MMAHE
JF-Expert Member
- Feb 14, 2012
- 815
- 420
Mwanaharakati mmoja anayefahamika kwa jina la Mohamed Namtande anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35, mkaazi wa kijiji cha Mihambwe kilichopo halmashauri ya Tandahimba mkoani Mtwara, amefariki dunia katika hospitali ya Ligula mkoani Mtwara.
Akizungumza na Pride fm Katibu wa Chama cha Wananchi CUF wilaya ya Mtwara, Said Issa Kulaga amesema kuwa, Mohamed Namtande maarufu kama Awilo amefariki leo majira ya saa 11 alfajiri katika hospitali ya Ligula baada ya kuwa hapo kwa takriban siku 3 kufuatia kujeruhiwa katika ajali ya gari akiwa katika harakati za kupinga gesi kusafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam.
Kulaga amesema kuwa, anatoa taarifa kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara, Lindi na Tanzania kwa ujumla kufuatia kifo hicho cha Awilo ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kupinga gesi asilia kupelekwa jijini Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu Mohamed Namtande unatarajiwa kuhifadhiwa katika makazi ya milele, hapo kesho majira ya saa nne asubuhi katika kijiji cha Mihambwe.
Kuhusu utaratibu wa kuhudhuria mazishi hayo, mwananchi mmoja amejitolewa usafiri huku mtu anayetaka kushiriki katika mazishi hayo anatakiwa kuchangia mafuta shilingi 3,000 huku mchango huo ukiwasilishwa katika ofisi za CUF, kituo kikuu cha mabasi dukani kwa Ndinda na soko kuu kwa Namdimba na waweza kutuma mchango kupitia 0653 183 169. Safari kuelekea mazishini itaanzia kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani majira ya saa 10 alfajiri na magomeni.
Inna lillah wa Inna Illah Rajiun!