Mwanafunzi aliyefukuzwa UDSM aomba msaada!

Namshauri awafuate wale aliowasaidia kuhakikisha wanapata mikopo,hiyo ndio faida ya kujitia kimbele mbele kwa mambo yasiyokuhusu,sasa wenzake wameshasoma na wanafanya shughuli zao yeye amegeuka matonya!
Sijui umefikiri kwa kutumia kiungo gani cha mwili mwehu wee!!
 
Wanafunzi wa Udsm ahaaa umenikumbusha kipindi cha Bush na Mtatiro pamoja na Odong odwar jamaa wa Uganda huko na David Silinde sasa mbunge ilikuwa migomo ya kweli Sio hiyo yenu akina Alphonce ya kutetea Chadema au CCM, Bush alikuwa anatetea ukweli akaajiriwa hapo hapo udsm baada ya kumaliza akideal na mikopo, Jiulize wewe Alphonce? Unadharau walimu wako hapo, mgomo na nidhamu muhimu
 
huyu jamaami namchukia seriously,

ningekua necta ningefungia cheti chake cha form 4 na 6.

aanze form one, maana hajakua
 
Baadhi ya majibu hapa yananikumbusha kuwa ujinga ni moja ya maadui zetu wakubwa. Natambua mchango wako Alphonse. Usingekuwa wewe na wenzako leo hii nisingesoma. Kesho nitakutumia mchango wangu naamini utakusaidia. Taifa linakuhitaji sana
 
ndivo tulivo ngozi nyeusi.ubaki wewe kama wewe.kila mtu ana angalia la kwake.
tenda wema nenda zako
hao ulio wabeba sio watakao kubeba.ndivo wa afrika tunavo ishi.ukitaka kujua haya jitoe kwa lolote
 
Katika maisha yangu katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu, ni Tanzania tu ambako kuna adhabu ya kumfungia mtu asiendelee na elimu kwa kosa la kuandamana au kuongoza mgomo; kuandamana au kugoma ni haki ya raia na wala hakuna mahakama huru inayoweza kumtia mtu hatiani kwa kosa la kuandamana au kuongoza mgomo.
 
[HASHTAG]#WATANZANIA[/HASHTAG] NIMEONEWA# Bado na ndoto ya kusoma. Nishikeni Mkono.

Mficha maradhi kifo humuumbua'. Huu ni msemo wetu. Naam, msemo wa kiswahili. Siku niliyopokea barua ya kukatisha masomo yangu kwa mara ya pili katika chuo kikuu UDSM, pamoja na pole nilizopokea kutoka kwa watu mbalimbali, ni uongo na dhambi kama nitasema niko sawa. Siko sawa ndugu zangu. Moyo wangu unavuja damu ya uchungu wa manyanyaso na kubaguliwa kupata elimu katika nchi yangu, katika taasisi iliyotokana na jasho na rasilimali za umma wa watanzania. Ndoto yangu ya kuwa mwanasheria imepepeswa.

Moyo wangu umejaa majeraha na uchungu mkubwa. Najiuliza, kwanini ninyimwe haki ya kusoma? Hata kama ilikuwa ni kosa mwaka 2011 kuwatetea watoto wa masikini kupata mikopo na kupigia kelele udhalimu wa bodi ya mikopo wa kupoka fedha za masikini kupitia majina hewa, mbona nimeshatumikia adhabu ya kukaa nje ya chuo mika 6 ( deterrence theory). Maisha yangu yamerudi nyuma ukilinganisha na yale ya wenzangu tulioanza pamoja chuo 2009 kwasababu tu ya kujitoa mhanga kwajili ya wenzangu.

Adhabu hii licha ya kutokuwa halali, ni adhabu kubwa sana inayozidi hata kipimo cha sheria ya udahili kifungu cha 43(1) kinachotaka mwanafunzi aliyefukuzwa kuruhusiwa kuendelea na masomo yake baada ya miaka 2 kupita. Uongozi wa UDSM umekataa kunituhusu niendelee na masomo yangu.

Nimeaumia sana kuona haki yangu ya kupata elimu ya juu ikifungwa na wenye funguo bila kujali wasinioneshe funguo licha ya jitihada za zaidi ya miaka mitano kuipigania haki hiyo kwa njia za kidiplomasia na kisheria (mahakamani). Sitakiwi kusoma kwenye vyuo vya umma Tanzania.

Licha ya kuwa na matumaini ya kupata haki yangu ya kupata elimu, nguvu yangu hasa ya kiuchumi imekuwa ndogo kwani vyuo vya binafsi ni gharama kidogo. Nahitaji kiasi cha million 7.6 kuwa na uhakika wa kupata elimu yangu kwa miaka 3.

Nisaidieni kutetea ndoto yangu. Natambua ukarimu wenu watanzania. Natambua mnavyothamini elimu. Pia natambua mnavyochukia vitendo vya ukandamizaji na vile vya watu wachache kuamua maisha ya wengine kwasababu tu wanamadaraka mikononi mwao na hawapendi mawazo tofauti. Nimekuja kwenu mnisaidie ndugu zangu.

Tumia njia zifuatazo kunisaidia kadri utakavyoguswa.

MICHANGO ITUMWE:

CRDB a/c No. 0152436033400

M. Pesa: +255 765 443 728

T. Pesa: +255 718 221 535

Airtl.M: +255 683 528 675

Namba zimesajiliwa (Alphonce Lusako M.)

Shukrani.

Alphonce Lusako.
Amtafute jamaa anayeitwa PHILIPO MWAKIBINGA YUPO DODOMA (UDOM NAYE ALIKUMBWA NA MKASA HUO ZAID YA X1 LKN MPAKA SASA ANAENDELEA NA CHUO
AU AINGIE FB A SEARCH PHILIPO MWAKIBINGA ATAMPATA
 
wew kuku usijaribu kutumia lugha ambayo huna utaalamu nayo kiingereza sio kimakonde
 
Namshauri awafuate wale aliowasaidia kuhakikisha wanapata mikopo,hiyo ndio faida ya kujitia kimbele mbele kwa mambo yasiyokuhusu,sasa wenzake wameshasoma na wanafanya shughuli zao yeye amegeuka matonya!

Hii ni indicator ya uwezo mdogo sana wa kufikiri. Duniani kote mabadiliko huletwa na watu wenye kujitoa sana kwa ajili ya wengine. Hata ukisoma historia, kuna watu wamechangia sana mabadiliko kutokana na kujitoa.
 
Baadhi ya majibu ya watu yameniogopesha sana ila badae nikakumbuka ndo tabia za watanzania. UNAFIKI ULIOPITILIZA

unaanzaje kumbeza jamaa kwa kupigania mafanikio ya wengi, sawa na kumbeza aliefariki akipigania uhuru ambao leo tunafurahia

hizi ni tabia za watoto mboga 7 tangu anaanza la kwanza hadi chuo ajawahi kukutana na kusimamisha/kufukuzwa shule wala dhoruba yoyote kwa kuwa MNAFIKI kujipendekeza na kuwachoma wenzake.

unaanzaje kufurahia mateso ya mtu na humfahamu, utoto wa hali ya juu
Mkuu kuna comments za watu huku zinakera sana,yaani ni upumbavu wa kiwango cha juu sana kumponda na kumkebehi mtu ambaye alisaidia wengine kwa kujitoa muhanga. Kiukwel nimesononeka na kuumia sana. Hivi Nyerere alivyojitoa kupigania uhuru wetu alikuwa na kiherehere eti?Hivi angekufa ila tukapata uhuru tungelaumu pia? Dah poor Tanzania
 
Huyu jamaa bado anaamini kutoka kimaisha lazima uwe na degree uchwara za bongo shame on you sisi tunazo hizo degree ila hazija tusaidia
 
Sasa hawa chadema waliokua wanamdanganya si wakamsomeshe nje ya nchi.
 
[HASHTAG]#WATANZANIA[/HASHTAG] NIMEONEWA# Bado na ndoto ya kusoma. Nishikeni Mkono.

Mficha maradhi kifo humuumbua'. Huu ni msemo wetu. Naam, msemo wa kiswahili. Siku niliyopokea barua ya kukatisha masomo yangu kwa mara ya pili katika chuo kikuu UDSM, pamoja na pole nilizopokea kutoka kwa watu mbalimbali, ni uongo na dhambi kama nitasema niko sawa. Siko sawa ndugu zangu. Moyo wangu unavuja damu ya uchungu wa manyanyaso na kubaguliwa kupata elimu katika nchi yangu, katika taasisi iliyotokana na jasho na rasilimali za umma wa watanzania. Ndoto yangu ya kuwa mwanasheria imepepeswa.

Moyo wangu umejaa majeraha na uchungu mkubwa. Najiuliza, kwanini ninyimwe haki ya kusoma? Hata kama ilikuwa ni kosa mwaka 2011 kuwatetea watoto wa masikini kupata mikopo na kupigia kelele udhalimu wa bodi ya mikopo wa kupoka fedha za masikini kupitia majina hewa, mbona nimeshatumikia adhabu ya kukaa nje ya chuo mika 6 ( deterrence theory). Maisha yangu yamerudi nyuma ukilinganisha na yale ya wenzangu tulioanza pamoja chuo 2009 kwasababu tu ya kujitoa mhanga kwajili ya wenzangu.

Adhabu hii licha ya kutokuwa halali, ni adhabu kubwa sana inayozidi hata kipimo cha sheria ya udahili kifungu cha 43(1) kinachotaka mwanafunzi aliyefukuzwa kuruhusiwa kuendelea na masomo yake baada ya miaka 2 kupita. Uongozi wa UDSM umekataa kunituhusu niendelee na masomo yangu.

Nimeaumia sana kuona haki yangu ya kupata elimu ya juu ikifungwa na wenye funguo bila kujali wasinioneshe funguo licha ya jitihada za zaidi ya miaka mitano kuipigania haki hiyo kwa njia za kidiplomasia na kisheria (mahakamani). Sitakiwi kusoma kwenye vyuo vya umma Tanzania.

Licha ya kuwa na matumaini ya kupata haki yangu ya kupata elimu, nguvu yangu hasa ya kiuchumi imekuwa ndogo kwani vyuo vya binafsi ni gharama kidogo. Nahitaji kiasi cha million 7.6 kuwa na uhakika wa kupata elimu yangu kwa miaka 3.

Nisaidieni kutetea ndoto yangu. Natambua ukarimu wenu watanzania. Natambua mnavyothamini elimu. Pia natambua mnavyochukia vitendo vya ukandamizaji na vile vya watu wachache kuamua maisha ya wengine kwasababu tu wanamadaraka mikononi mwao na hawapendi mawazo tofauti. Nimekuja kwenu mnisaidie ndugu zangu.

Tumia njia zifuatazo kunisaidia kadri utakavyoguswa.

MICHANGO ITUMWE:

CRDB a/c No. 0152436033400

M. Pesa: +255 765 443 728

T. Pesa: +255 718 221 535

Airtl.M: +255 683 528 675

Namba zimesajiliwa (Alphonce Lusako M.)

Shukrani.

Alphonce Lusako.
Chadema wakusomeshe Si ulikuwa unawapigania Ndiyo mjue mkiwa vyuoni mlifuata masomo siyo siasa. Unaendekeza siasa ukipata tatizo itakuwa lako. Hao Makamanda wako Akina Heche wako wapi sasa
 
Mtafute Mbowe au Lissu kamanda mihemko hao ndio watetezi wa wanyonge qwi qwi qwi qwi qwi
 
Namshauri awafuate wale aliowasaidia kuhakikisha wanapata mikopo,hiyo ndio faida ya kujitia kimbele mbele kwa mambo yasiyokuhusu,sasa wenzake wameshasoma na wanafanya shughuli zao yeye amegeuka matonya!
Mungu akusamehe maana hujui ulisemalo kwa maana umepewa ufahamu Mdogo mno kuliko wa mtoto mchanga,Amen
 
Bwege ni huyo mwanarakati uchwara,kama vp amtafute Kaoge ampe michongo ya kupata hela ya ada,shwaini mkubwa
Kama watanzania uwezo wao wa kufikiri na kuyaangalia mambo ndo huu...tuna safari ndefu sana. Pengine we need "a genetical drift" kupata haueni ya kuzazi cha kuhoji, kuwasemea na kuwainua wanyonge n.k. Hizi mentality kwamba mwenye mamlaka ana "absolute power" kufanya lolote kwa wenzake ni akili na mawazo ya kalne ya 10. Worse enough uwe na watu wakusimamia mambo haya alafu wenye fikra kama hizi. Ni taabu saaana.
 
Back
Top Bottom