MwanaHalisi laivua nguo Tume ya Uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MwanaHalisi laivua nguo Tume ya Uchaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Oct 12, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Leo gazeti la MwanaHalisi limeanika madudu yaliyofanywa na Tume ya Uchaguzi (NEC) katika daftari la wapiga kura wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga.

  Sehemu husika (relevant paragraphs) za habari hiyo ni kama ifuatavyo:

  Tume ya uchaguzi (NEC) yaweza “kutiwa kitanzini” iwapo itathibitika kuwa ilichakachua daftari la wapiga kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Igunga, MwanaHalisi limeelezwa.

  Taarifa kutoka ndani ya serikali, NEC na mashirika huru ya uangalizi wa uchaguzi nchini, zinaonyesha kwamba idadi ya wapigakura waliomo katika daftari la mwaka 2010 na wale waliotajwa katika uchaguzi mdogo wa Igunga inapishana, tena kwa mbali…………….

  ………..Kuna taarifa za kuondoa majina ya wapiga kura, kuongeza majina yaw engine na kuonekana, angalau kwa namba moja ya shahada isiyokuwa na jina mbele………

  ………………..MwanaHalisi limetarifiwa kuwa kazi ya kuingiza wapigakura hewa na kuondoa baadhi ya majina imefanyika kwa ustadi mkubwa, kwa kuhusisha NEC na wataalam wenye ujuzi katika mawasiliano ya kompyuta (IT).

  Taarifa zinaonyesha kwenye Kata ya Mbutu peke yake, wapigakura zaidi ya 2500 waliongezwa kwenye daftari hilo kwenye uchaguzi mdogo wa Igunga. Jimbo hilo lina jumla ya kata 26.

  Kwa mujibu wa uchunguzi wa MwanaHalisi, daftari la wapiga kura lilitumika kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana (2010) linaonyesha wapigakura waliopo kwenye kituo cha Shule ya Msingi Mwakabima C, kata ya Mbutu, ni 382, lakini daftari lililotolewa na NEC kwa vyama vyote vya siasa katika uchaguzi mdogo wa Igunga, limetaja wapigakura 393 kwa kituo hicho.

  Daftari hilo la wapiga kura 382 lilitolewa na NEC 18 Oktoba 2010.

  Kwenye kituo hiki peke yake, daftari linaonyesha ongezeko la wapigakura 11, wakati ambapo NEC haikuwahi kufanya marekebisho yeyote kwenye daftari la wapigakura kati ya 23 Septemba 2010 na 10 2010, wala wakati wa kuelekea uchaguzi mdogo wa Igunga.

  NEC inasema katika maelezo yake yaliyo mbele ya daftari hilo, “Daftari hili litatumika kuanzia 15 Oktoba 2010 hadi itakapotangazwa vinginevyo na Tume ya Uchaguzi.”

  Kati ya wakati huo na sasa NEC haijatangaza kusitishwa kwa matumizi ya daftari hilo.

  Aidha kwenye kituo cha Mwambakima Shule ya Msingi 3 chenye Na. 00015059, idadi ya wapigakura imeongezeka kutoka 393 waliotajwa na NEC 18 Oktoba 2010 hadi wapigakura 419 waliotajwa kwenye uchaguzi mdogo wiki iliyopita………….

  Habari zaidi katika MwanaHalisi la leo.


  My take:

  Jee NEC wataeleza nini hapa? NEC ni taasisi inayotaka kuleta machafuko hapa nchini, maana haikujifunza kutoka kwa ile Tume ya Kenya mwaka 2007.

  Ewe Mwenyezi Mungu tunusuru tunakokwenda.
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ipo siku nchi itakapokombolewa hawa jamaa lazima wapande kizimbani kujibu mashitaka wasidhani CCM wanayoibeba itakaa madarakani milele
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu, nimeisoma hiyo habari na kupandisha hasira kuona jinsi NEC walivyofanya madudu ili CCM ishinde Igunga. Ni bora NEC ikavunjwa na iundwe upya, na kama mwaka 2015 NEC hii hii ya akina Kiravu itakuwapo na kusimamia uchaguzi huo, basi serikali ya CDM ikishaingia madarakani imnyonge kwa kitanzi huyo Kiravu na wenzake pale Coco Beach!

  Wauwaji wakubwa hawa kutokana na hako kamchezo kao!
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Sasa nimeelewa kwa mapana zaidi DR SLAA huwa anamaanisha nini anaposema
  Kwanza, Serikali na CCM ndio wanaowalazimisha wao kufanya mambo wasiyoyataka (Maandamano)
  Pili, Wanafanya kazi kubwa sana kupunguza dhamira ya wananchi kutumia nguvu ya UMA.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kuna haja ya Chadema kusimaa Mahakamani kutaka haki haya si mambo ya kuvumiliwa then wanasema wameshinda hahaha CCM ndugu zanguni .
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wadau, hivi hamna namna kwa akina Tundu Lissu kwenda mahakamani kuzuia kuapishwa kwa Kafumu bungeni mwezi ujao hadi NEC itoe tamko la bila kuuma maneno kwa nini walifanya madudu hayo? Kwa kiasi gani cha pesa?

  Mimi nafikiri Watz angalau bado wana imani na mahakama na inaweza kuzuia kuapishwa kwa Kafumu.

  Naomba CDM walifanyie kazi hili.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  Mkuu Lunyungu mpaka hapo nchi yetu itakapokuwa na tume huru ya uchaguzi na siyo hii tume ya uchaguzi ya magamba, basi chaguzi zetu zitaendelea kutokuwa huru na zilizojaa wizi wa hali ya juu. CCM hawakushinda Igunga bali walitumia mbinu mbali mbali ikiwemo vitisho, rushwa na hata wizi ili kuhakikisha hawalipotezi jimbo la Igunga.

  Nina wasiwasi kama kweli tutapata katiba mpya ambayo inakubaliwa na Watanzania wengi na tume huru ya uchaguzi kabla ya uchaguzi wa 2015.
   
 8. F

  FUSO JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,878
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  YES, You can do this today, but you will NEVER do it forever.
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hapana, anyanyuliwe mzima mzima na kutundikwa shingoni kwenye ndoana za buchani huko maeneo ya Manzese! Hivi hawa jamaa wanatambua ni Watanzania wangapi wanaweza kupoteza maisha kwa ushenzi wao huu?
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Halafu mtaona, hawa jamaa wa NEC watauchuna tu badala ya kujibu tuhuma nzito za madudu yao hayo. Ukija uchaguzi mwingine mdogo watajifanya kama haya ya Igunga hayakutokea!

  Hebu zungumzeni NEC -- at least this once. Mnaweza hata kukiri kwamba "Sorry, tulikuwa tunaandikisha wapigakura Igunga baada ya uchaguzi mwaka jana na tulidhani tuliwatangazia watu wote kumbe hatukufanya hivyo."

  Angalau tusikie sauti zenu tu -- hata ile ya kawaida ya kusema "Kubenea ni mzushi na tunampeleka mahakamani kesho."
   
 11. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Una utani ww, umenifurahisha kwa mawazo yako, sasa hivi nipo coco ,atanyongewa wapi, dawa yake afungwe jiwe atoswe baharini wanahatarisha sana amani hawa NEC
   
 12. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Naamini CDM Legal team inacompile data na soon Nec itatakiwa kuwajibu watanganyika mahakamani

  NEC ni kampuni ya chama cha ccm na hata kaimu Mwenyekiti mteule Prf.naona amekubali kuudhalilisha uprof wake
   
 13. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ngoja ninyamaze kwanza, nina hasira naweza kula ban ya mwaka!! NEC na CCM hawatufai karne ya 21.
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hivi sisi watanganyika tutalialia mpaka lini jamani wanaua, wanaiba, wanalipa mabilioni kama siyo matrioni aahhhh lianzishwetu tu wangoe hawa maheyawani....
   
 15. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nadhani maji yalikuwa marefu Igunga wakamua kufanya hata yale ambayo ni ngumu kuficha ukweli wake. Chadema walifanyie kazi hili. Haya ndo matunda ya chadema kuwabana pale Igunga. Chadem wakikomaa na Tume kwa umafia huu walioufanya, uchaguzi wa Igunga ni batili.
   
 16. N

  Noel Kwai Member

  #16
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuendako naona giza
   
 17. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hii ya kutundika kwenye ndoano za buchani....some creativity in torture techniques.
   
 18. Gobegobe

  Gobegobe JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama haya yana ukweli (naamini ni kweli) vyma vilivyoshiriki uchaguzi vitakiwa kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi. Wakati huo huo nadhani ni vyama kwa vyama vya upinzani kuhimiza mchakato wa mabadiliko ya Katiba ili walau uchaguzi ujao ufanyike kwa misingi ya Katiba mpya, vinginevyo tutaendelea kulizwa kwa staili hii kila uitwapo uchaguzi.
   
 19. K

  KIBONGOMKUTI JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 1,415
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Duh kumbe leo nimegundua kuwa NEC ni NATIONAL ENSLAVING COMPANY
   
 20. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 940
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  ccm na tume yao ya uchaguzi kiama chao kinakaribia kwani siku zote chenye mwanzo siku zote huwa na mwisho.
   
Loading...