PreGE2025 Mwanafunzi UDSM: Wabunge wanawaza kurudi 2030 sio kujenga taifa

PreGE2025 Mwanafunzi UDSM: Wabunge wanawaza kurudi 2030 sio kujenga taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
huyo kijana huenda anatafuta kiki tu, but aende na hoja hiyo kuomba ridhaa ya uongozi kwa wananchi, hawezi kuambulia chochote.

na matokeo ya dhana za aina hii,
huibua kasumba ya ubaguzi baina ya wanajiona wamesoma dhidi ya ambao hawajasoma.

na ni hatari kwa umoja wa kitaifa šŸ’
Kwa mfano kama kigezo cha kuwa rais ni hadi uwe na degree moja, mbona hatusikii wenye stashahada wakilalamika kwamba wanabaguliwa ?
 
Hilo jina lake la Mwisho wanaweza kulitumia kama fursa.
 
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Angasi Robert Okechi, amesema kuwa katika nchi zilizoendelea, Bunge ni mahali pa watu wenye upeo mkubwa wa fikra na maarifa, ambapo wabunge hukutana kuandaa mipango mikakati ya maendeleo ya muda mrefu kwa manufaa ya taifa.

Akizungumza leo Juni 22, 2025 jijini Dar es Salaam, mbele ya wanahabari, Angasi amesema tofauti na mataifa mengine, hapa nchini baadhi ya wabunge huingia bungeni kwa lengo la kupanga mbinu za kisiasa zitakazowarejesha madarakani ifikapo mwaka , badala ya kujadili masuala ya msingi ya maendeleo.

ā€œMbunge anatakiwa aingie bungeni kuwasemea wananchi wake kwa maslahi mapana ya nchi. Lazima awe na uwezo wa kuandaa mpango mkakati na kuupeleka bungeni ili utungwe sheria zenye manufaa kwa wananchi,ā€ amesema.

Aidha, Angasi amekosoa tabia ya kuchagua wabunge kwa misingi ya umaarufu au uwezo wa kifedha bila kuzingatia elimu na uelewa wa masuala ya kisheria na kiuchumi.

ā€œHaiwezekani mtu mwenye elimu ya darasa la saba, kwa sababu tu anajua kusoma na kuandika, anazo fedha na anajua kuzungumza vizuri, apewe jukumu la kutunga sheria za kuongoza taifa. Bunge ni chombo nyeti kinachopaswa kuwa na watu makini,ā€ amesisitiza.

Angasi amehimiza Watanzania kuwaamini vijana waliobobea kutoka vyuo vikuu na vyuo vya kati, kwa kuwa wanaweza kuibua mipango madhubuti ya kulisaidia taifa kwa nguvu na maarifa yao.

View attachment 3379696
Wasomi wa ukweli hawa.Sio ile mingine.
 
MWEZI WA SITA KAMA SIYO KARIBIA MWEZI WA SABA UNATAKA MBUNGU AWAZE NINI KAMA SIYO UBUNGE? JULY BUNGE LINAVUNJWA.SO USIWALAUMU BURE.WATAJENGA TAIFA HAPO BAADAYE NOVEMBA
 
Mimi naamini, Muhimili muhimu kama Bunge unahitaji watu wasomi na si tuu wasomi bali wasomi wenye upeo mpana sana wa kupambanua mambo ya kijamii, kitaifa, kikanda na kimataifa. Kwanini tunahitaji watu hao?
Sababu kubwa ni kwamba kutokana na ukuaji wa kasi sanaa wa utandawazi unachangizwa na kukua kwa teknolojia basi hatuna budi kupata watu mahiri watakao weza kufanya uchambuzi wa hoja za NDANI na NJE kwa kina kisha kuielekeza SERIKALI nini inatakiwa kufanya ili taifa letu libaki salama. Wote tumekuwa mashahidi baadhi ya Taasisi nyeti hasa zile zinazojitegemea hapo miaka ya nyuma zilikuwa zikifanya recruitment bila kujali sifa ya elimu, lakini siku hizi wenye elimu wanapewa kipaumbele sanaa na tena wale wenye elimu mahsusi wanapewagwa na ka-upendeleo fulani ili hata kama mtu hakuwahi kuwaza kuajiriwa huko basi aone sababu. Wote tunaona mambo yanayoendelea Dunian kwa sasa, ni teknolojia kwa kwenda mbele matumizi ya nguvu hayapewi tena kipaumbele.
Sababu ya pili, kwa sasa dunia inakabiliwa na matishio mengi sanaa karibu kwenye kila sekta, elimu, afya, kilimo, ulinzi, misingi ya tamaduni(maadili) katika jamii, uchumi, n.k
Sasa katika uwanda mpana kama huo tunahitaji kuwa na taifa lenye wabobevu wa uchambuzi makini katika muhimili muhimu kama BUNGE. Tuweke maslahi ya taifa mbele jameni. Taifa kwanza mambo mengine baadae...
Nawatakia kazi njema Wakuu.
 
Huyu anachanganya elimu ya chuo na siasa🐼
Bunge kama ni la kutunga sheria basi wanatakiwa wabunge wasomi na wenye uelewa mzuri wa masuala ya dunia.
Waziri ama mwenyekiti wa ccm hata akiwa la saba ama failure hilo halina shida!
 
Back
Top Bottom