Mwanafunzi aliyepigwa risasi apewa mil. 1/- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi aliyepigwa risasi apewa mil. 1/-

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  SERIKALI imetoa Sh. milioni moja kwa mwanafunzi aliyepigwa risasi na polisi wakati wa vurugu za wanafunzi za kufunga barabara eneo la Mbezi kwa Yusuf Dar es Salaam wakishinikiza kuwekwa matuta na alama za wavuka kwa miguu.

  Msaada huo umetolewa jana na Waziri Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha alipomtembelea mwanafunzi huyo ambaye amelazwa katika kitengo cha watu mahututi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani, mwanafunzi huyo ni wa Shule ya Sekondari Mbezi.

  Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Nahodha aliwapongeza madaktari hao na kuahidi kwamba Serikali itakuwa tayari kuchangia gharama za matibabu ya mwanafunzi huyo kama itahitajika.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kabla ya Waziri Nahodha kumtembelea mwanafunzi huyo, alitembelea katika Shule ya Sekondari Mbezi na kuzungumza na walimu na wanafunzi pamoja na kutoa pole kwa wote walioumia katika vurugu hizo.

  Taarifa ilifafanua kuwa, akiwa shuleni hapo, Nahodha aliwataka wanafunzi kuepuka kujiingiza katika vitendo vya kuvunja sheria kama walivyofanya kwa kufunga barabara ili kuepusha kukabiliana na vyombo vya dola.

  Waziri Nahodha alisema, kumezuka tatizo la baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi na kusababisha vyombo vya dola kuingilia kati jambo ambalo ni hatari na kuwataka wananchi kuepuka tabia hiyo.

  Hata hivyo, aliwaahidi wanafunzi hao kuwa, Serikali itaweka alama za kuvuka barabara pamoja na kuwasiliana na wataalam kuona uwezekano wa kuweka matuta ingawaje kwa kuanzia itaweka askari wa usalama barabarani ili kulinda usalama wa wanaovuka barabara katika eneo hilo.

  Vilevile ilielezwa kuwa, Serikali haitasita kuwafutia leseni madereva wote ambao watakiuka sheria za usalama barabarani na kusababisha maafa kwa raia na mali zao.
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Polisi aliyempiga risasi vipi?
   
 3. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Risasi za moto hadi kwa wanafunzi ? Kuanzia kiranja mkuu hadi wasaidizi wake wote vilaza tu ... no wonder we are still very poor while we do have everything ....
   
 4. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Duu! Milioni moja tu?
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sio pesa hv risasi mpaka kwa wanafunzi tena za moto hawa polisi wana akili kweli?hv waqlishindwa kutumia risasi za mpira au mabomu ya machozi au hata za plastiki na huyu polisi aliyepiga risasi yupo wapi?

  Hapa kweli inaonyesha ni jinsi gani hawa polisi wetu wasivyo na akili yaani wanafunzi ni watoto wadogo sana kluliko hata maandamano ya watu wazima ama vyuo vikuu sasa kuna siku si watatumia mabomu ya moto kabisa yaani system ya jeshi la polisi inatakiwa ifanyiwe marekebisho ya hali ya juu sana kama inawezekana bora polisi wachukuliwe wakiwa na degree kabisa na sio darasa la saba!
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Sijasikia wanaharakati wakiongelea issue hii, manake nini?
   
 7. STREET SMART

  STREET SMART JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 666
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  Nadhani amepewa kwa staili ya Take it or Leave it.
   
 8. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,139
  Trophy Points: 280
  Polisi wetu wanatumia nguvu nyingi pasipo na sababu ya msingi.
  Unaenda kuwatawanya wanafunzi kwa risasi, kwani mabomu ya machozi na gari la upupu vilikuwa wapi?
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Jul 2, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Africa, in particular Tanzania, is known for having many trigger-happy police officers. Look at what is happening in Greece today and no live bullets have been used even through some police officers are reported to have been injured.
   
 10. S

  Sweetlove Member

  #10
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maafande wanafundishwa kutumia nguvu na siyo akili na haya ndo matokeo yake.Mungu aponye mwanafunzi hyo 2we nae tna.
   
 11. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kwani hiyo hela ni msaada au ni fidia ambayo PT wanapashwa kutoa maana mi sielewi..
   
 12. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,756
  Trophy Points: 280
  hivi nji hii ikoje? watoto wanapigwa risasi za moto while kina chenge walioua na yule kilaza wa maafande aliewasingizia watu ujambazi na kuwatwanga risasi bila huruma na yule aliemtwanga dereva tax risasi ila nayeye israili akamnyakulia guest, kwanini ndo wasiuwawe? naipenda tz nauchukia uongozi wake khaaaa
   
 13. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hv hawa polisi kupiga watu risasi ishakuwa dili kipindi hiki halafu hamna hatua yoyote ya maana inayochukuliwa.
   
 14. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  If you may try to look from both sides, do you know to what extent other drivers were affected by hooliganism of these kids?!, do you how much loses they sufered through stones thrown by pupils on passing vehicles?!. To me-they desrved.
   
 15. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Are you a parent? Usitukane mkunga uzazi ungalipo! when this happens to your son/daughter...
   
 16. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  unataka nishabikie watoto kuandamana barabarani na kurushia mawe magari ya wapitanjia?, supose mwanao anasoma Mbezi HS na siku hiyo umepita na gari akakurushia mawe na kuharibu gari lako, ungemsifu kwa kuharibu gari lako?, hivi pamoja na elimu yote tuliyonayo tumekosa njia za kibinadamu za kutatua matatizo and turned to behave like animals?!. Nawalaumu jeshi la polisi kutowafungulia mashitaka walichochea vurugu hizo, nampongeza aliye-fire to give us a leson.
   
 17. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  hii ndo tanzania bana au unabisha!!!!!!!??
   
 18. N

  NCHABIRONDA JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Msiwalaumu polisi. Polisi wanatekeleza kile walichotumwa na wakubwa zao na ndio maana hawachukuliwi hatua yoyote. Huu ni mwanzo tu mtakuja kuona huko mbeleni tunakoelekea.
   
 19. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mpaka kapigwa risasi ndo waziri anashtuka?

  Shame on you Magamba's Govnment.
   
 20. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kuna mengine yanatia hasira sana yaani
   
Loading...