Che Mkira
Senior Member
- Jul 8, 2014
- 117
- 152
[HASHTAG]#WATANZANIA[/HASHTAG] NIMEONEWA# Bado na ndoto ya kusoma. Nishikeni Mkono.
Mficha maradhi kifo humuumbua'. Huu ni msemo wetu. Naam, msemo wa kiswahili. Siku niliyopokea barua ya kukatisha masomo yangu kwa mara ya pili katika chuo kikuu UDSM, pamoja na pole nilizopokea kutoka kwa watu mbalimbali, ni uongo na dhambi kama nitasema niko sawa. Siko sawa ndugu zangu. Moyo wangu unavuja damu ya uchungu wa manyanyaso na kubaguliwa kupata elimu katika nchi yangu, katika taasisi iliyotokana na jasho na rasilimali za umma wa watanzania. Ndoto yangu ya kuwa mwanasheria imepepeswa.
Moyo wangu umejaa majeraha na uchungu mkubwa. Najiuliza, kwanini ninyimwe haki ya kusoma? Hata kama ilikuwa ni kosa mwaka 2011 kuwatetea watoto wa masikini kupata mikopo na kupigia kelele udhalimu wa bodi ya mikopo wa kupoka fedha za masikini kupitia majina hewa, mbona nimeshatumikia adhabu ya kukaa nje ya chuo mika 6 ( deterrence theory). Maisha yangu yamerudi nyuma ukilinganisha na yale ya wenzangu tulioanza pamoja chuo 2009 kwasababu tu ya kujitoa mhanga kwajili ya wenzangu.
Adhabu hii licha ya kutokuwa halali, ni adhabu kubwa sana inayozidi hata kipimo cha sheria ya udahili kifungu cha 43(1) kinachotaka mwanafunzi aliyefukuzwa kuruhusiwa kuendelea na masomo yake baada ya miaka 2 kupita. Uongozi wa UDSM umekataa kunituhusu niendelee na masomo yangu.
Nimeaumia sana kuona haki yangu ya kupata elimu ya juu ikifungwa na wenye funguo bila kujali wasinioneshe funguo licha ya jitihada za zaidi ya miaka mitano kuipigania haki hiyo kwa njia za kidiplomasia na kisheria (mahakamani). Sitakiwi kusoma kwenye vyuo vya umma Tanzania.
Licha ya kuwa na matumaini ya kupata haki yangu ya kupata elimu, nguvu yangu hasa ya kiuchumi imekuwa ndogo kwani vyuo vya binafsi ni gharama kidogo. Nahitaji kiasi cha million 7.6 kuwa na uhakika wa kupata elimu yangu kwa miaka 3.
Nisaidieni kutetea ndoto yangu. Natambua ukarimu wenu watanzania. Natambua mnavyothamini elimu. Pia natambua mnavyochukia vitendo vya ukandamizaji na vile vya watu wachache kuamua maisha ya wengine kwasababu tu wanamadaraka mikononi mwao na hawapendi mawazo tofauti. Nimekuja kwenu mnisaidie ndugu zangu.
Tumia njia zifuatazo kunisaidia kadri utakavyoguswa.
MICHANGO ITUMWE:
CRDB a/c No. 0152436033400
M. Pesa: +255 765 443 728
T. Pesa: +255 718 221 535
Airtl.M: +255 683 528 675
Namba zimesajiliwa (Alphonce Lusako M.)
Shukrani.
Alphonce Lusako.