pombe so chaiKatika hali ya kuhuzunisha, mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule moja mkoani Tabora amefariki dunia kwa kunywa 'Methanol'.
Hali hiyo imetokea baada ya kuugua kwa siku kadhaa kabla ya kufariki leo hii.
Mwanafunzi huyo pamoja na wenzake walikuwa katika maabara ya shule wakifanya mazoezi kwa vitendo (practicals) ili kujiweka sawa katika kuikabili mitihani yao baadae mwezi Novemba.
Walipokuwa wakiendelea na mazoezi, waliona chupa yenye kemikali hiyo ya Methanol yenye molecular fomular CH3OH wakidhani ni Ethanol.
Ethanol ni kemikali itumikayo katika utengenezaji wa pombe. Basi nao wakidhania ni pombe wakaibugia. Asaleeh! Tuwakemee watoto wetu wajaribupo kuonja ama kushawishika katika matumizi ya pombe katika umri mdogo.
Baada ya kuinywa, waliendelea na mambo yao. Hali zao zilianza kubadilika baada ya siku mbili. Wakakubaliana kuifanya siri isigundulike. Walilegea na kuzidiwa na kufikishwa katika kituo cha afya cha karibu. Madaktri walianza kuwapima, hawakuonyesha dalili ya ugonjwa wowote.
Mmoja wao ambaye sasa ni marehemu aliruhusiwa kutoka baada ya kuonyesha unafuu. Lakini uoni wake ulififia kwa kiasi kikubwa.
Mwingine aliendelea kubaki na hali yake ilizidi kuzorota. Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya, mwanafunzi aliyekuwa akimuuguza ikabidi atoboe siri kwa wauguzi kuwa vijana hao walikunywa Methanol.
Ndipo taratibu za haraka kufanyika na kuhamishiwa hospital ya Rufaa Kitete. Nao wakafanya utaratibu wa kumpeleka hospital ya taifa Muhimbili.
Marehemu baada ya kuonyesha unafuu kidogo, yeye akabakia Kitete ambapo baadae leo akifariki dunia.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali anapostahili.
My take:
Walimu kuweni makini sana katika maabara. Wanafunzi wengine ni watundu na walevi. Kosa kidogo tu linagharimu maisha ya mwanafunzi na ya kwako pia.
Any laboratory, its either chemistry, biology or physics laboratoryWhich laboratory??
Unawananga form 4 kuwa na tabia za kitoto? Walio mitaani je shahada mpaka za udaktari?Ina maana hao form4 hawajafundishwa laboratory rules au hawakuelewa ila walikariri kwa ajiri ya mitihani.
Na hao form4 ni watu wazima na bado wana tabia za kitoto alafu wanaitwa taifa la kesho.
Serikali badilisheni huu mfumo wa elimu.
Covid 19 lab...ile iliyotupa results ya papai kuwa ni +veWhich laboratory??
Mi nilishawahi kumlipua mtu mgongoni kwenye shati lake la shule...Maskini ee mungu awasimamie kwani utaratibu maabara za shule umebadilika nini hadi watu wanakunywa kabisa


Ulitaka waone Ugonjwaa gani????? Unadhani kuwa na dalili za ugonjwa inatoshaa kufanya vipimo vioneshe una ugonjwaa.. Kilochotokea itakuwa walitreat symptoms za ugonjwa lakini Methanol ni sumu inayoharibu macho...maini na figo yani slow slow tu lakini mwisho wa siku yanakukuta hayoo...Ukiachilia mbali hao wajinga kunywa sumu, kuna hili ambalo wengi ni kama hatulioni kwenye hii habari.
Wamepimwa ugonjwa haukuonekana (bila shaka hapa ni ishu ya vifaa kutokidhi mahitaji katika kituo cha afya husika na hili ni tatizo karibia nchi nzima isipokuwa kwa baadhi vilivyopo dar) na bado madaktari na manesi wanaendelea kukaa na mgonjwa.
Hii ina maana kwamba kama sio dogo kukiona kifo jirani na kutoboa siri, wangekufa bila kujulikana tatizo ni nini. Kwann kama hapo walipopokelewa na kupewa huduma ya kwanza walishindwa kutambua tatizo hawakuwapa rufaa mapema?
Ifike mahali tuache kucheza na afya za watu![]()
Anyway, sijaandika ili tubishane. Atakayeona hoja unamashiko, sawa. Atakayeona nimeandika pumba, haya.Ulitaka waone Ugonjwaa gani????? Unadhani kuwa na dalili za ugonjwa inatoshaa kufanya vipimo vioneshe una ugonjwaa.. Kilochotokea itakuwa walitreat symptoms za ugonjwa lakini Methanol ni sumu inayoharibu macho...maini na figo yani slow slow tu lakini mwisho wa siku yanakukuta hayoo...
Lakini wenzake wataponaa...!! Maana sasa wameshasema nini kilitokea...Anyway, sijaandika ili tubishane. Atakayeona hoja unamashiko, sawa. Atakayeona nimeandika pumba, haya.
Hoja yangu ni, je! Inamaana dogo asingesema, wangeachwa wafe bila kuwafanyia vipimo zaidi?Lakini wenzake wataponaa...!! Maana sasa wameshasema nini kilitokea...
Mkuu unaweza weka duru ya hii habari?
Wangefanya kipimo cha nini?? Je ukiacha methanol kuna sumu ngapi ambazo binadamu zinaweza kumuathiri??? Historia ya mgonjwa kwa nchi zetu za africa ni jambo kubwa sana kwenye matibabu yanii sawa na Mtoto ameze panadol nyingi wewe usijue japo Hospital wanaweza pima kiwango cha panadol mwilini lakini Bila kujua mtoto alipata shida tokana na kunywa panadol nyingi bhasi wataendelea kutibu Dalili zinazojitokeza bila Kuondoa sumu mwilini ambapo huyu mtoto dalili zinaweza kuwa nzuri lakini Panadol inaendelea kuaribu maini na Ubaya Sumu karibu zote zinakuwa na dalili mojaa so ili mtu apate matibabu sahihi kwa musa sahihi suala la historia ya Ugonjwa na nini kilitokea ni MUHIMU sana kuliko vipimooo.Hoja yangu ni, je! Inamaana dogo asingesema, wangeachwa wafe bila kuwafanyia vipimo zaidi?
Laboratory rules..... Don't eat or drink anything in the laboratory