Mwanafunzi uandishi wa habari ajiua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi uandishi wa habari ajiua

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Michael Amon, Mar 24, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  MWANAFUNZI wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro, Hemed Athuman (21), amejinyonga kw akutumia shuka baada ya kufeli mitihani.

  Kamanda wa polisi mkoani hapo, Adolphina Chialo, alisema tukio hilo lilitokea Machi 22, mwaka huu saa 2:30 usiku nyumbani kwao, eneo la Mafiga.

  Chialo alisema mwanafunzi huyo alikuwa anasoma Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro ngazi ya cheti, baada ya majibu kutoka ya kuingia semista ya pili, ilionekana hakufanya vizuri.

  Kwa mujibu wa ndugu, Athuman aliacha barua ujumbe kuwa hakutendewa haki katika mitihani yake na asihusishwe mtu yeyote na kifo chake, kwani ameamua mwenyewe.

  Alisema ameamua kujiua kutokana na kutotendewa haki kwenye mitihani yake huku akisema alijitahidi kusoma kwa bidii kutokana na kwamba, ndugu ndiyo waliokuwa wakimsaidia kwa sababu wazazi wake walishafariki, lakini ameona ndoto yake haiwezi kutimia.

  Hata hivyo, Chialo alisema uchunguzi zaidi wa kifo hicho unaendelea. Katika lingine, mtu asiyefahamika amefariki dunia baada ya kugongwa na gari.

  Chialo alisema tukio hilo lilitokea Machi 22, mwaka huu saa 2:00 usiku eneo la Makunganya barabara ya Morogoro – Dodoma, gari isiyofahamika ilimgonga mtu huyo na kusababisha kifo chake papo hapo.

  Wakati huohuo, Martine Emilly (38), mkazi wa Kihonda, Manispaa ya Morogoro, akiwa katika pikipiki aina ya SanLG aligongwa na gari isiyofahamika na kufariki papo hapo.

  Kamanda Chialo alisema tukio hilo lilitokea Machi 22, mwaka huu saa 2:00 usiku eneo la Makunganya, baada ya ajali hiyo kutokea mwenye gari alikimbia na polisi inaendelea na uchunguzi zaidi

   
 2. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Makubwa haya. Kutotendewa haki ndio ajiue! Siku zake za kukaa ktk sayari hii, labda zilikuwa zimetimia!!
   
 3. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #3
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Amejitakia mwenyewe. Kama kweli siku zake zingekuwa zimetimia kweli Mungu angemchukua kwa njia zake mwenyewe bila ya hata yeye kujiua.
   
 4. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hiyo nayo ni njia Mkuu,kwani we unajua mipango/njia zake Mungu?
   
 5. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #5
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Sijui mipango yake. Ila Mungu sio mjinga wala yeye si kigeugeu. Haiwezekeni Mungu aweke amri ya kusema usiue halafu yeye achukue uhai wako kwa kujiua mwenyewe.
   
 6. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,042
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Habari za ndani ni kwamba waliomlipia hada walimwambia akifeli awawezi kumlipia tena hada
   
 7. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #7
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo hiko ndio chanzo halisi cha yeye kujiua?
   
 8. nsangaman

  nsangaman JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Denti kaenda kupiga zake field kuzimu,subirini ataibukia hapa JF na HABARI TOKA KUZIMU.
   
 9. K

  Kayinga junior Senior Member

  #9
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jamani msaada usiwe namashariti,watu watajimaliza mno
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2012
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Suicides zinazidi kuongezeka siku hadi siku.
  Utafiti unahitajika ili kubaini chanzo na pia kuona namna
  ya kuwasaidia watu wanaopatwa na msongo wa mawazo na kukata tamaa.
  Inasikitisha sana kuona kijana mdogo kama huyu akiamua kujiua
  kama njia ya kukimbia matatizo.

  Kushindwa mitihani siyo kushindwa maisha ndivyo tulikua
  tunaamini huko nyuma.Inaelekea siku hizi kushinda mitihani ni
  kila kitu na ndio maana tunaona wizi wa mitihani na kuibia wakati
  wa mtihani vikishika kasi na kuleta matokeo mabaya sana!

  Wazazi na walezi wasaidie katika kutoa elimu ya kujiamini
  kwa vijana na watoto. Kadhakika viongozi wa dini na hata
  viongozi wengine wakiwemo wa kijamii wasaidie kutoa elimu
  kuhusu ubaya wa kujiua.
   
 11. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa, kwa muda wa wiki hii inayoishia leo watu watatu imejulikana wamejinyonga,acha ambao habari zao hazijajulikana, Ilianza habari ya Mkufunzi msaidizi UDSM sweden,Ikafuatiwa na Auditor wa Mahakama kuu Kimara baruti,then Mwanafunzi wa uandishi wa habari. hali ni mbaya jamani.
   
 12. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #12
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Wewe umejuaje kuwa yupo kuzimu? Upo naye nini?
   
 13. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #13
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Lakini huo ni ujinga wake. Mimi sioni sababu ya yeye kujiua eti kwa sababu ya kufeli au kutokulipiwa ada tena. Mbona mimi baba yangu mzazi alikataa kunisomesha nikasoma kwa shida kama chokoraa nikijishibisha kwa makombo na maji ya chooni lakini hata siku moja sikuwahi kufikiria kujia kwa namna yoyote ile.
   
 14. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #14
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Na ndio maana hata ufanisi makazini unakuwa ni mbovu kwa sababu wengi wetu tunasoma si kwa ajili ya kujifunza na kuelimika bali kwa ajili ya kufaulu mtihani na hapo ndipo tunapokosea.
   
 15. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Uhai ni bora sana kuliko anything in this world even money...
   
 16. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #16
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  yep. you are right bro.
   
 17. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  All the best
   
 18. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #18
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  All the best katika kujiua?
   
 19. b

  bibi.com JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 1,155
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mungu tusimzingizie kabisa tunafanya ujinga tunasema mapenzi ya Mungu! Mungu gani huyo anayeumba watu halafu akuchukue ungali mbichi hii kitu ndio inatumaliza waafrika, tunaishi ovyo, magari twaendesha speed ajali ikitokea ni Mungu, Mungu gani huyo mbona wajapan wanaishi miaka 80 huyo Mungu wao yukoje! tumheshimu Mungu, utu, na tufanye yaliyo mema uone kama hakutakuwa na vifo vya kizembe! watu haturespect uhai wa mtu kabisa!
   
 20. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #20
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Usemayo ni kweli kabisa bibi.
   
Loading...