Mwanafunzi wa shule ya sheria aiomba mahakama isimamishe mafunzo

John7371

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
2,994
6,641
Mmoja wa wanafunzi walioathirika na matokeo katika Taasisi ya mafunzo ya Sheria kwa Vitendo (LST), Alexander Barunguza ameiomba mahakama iizuie shule hiyo kuendelea na mafunzo kwa muda ili kufanya uchunguzi wa mazingira ya kujifunzia na kuzuia ubadhirifu.

Barunguza, ambaye pia amefungua kesi Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) na nyingine ya kikatiba Mahakama Kuu, katika kesi hizo anapinga uamuzi wa taasisi hiyo kutupilia mbali rufaa yake ya kupinga matokeo yaliyoonesha kuwa ameshindwa kufaulu somo moja hata baada ya kulirudia.

Wakati kesi ya kikatiba inayosikilizwa na jopo la majaji watatu, Dk Deo Nangela, Ephery Kisanya na Dk Theodora Mwenegoha ilipotajwa Ijumaa iliyopita, ndipo alipowasilisha ombi la zuio la muda la shule hiyo kuendelea kutoa mafunzo hayo.

Barunguza alieleza kuwa anaomba amri hiyo ya zuio la muda ili kuzuia ubadhirifu na uharibifu wa rasilimali za umma, ikiwemo bajeti inayotengwa kila mwaka Sh4 bilioni kwa ajili ya kuboresha mafunzo hayo.

Alidai kuwa tangu chuo hicho kianze kimekuwa na mazingira yasiyo rafiki kwa kutokuwepo hosteli za wanafunzi watokao mikoani na hivyo kusababisha vijana hao kushindwa kufikia hatima yao ya kitaaluma ya kulitumikia taifa.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Stanley Kalokola alipinga hoja hizo pamoja na mambo mengine akidai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri hiyo kwa kuwa inakaa kama mahakama ya kikatiba
Katika shauri hilo la kikatiba namba 11 la mwaka 2022, Barunguza anapinga matokeo ya mitihiani yake ya muhula wa kwanza na wa pili mwaka 2019/2020 ambayo alishindwa kufikisha alama za ufaulu katika kozi mbili.

Pia anapinga kanuni na taratibu za rufaa akisema ni kinyume cha Katiba na kwamba katika mchakato wa rufaa yake iliyotupiliwa mbali na LST hakupewa haki ya kusikilizwa.

Vilevile anadai kuwa haki zake za kuishi na usalama zimekiukwa au zinaelekea kukiukwa kutokana na kutishiwa maisha na mmoja wa walimu chuoni hapo baada ya kukata rufaa kupinga matokeo hayo, huku akidai kutengwa, kubaguliwa na kutokutambuliwa kama mwanafunzi.

Katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki mwanafunzi huyo amefungua mashauri mawili, moja anapinga taratibu za kukata rufaa chuoni hapo ili kupinga matokeo mwanafunzi asiporidhika.

Shauri la pili anahoji uwezo wa kitaaluma na kimaadili wa baadhi ya watumishi wa chuo hicho na anaiomba mahakama itamke kuwa hawana uwezo wa kitaaluma na maadili ya kitaaluma.

Mashauri yote yanasubiri kupangiwa tarehe ya kuanza mchakato wa kuyasikiliza.
Kumekuwa na mjadala mkali katika jamii, hususan kwa wanafunzi wa mafunzo ya uwakili shuleni hapo pamoja na wadau wa taaluma hiyo nchini kuhusiana na wanafunzi wengi kushindwa katika mitihani hiyo.

Takwimu za matokeo ya mitihani hiyo zinaonyesha kila mwaka wanafunzi wengine wamekuwa wakishindwa kufaulu mitihani hiyo, baadhi wakitakiwa kurudia sehemu ya masomo na wengine wakiwa wamerudia kwa miaka zaidi ya saba bila kufaulu.

Source: Mwananchi
 
hii kesi inaweza kuwa hatua kubwa kwenye maamuzi ya rufaa za mitihani vyuoni kama haki itatendeka.
Sidhan sana kama inaweza kutoa maamuzi yenye tija sana.

Proceedings nyingi sana zinazoendeshwa mahakamani zina mapungufu makubwa sana ya kisheria kutokana na mikono ya kisiasa, na baadae hizi kesi kuamuliwa kwa kupingana na katiba, na hvyo baadae kutengeneza bad precedents.

Hz bad precedents ukizitumia kujibia mtihani ndo hivyo tena inakula kwako.

System overhaul nzima ndo kitu kinachohitajika, otherwise tutakuwa kwenye never ending game. Mahakama zimekuwa politically manipulated.
 
Mmoja wa wanafunzi walioathirika na matokeo katika Taasisi ya mafunzo ya Sheria kwa Vitendo (LST), Alexander Barunguza ameiomba mahakama iizuie shule hiyo kuendelea na mafunzo kwa muda ili kufanya uchunguzi wa mazingira ya kujifunzia na kuzuia ubadhirifu.

Barunguza, ambaye pia amefungua kesi Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) na nyingine ya kikatiba Mahakama Kuu, katika kesi hizo anapinga uamuzi wa taasisi hiyo kutupilia mbali rufaa yake ya kupinga matokeo yaliyoonesha kuwa ameshindwa kufaulu somo moja hata baada ya kulirudia.

Wakati kesi ya kikatiba inayosikilizwa na jopo la majaji watatu, Dk Deo Nangela, Ephery Kisanya na Dk Theodora Mwenegoha ilipotajwa Ijumaa iliyopita, ndipo alipowasilisha ombi la zuio la muda la shule hiyo kuendelea kutoa mafunzo hayo.

Barunguza alieleza kuwa anaomba amri hiyo ya zuio la muda ili kuzuia ubadhirifu na uharibifu wa rasilimali za umma, ikiwemo bajeti inayotengwa kila mwaka Sh4 bilioni kwa ajili ya kuboresha mafunzo hayo.

Alidai kuwa tangu chuo hicho kianze kimekuwa na mazingira yasiyo rafiki kwa kutokuwepo hosteli za wanafunzi watokao mikoani na hivyo kusababisha vijana hao kushindwa kufikia hatima yao ya kitaaluma ya kulitumikia taifa.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Stanley Kalokola alipinga hoja hizo pamoja na mambo mengine akidai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri hiyo kwa kuwa inakaa kama mahakama ya kikatiba
Katika shauri hilo la kikatiba namba 11 la mwaka 2022, Barunguza anapinga matokeo ya mitihiani yake ya muhula wa kwanza na wa pili mwaka 2019/2020 ambayo alishindwa kufikisha alama za ufaulu katika kozi mbili.

Pia anapinga kanuni na taratibu za rufaa akisema ni kinyume cha Katiba na kwamba katika mchakato wa rufaa yake iliyotupiliwa mbali na LST hakupewa haki ya kusikilizwa.

Vilevile anadai kuwa haki zake za kuishi na usalama zimekiukwa au zinaelekea kukiukwa kutokana na kutishiwa maisha na mmoja wa walimu chuoni hapo baada ya kukata rufaa kupinga matokeo hayo, huku akidai kutengwa, kubaguliwa na kutokutambuliwa kama mwanafunzi.

Katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki mwanafunzi huyo amefungua mashauri mawili, moja anapinga taratibu za kukata rufaa chuoni hapo ili kupinga matokeo mwanafunzi asiporidhika.

Shauri la pili anahoji uwezo wa kitaaluma na kimaadili wa baadhi ya watumishi wa chuo hicho na anaiomba mahakama itamke kuwa hawana uwezo wa kitaaluma na maadili ya kitaaluma.

Mashauri yote yanasubiri kupangiwa tarehe ya kuanza mchakato wa kuyasikiliza.
Kumekuwa na mjadala mkali katika jamii, hususan kwa wanafunzi wa mafunzo ya uwakili shuleni hapo pamoja na wadau wa taaluma hiyo nchini kuhusiana na wanafunzi wengi kushindwa katika mitihani hiyo.

Takwimu za matokeo ya mitihani hiyo zinaonyesha kila mwaka wanafunzi wengine wamekuwa wakishindwa kufaulu mitihani hiyo, baadhi wakitakiwa kurudia sehemu ya masomo na wengine wakiwa wamerudia kwa miaka zaidi ya saba bila kufaulu.

CHANZO: MWANANCHI
 
Back
Top Bottom