Mwanafunzi aliyepigwa risasi apewa mil. 1/-

SERIKALI imetoa Sh. milioni moja kwa mwanafunzi aliyepigwa risasi na polisi wakati wa vurugu za wanafunzi za kufunga barabara eneo la Mbezi kwa Yusuf Dar es Salaam wakishinikiza kuwekwa matuta na alama za wavuka kwa miguu.

Msaada huo umetolewa jana na Waziri Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha alipomtembelea mwanafunzi huyo ambaye amelazwa katika kitengo cha watu mahututi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani, mwanafunzi huyo ni wa Shule ya Sekondari Mbezi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Nahodha aliwapongeza madaktari hao na kuahidi kwamba Serikali itakuwa tayari kuchangia gharama za matibabu ya mwanafunzi huyo kama itahitajika.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kabla ya Waziri Nahodha kumtembelea mwanafunzi huyo, alitembelea katika Shule ya Sekondari Mbezi na kuzungumza na walimu na wanafunzi pamoja na kutoa pole kwa wote walioumia katika vurugu hizo.

Taarifa ilifafanua kuwa, akiwa shuleni hapo, Nahodha aliwataka wanafunzi kuepuka kujiingiza katika vitendo vya kuvunja sheria kama walivyofanya kwa kufunga barabara ili kuepusha kukabiliana na vyombo vya dola.

Waziri Nahodha alisema, kumezuka tatizo la baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi na kusababisha vyombo vya dola kuingilia kati jambo ambalo ni hatari na kuwataka wananchi kuepuka tabia hiyo.

Hata hivyo, aliwaahidi wanafunzi hao kuwa, Serikali itaweka alama za kuvuka barabara pamoja na kuwasiliana na wataalam kuona uwezekano wa kuweka matuta ingawaje kwa kuanzia itaweka askari wa usalama barabarani ili kulinda usalama wa wanaovuka barabara katika eneo hilo.

Vilevile ilielezwa kuwa, Serikali haitasita kuwafutia leseni madereva wote ambao watakiuka sheria za usalama barabarani na kusababisha maafa kwa raia na mali zao.

Sijaona pahala aliposema Polisi waliotumia nguvu nyingi sana ikiwa pamoja na kujeruhi wanafunzi hao ambao hawakuwa na silaha yoyote watachukuliwa hatua gani.

Ndio maana nasema huko Tanzania hakuna amani hata kidogo bali watu ni waoga tu
 
mmmh hata soni huna?kuna njia sahihi za kufire to kill,hao sawa walifanya vururugu
lahini im sure wangemwagiwa upupu na risasi baridi mambo yangeenda sawasawa
si kuwatwanga watoto risasi
kwani gari kitu gani bwanaa ! by the way utakufa atakliacha hapa huzikwi hata na tairi
shame on you
 
If you may try to look from both sides, do you know to what extent other drivers were affected by hooliganism of these kids?!, do you how much loses they sufered through stones thrown by pupils on passing vehicles?!. To me-they desrved.

Gama, can you give an indication of the losses suffered, show pictures and if possible tell the whole story from the "other side" as you call it?
Does anyone have any pictures of this young man in his current condition? Heck, what is his current condition?
 
Sijaona pahala aliposema Polisi waliotumia nguvu nyingi sana ikiwa pamoja na kujeruhi wanafunzi hao ambao hawakuwa na silaha yoyote watachukuliwa hatua gani.Ndio maana nasema huko Tanzania hakuna amani hata kidogo bali watu ni waoga tu
mimi nadhani wanafunzi wote walioandamana barabarani na kurusha mawe na kuharibu magari na kujeruhi watu washitakiwe, na walimu wao pia waliowashawishi kufanya vurugu nao washitakiwe na waadhibiwe.
 
mmmh hata soni huna?kuna njia sahihi za kufire to kill,hao sawa walifanya vururugulahini im sure wangemwagiwa upupu na risasi baridi mambo yangeenda sawasawasi kuwatwanga watoto risasikwani gari kitu gani bwanaa ! by the way utakufa atakliacha hapa huzikwi hata na tairishame on you
unaiambia dora isitumie nguvu, lakini jamii(wanafunzi) unawambia nini?, kwamba ni sahihi kuweka magogo barabarani na kurushiamawe wapita njia?!, nilidhani ni wakati muafaka sasa kuwaeleza wanafunzi kuwa walitakiwa kufanya peaceful demonstration wakiwa na mabango yenye ujumbe na bila kuharibu mali za watanzania wengine. Kama hili hulioni you remain an irresponsible citizen unayedhanikuwa dora haipaswi kutumia nguvu kulinda raia wake.
 
Gama, can you give an indication of the losses suffered, show pictures and if possible tell the whole story from the "other side" as you call it?Does anyone have any pictures of this young man in his current condition? Heck, what is his current condition?
naona wewe unadandia bodaboda kwa nyuma, kabla hujachangia mada hii rudi kwenye thread za siku ya tukio uone kilichotokea. Hatuwezi kuendelea kufanya repeatition ya kilichotokea, elewa kuwa wanafunzi walikuwa walirusha mawe kwa magari ya kiraia na ya polisi-they had to be contained that way, nakushari ulione kuwa ni fundisho kwa wanaotumia downstairs ku-aproach issues. Naunga mkono maandamano lakini sitaunga mkono uvunjaji wa amani kwa watu wengine kwa kisingizio cha kudai haki.
 
mmmh hata soni huna?kuna njia sahihi za kufire to kill,hao sawa walifanya vururugulahini im sure wangemwagiwa upupu na risasi baridi mambo yangeenda sawasawasi kuwatwanga watoto risasikwani gari kitu gani bwanaa ! by the way utakufa atakliacha hapa huzikwi hata na tairishame on you
Hapo ndipo akili yako inapofika, kuwa kama mtu hatazikwa na gari basi watu waamue kuyaharibu na polisi wasiingilie?! Huoni soni kutapika haya jukwaani?!. Let me tell you: tujifunze na tuwafundishe vizazi vyetu njia za kibinadamu za kudai haki la sivyo yatatukuta haya yaliyowakuta hawa wajinga wa mbezi HS.
 
Askali aliefyatua risasi amepewa nini? Bado yupokazini? Anafanya kazi ya nani? Au yupo gerezani
 
Askali aliefyatua risasi amepewa nini? Bado yupokazini? Anafanya kazi ya nani? Au yupo gerezani
Amepandishwa cheo kwa kudhibiti vurugu na kuwalinda raia na mali zao kikamirifu. He did a good job.
 
Amepandishwa cheo kwa kudhibiti vurugu na kuwalinda raia na mali zao kikamirifu. He did a good job.
Duh, mwanaJF mwenzetu! Yaani kioo cha gari ulichovunjiwa kimekutia hasira sana kiasi kwamba unaona ni halali kwa askari wa TZ kumpiga mtoto wa shule risasi ya moto! Kaaz kweli kweli.
 
naona wewe unadandia bodaboda kwa nyuma, kabla hujachangia mada hii rudi kwenye thread za siku ya tukio uone kilichotokea. Hatuwezi kuendelea kufanya repeatition ya kilichotokea, elewa kuwa wanafunzi walikuwa walirusha mawe kwa magari ya kiraia na ya polisi-they had to be contained that way, nakushari ulione kuwa ni fundisho kwa wanaotumia downstairs ku-aproach issues. Naunga mkono maandamano lakini sitaunga mkono uvunjaji wa amani kwa watu wengine kwa kisingizio cha kudai haki.

Una defend hii ishu kwa hasira na kashfa. Sawa, in your opinion, they had to be contained by bullets. How is the young man doing? Kuna watu wanataka kumtembelea.
 
Una defend hii ishu kwa hasira na kashfa. Sawa, in your opinion, they had to be contained by bullets. How is the young man doing? Kuna watu wanataka kumtembelea.
Namuombea apone haraka aendelee na shule. Nawaomba wana JF wanaopenda vurugu wajifunze na tutumie JF kuielimisha jamii kuwa tunaweza kufanya maandamano ya amani na ujumbe ukafika kuliko kumuona mtanzania mwenzio kama adui wakati sote tunathirika na huu mfumo wa kutokuwa na organized system. Kama hatuwezi kuyangalia haya end of the day kila mwananchi atataka kujilinda mwenyewe na kulinda mali zake nchi haitakalika.
 
Back
Top Bottom