Mwanahisa wa Jamii Media, Micke William aunganishwa katika kesi mbili zinazomkabili Maxence Melo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,962
13,735
Habari wakuu,
Baada ya sekeseke la Maxence Melo mahakamani, leo mwanahisa mwingine Jamii Media, Micke William anatarajiwa kupandishwa kizimbani muda si mrefu.

Mnamo Januari 16 aliitwa na kuhojiwa kituo cha polisi cha kati jijini Dar na kupata dhamana ya polisi.

Habari zaidi kufuata...

IMG_2650.JPG

UPDATES:

Micke William ameunganishwa kwenye kesi mbili za kuzuia Upelelezi wa Jeshi la Polisi zinazomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo.

Amefanikiwa kupata dhamana kwa mashitaka yote mawili.

Upelelezi umekamilika kwa shitaka moja na Usikilizaji wa awali wa kesi unaanza Tarehe 9 Februari 2017.
=======

Tazama mjadala kuhusu habari hii ukisomwa katika
kipindi cha JamiiLeo

 
Yani wanaruka taasisi serikalini wanatumia .com wanakimbilia watu binafsi, kwanini watu wasifikiri ni kesi ya kisiasa? Mawaziri wana tovuti binafsi zinazotumia .com etc. Alafu unazuia .com wakati dunia nzima ni habari ya mjini. Tuna safari ndefu sana. Na vipi kwa jirani zetu Kenya ambao wamo humu, watapendezwa na kutumia .co.tz?
 
Ee Mungu tunusuru na mabalaa haya kwani tunakutumainia wewe katika shida na taabu na sasa tuokoe na utulinde dhidi ya mikono dhalimu ya watesi wetu.
 
Back
Top Bottom