mkizinguana na mkeo silaha hizo hizo ndio zitatumika kutoana uhai na mwenzi wako. Bora muweke mlango wa dharula ukisikia wezi wanavunja unatoka unakimbia.

Kifo cha huyo dada mjeda kimesababishwa na silaha kuwa karibu yao
Uwe unasoma kabla ya kucomment akipigwa kambini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio raha ya risasi yaani ukipiga moja unajisikia kuzimimina tuu
 
Uwe unasoma kabla ya kucomment akipigwa kambini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimesoma vizuri kisa ila nimetoa tahadhari niliwahi kuwa na silaha ya moto ndani na pia niliwahi kumtolea wife tulipozinguana tena jambo dogo tu.

Hayo masilaha kuyamiliki au kuyabeba beba kuna sababisha unatamani kuyatumia sasa kwa kuwa hamna watu wa kukuzingua mtaani siku mkeo akizingua analo
 
Back
Top Bottom