Mwanafunzi kilaza

Mwanafunzi kilaza

mankachara

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2013
Posts
6,161
Reaction score
3,495
Cheka kidogo:

Kuna kijana mmoja alikua anaitwa Said. Kijana huyo shuleni kwao, wanafunzi wenzake hata mwalimu wake hakuna aliyekua anampenda kwa sababu alikua kilaza sana.

Siku moja mama yake alikwenda shuleni kwao kufuatilia maendeleo yake, mwalimu wake hakumficha, akamwambia ukweli kuwa tangu aanze kufundisha hajawahi kufundisha mtoto kilaza kama huyo.. Mama yake akamuhamisha shule na kumuhamisha mji kabisa.

Miaka 25 baadae, yule mwalimu alikua anaumwa na madaktari walimshauri kuwa njia pekee ya yeye kupona ni kufanyiwa operation ya moyo na dr pekee ni mmoja anaeweza fanya hiyo... Mwalimu akafanyiwa operation vizuri na alipozinduka alimuona daktari akitabasamu mbele yake.

Ghafla daktari alianza kushangaa mwalimu akianza kubadilika, ghafla akakata roho. Yule daktari alipoangalia kujua nini tatizo akamuona Said aliyekua mfagiaji pale akichomoa waya wa oxygen na kuchomeka simu yake chaji ...

Kama ulifikiri doctor alikua Said nawe ni kilaza.
 
Na kama ulizan ss tutamfikiria said bc ww ni kilaza wa kutupwa
 
We ndo kilaza tangu lini chumba cha upasuaji wakaingia ingia tu mpaka wafagiaji tena pindi cha kazi maalum?

Hata me sikubali ukilaza!!! Tena waya haupeleki oxygen kwa mgonjwa ni bomba ndilo latumika
 
Cheka kidogo:

Kuna kijana mmoja alikua anaitwa Said. Kijana huyo shuleni kwao, wanafunzi wenzake hata mwalimu wake hakuna aliyekua anampenda kwa sababu alikua kilaza sana.

Siku moja mama yake alikwenda shuleni kwao kufuatilia maendeleo yake, mwalimu wake hakumficha, akamwambia ukweli kuwa tangu aanze kufundisha hajawahi kufundisha mtoto kilaza kama huyo.. Mama yake akamuhamisha shule na kumuhamisha mji kabisa.

Miaka 25 baadae, yule mwalimu alikua anaumwa na madaktari walimshauri kuwa njia pekee ya yeye kupona ni kufanyiwa operation ya moyo na dr pekee ni mmoja anaeweza fanya hiyo... Mwalimu akafanyiwa operation vizuri na alipozinduka alimuona daktari akitabasamu mbele yake.

Ghafla daktari alianza kushangaa mwalimu akianza kubadilika, ghafla akakata roho. Yule daktari alipoangalia kujua nini tatizo akamuona Said aliyekua mfagiaji pale akichomoa waya wa oxygen na kuchomeka simu yake chaji ...

Kama ulifikiri doctor alikua Said nawe ni kilaza.

Ume umesahau bana kilaza hakua Saidi, nakumbuka vizuri tu alikua ni Joji wa mwananyamala mkuu
 
Back
Top Bottom