Mwanahalisi fanya yafuatayo

london

JF-Expert Member
Sep 12, 2010
221
143
Ndugu zangu MwanaHalisi kuvunjika kwa pakacha si mwisho wa uchukuzi. Nashauri yafuatayo ili mwendelee kutuhabarisha:
1. Fanya MwanaHalisi liwe linachapishwa mtandaoni tu kwa sasa kwani zuio la serikali ni kwa ajili ya print tu. Habri zenu mziwekee mafaili ya pdf ili tuwe tunaweza kuchapisha nakala.
2. Fungua blog kupitia marafiki waliopo nje ya nchi ili lisibanwe na sheria zinazosigina haki ya vyombo vya habari, ili mwendelee kutuhabrisha.
3. Geuzeni gazeti lenu la michezo la Mseto liwe la habari za kawaida/makala ama kwa kuliongezea kurasa za mwanzo na nyingine kuliwekea habari za michezo km kawaida.
4. Ombeni Jamii Forums iwape space ambayo mtaweka link yenu tuwe tunalipata kupitia humu.
5. Mnaweza kuanzisha gazeti jingine kwa jina jipya labda mkaliita HabariHalisi
 
Niliposoma title yako nilifikiri Unaipa USHAURI WA kiusalama salama ili wafunguliwe, Kumbe huu......Good idea.
 
Ntalimiss sana gazeti hili makini. Naomba wahusika wa mwanahalisi (kubenea na wenzako) angalieni ushauri huu km mnaweza kuufanyia kazi kiukweli mimi kila jumatano ni lazima niondoke ofisini mpaka ntakapomaliza kusoma gazeti la mwanahalisi.nikisoma nilikuwa nashiba kwa habari nzito na makini. Mwanahalisi wametutoa matongotongo na kutupa mwanga kuhusu ufisadi n a mafisadi.tutakuwa nanyi pamoja. Km gazeti lilikuwa ndio kipato chenu napendekeza uje uwekwe utaratibu wa kuwachangieni hapa jf ili muendelee kuhudumia watoto wenu pamoja na kuwahudumia watz. Serikali inajitakia laana yenyewe kwa kufungia gazeti pendwa zaidi nchini
 
Au kama mwanahalisi yeyote yuko umu,atumie nafas hiyo kupost mavituz ili kutujuza wadanganyika wenzao!
 
Wazo zuri mdau. Kwa kuongezea kabla hawaja tumia gazeti la Mseto kama mbadala wa Mwanahalisi wafanye matangazo ya majuma mawili au hata mwezi mmoja mfululizo halafu siku ya kuhamishia idea za mwanahalisi kwenye mseto ufanyike uzinduzi babu kubwa na mgeni rasmi awe Dr Ulimboka au miongoni mwa wanafamilia ya Dr Ully.
 
Ndugu zangu MwanaHalisi kuvunjika kwa pakacha si mwisho wa uchukuzi. Nashauri yafuatayo ili mwendelee kutuhabarisha:
1. Fanya MwanaHalisi liwe linachapishwa mtandaoni tu kwa sasa kwani zuio la serikali ni kwa ajili ya print tu. Habri zenu mziwekee mafaili ya pdf ili tuwe tunaweza kuchapisha nakala.
2. Fungua blog kupitia marafiki waliopo nje ya nchi ili lisibanwe na sheria zinazosigina haki ya vyombo vya habari, ili mwendelee kutuhabrisha.
3. Geuzeni gazeti lenu la michezo la Mseto liwe la habari za kawaida/makala ama kwa kuliongezea kurasa za mwanzo na nyingine kuliwekea habari za michezo km kawaida.
4. Ombeni Jamii Forums iwape space ambayo mtaweka link yenu tuwe tunalipata kupitia humu.

Wazo lako ni zuri. Ambapo linaonesha una mapenzi kiasi gani kwa gazeti hili. Tatizo tu ni kwamba kufanya unavyopendekeza kutaligeuza MwanaHalisi kuwa Charity organization kama WikiPedia, na sidhani kama Kubenea na wenzake wanataka kulifanya gazeti lao kuwa Charity organization. Ukifanya say copy 90,000 kwa wiki mara 500/- ni mihela mingi sana hata ukiondoa operating costs kama pesa za mawakala bado weekly income inavutia sana. Upande wa Business wa mwanahalisi ninavyoona mimi unaelekeza Kubenea ashuke tu kidogo na kubembeleza serikali imwachie. Nimewahi kusikia watu wanasema Serikali hii ni sikivu sana watamwachia tu.

Ingawa panaweza pakahitajika political pressure kidogo kutoka mashirika ya taaluma ya habari--au hata vyama vya siasa.
 
Hata alielifungia hakupenda lifungiwe amini usiamini, pale lumumba gazeti hilo lilikuwa linanunuliwa sana, Ngoja ifike kesho ndio tutaona umuhimu wa hilo gazeti kutokuwepo, naamini watalifungulia wenyewe tu ndio maana wamesema muda usiojulikana yaweza kuwa wiki mbili zijazo, Chezea CCM wewe
 
Wazo lako ni zuri. Ambapo linaonesha una mapenzi kiasi gani kwa gazeti hili. Tatizo tu ni kwamba kufanya unavyopendekeza kutaligeuza MwanaHalisi kuwa Charity organization kama WikiPedia, na sidhani kama Kubenea na wenzake wanataka kulifanya gazeti lao kuwa Charity organization. Ukifanya say copy 90,000 kwa wiki mara 500/- ni mihela mingi sana hata ukiondoa operating costs kama pesa za mawakala bado weekly income inavutia sana. Upande wa Business wa mwanahalisi ninavyoona mimi unaelekeza Kubenea ashuke tu kidogo na kubembeleza serikali imwachie. Nimewahi kusikia watu wanasema Serikali hii ni sikivu sana watamwachia tu.

Ingawa panaweza pakahitajika political pressure kidogo kutoka mashirika ya taaluma ya habari--au hata vyama vya siasa.

Ntapingana na wewe.....kunradhi kwa hilo.........hapa kinatakiwa ni continuity na si sustainability.....siungi mkono hili la kubembeleza kwa kuwa litawapa masharti magumu na kupoteza umaana wa MWANAHALISI.........yaani wageuke kuwa UHURU-2?
 
SASA kubenea anaona haya tunayomshauri?? ingefaa watu wa kwanza kumsaidia ni jamii forumz hebu tumsaidieni mwana habari bora wetu huyu
 
Mwanahalisi mjue tunaopenda ukombozi wa fikra tunataabika kuwakosa fanyeni kila linalowezekana tusiwakose. Serikali mnajidangaya kulifungia Mwanahalisi ni sawa na kulifunika jua kwa kuchoma moshi, Lakini Satelaiti mtazifungia?.
 
Gazeti la Mwanahalisi lafungiwa
• Kubenea atoa kauli, wadau wa habari waja juu

na Happiness Mnale
Tanzania Daima

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelifungia gazeti la Mwanahalisi kwa muda usiojulikana, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutokana na mwenendo wake wa kuandika habari na makala za uchozezi.

Kwa mujibu wa serikali, sababu nyingine ya kufungiwa kwa gazeti hilo ni pamoja na kujenga uhasama na uzushi, likiwa na nia ya kusababisha wananchi wakose imani na vyombo vya dola, hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa nchi.

Akisoma tamko la serikali lililotolewa na Msajili wa Magazeti jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (MAELEZO), Phabian Lugaikamu, alisema kuwa katika toleo la gazeti hilo namba 302, 303 na 304 ya mwaka 2012 na mengine yaliyotangulia yalichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.

"Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi ameitwa na kuonywa mara nyingi lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii, pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari," alisema.

Aidha, alisema kuwa mhariri huyo mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha Katiba ya nchi kinachotoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutokunukuu kifungu cha 30 cha Katiba hiyo hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru wa kutoa maoni.

"Serikali imeamua kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa muda usiojulikana kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976, kifungu namba 25(i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai, 2012 kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 258 lililochapishwa katika gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dar es Salaam Julai 27, 2012," alisema.

Aidha, serikali imewataka wamiliki, wahariri na wanahabari kuzingatia sheria, uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari ili kutekeleza wajibu wa kuhabarisha, kuelimisha na kutoa burudani kwa wananchi.

Aidha, Lugaikamu alisema kuwa serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari ambavyo vitatoa taarifa za uchochezi ambazo zitahatarisha hali ya amani na utulivu.

Saed Kubenea atoa kauli
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwanahalisi Communications inayochapisha gazeti la Mwanahalisi na gazeti dada la michezo la Mseto, Saed Kubenea, alisema kuwa ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha kwani kisheria mashitaka ya uchozezi ni ya jinai, hivyo serikali kama ilikuwa na ushahidi ilitakiwa ilipeleke Mwanahalisi mahakamani.

Kubenea alisema hakuna haja ya kuogopa serikali (^^^^^), kwani kama ina hoja ni vema iende mahakamani ili aamuliwe mshindi nani, na kuachana na tabia ya kuendesha shughuli zake kwa kuvizia.

"Serikali ikae kimya iandikwe, kulifungia Mwanahalisi kwa habari iliyoandikwa itaonekana inakiri na inaogopa kusemwa ukweli," alisema.
CUF yatoa tamko, Lissu awaka bungeni
Wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya afya mjini Dodoma jana, Mnadhimu Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Tundu Lissu, alitumia nafasi hiyo kuishambulia serikali na kutaka iachane na sheria kandamizi dhidi ya vyombo vya habari.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, alisema serikali isije kudhani kutumia mabavu kwa vyombo vya habari kutasaidia kuficha maovu yake na kutaka uhuru wa vyombo vya habari upewe kipaumbele.

Jukwaa la Wahariri waja juu
Baadhi ya wadau wa habari akiwamo Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Neville Meena, alisema kuwa kitendo cha kulifungia gazeti la Mwanahalisi hakikubaliki, huku akihoji aliyelifungia ni nani na kwa utaratibu upi, kwa kipi na waziri anatoa wapi maamuzi ya kulifungia.

Meena pia alisema mfumo mzima una matatizo kwani mtu mmoja hawezi kutoa maamuzi na mahali pekee penye haki ni mahakamani, kwani ndipo sehemu watu wanapopambana na kupatikana aliyesimama kwenye haki.

"Hakuna haki wala uhuru wa habari, tunataka haki itendeke kwa wanaoandikiwa na wanaoandika, tutajuaje kama makosa waliyofungiwa yana ukweli na unasema tunalifungia muda usiojulikana ndiyo nini? Ungefuatwa utaratibu wa mahakama," alisema.

Meena pia alisema TEF wanatarajia kutoa tamko leo kuhusiana na jambo hilo.

Mhariri Tanzania Daima aguswa
Naye Mhariri Mtendaji wa gazeti hili, Absalom Kibanda, alisema taarifa za serikali kulifungia gazeti hilo zilivuja na jambo hilo haliingii akilini kwani taifa limekuwa likizungumzia uhuru wa kujieleza.

Kibanda pia alisema kuwa sheria zilizopo ni kandamizi na kulifungia gazeti hilo ni hatua nyingine ya kukandamiza na kutishia, ikiwamo kuwanyima wanahabari haki yao na maelfu ya wananchi kupata habari kupitia Mwanahalisi.

"Kwanini wasitoe maelezo kuhusu Mwanahalisi lilifanya nini kuhusiana na kile kilichokuwa kikiandikwa? Mimi naona hata serikali haikuzingatia weledi, ikiwamo kutoa ufafanuzi na kwa stahili hii nasema Mwanahalisi iliigusa serikali pabaya," alisema Kibanda.

Pia aliitaka serikali kutoingilia uhuru wa habari, ikiwamo kutambua gharama za demokrasia, isiinyime mawazo na kutambua kuwa ukinzani wa mawazo ndipo kwenye maendeleo.

TAMWA nao wacharuka
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake, Ananilea Nkya, alieleza kupitia mtandao wa mabadiliko kuwa hatua hiyo ya serikali ya kulifungia gazeti la Mwanahalisi badala ya kwenda mahakamani ni ishara kwamba yaliyoandikwa na gazeti hilo ni ukweli mtupu.

"Labda niulize swali moja tu, hivi mfalme akiambiwa yuko uchi, kama hajawa uchi ni kwa nini aamue kumuua/kumwadhibu aliyemwambia yuko uchi kabla ya yeye mfalme kuthibitisha kuwa hajawa uchi?," alihoji.

Ndugu zangu MwanaHalisi kuvunjika kwa pakacha si mwisho wa uchukuzi. Nashauri yafuatayo ili mwendelee kutuhabarisha:
1. Fanya MwanaHalisi liwe linachapishwa mtandaoni tu kwa sasa kwani zuio la serikali ni kwa ajili ya print tu. Habri zenu mziwekee mafaili ya pdf ili tuwe tunaweza kuchapisha nakala.
2. Fungua blog kupitia marafiki waliopo nje ya nchi ili lisibanwe na sheria zinazosigina haki ya vyombo vya habari, ili mwendelee kutuhabrisha.
3. Geuzeni gazeti lenu la michezo la Mseto liwe la habari za kawaida/makala ama kwa kuliongezea kurasa za mwanzo na nyingine kuliwekea habari za michezo km kawaida.
4. Ombeni Jamii Forums iwape space ambayo mtaweka link yenu tuwe tunalipata kupitia humu.
5. Mnaweza kuanzisha gazeti jingine kwa jina jipya labda mkaliita HabariHalisi

Lete pia mapendekezo ya namna atakavyokuwa analipwa kwa kutuletea habari za kiuchunguzi. Mimi niko tayari kuchangia.
 
Back
Top Bottom