Mwanafunzi achinjwa kama kuku

Mwanafunzi achinjwa kama kuku

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
HOFU imetenda kwenye Shule ya Msingi Living stone ya mchepuo wa Kiingereza, wilayani Njombe, baada ya mwanafunzi Doris Lutego (12), aliyetekwa ndani ya bweni wiki iliyopita kukutwa ameuawa kwa kuchinjwa kama kuku, mwili wake kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.

Mauaji ya mwanafunzi huyo yametokea siku chache baada ya polisi kutoa taarifa ya kutoweka kwa mwanafunzi huyo, kutokana na watu wasiojulikana kumteka ndani ya bweni.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, alisema mwili huo uliokotwa Juni 13, mwaka huu majira ya asubuhi, kichwa kilikutwa kimetupwa Mtaa wa Nzerengete, huku kikiwa kimewekwa kwenye mkoba wa daftari wa mwanafunzi huyo.

Mangala alisema kiwiliwili chake kilikutwa kimewekwa kwenye genge la biashara lililopo karibu na makazi ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kambarage, kilomita 10 kutoka eneo la shule hiyo.

Awali, ilidaiwa mwanafunzi huyo alitekwa na watu wasiojulikana akiwa amelala baada ya kuvamia bweni la wasichana Juni 12, mwaka huu majira ya usiku na kutoweka naye, huku wakiacha jino na damu kwenye bweni.

Kutokana na uchunguzi wa polisi, watu watatu wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

Alitaja wanaoshikiliwa kuwa, wote ni wakazi wa Njombe, mkoani Iringa.

Mangala alisema polisi inafanya uchunguzi wa kina kujua sababu za mauaji hayo ya kinyama, hasa yakishusisha mwanafunzi ambaye uchunguzi wa mwili wa marehemu unaonyesha kabla ya kuuawa, alipigwa na kitu kizito kichwani.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sara Dumba, alisikitishwa na hali hiyo ambayo imesababisha hofu kwa wanafunzi wa shule hiyo na kwamba, wananchi wanapaswa kutulia wakati polisi wakiendelea na msako kubaini wahusika.

"Serikali imesikitishwa na mauji haya ya kinyama, ninachoomba wananchi wawe watulivu kwa wakati huu polisi wanafanya uchunguzi kubaini wahusika ili hatua za kisheria zichukuliwe," alisema Dumba.

Baadhi ya wananchi walitaka serikali kuhakikisha usalama wa shule zote ambazo zimekuwa zikiweka bwenini wanafunzi, ili kuepusha matukio ya mauaji.

Augustino Wikesi, alisema kama shule hizo zingekuwa na ulinzi wa kutosha, mwanafunzi huyo asigetekwa usiku.
 
Binadamu kwa sasa tumegeuka wanyama wa mwituni? kwanini jaamani? hivi inakuwaje mtu amkate mwenzake shingo kama kuku
ama kweli siku za mwisho zimefika r.i.p marehemu
 
Ni zaidi ya kusikitisha kwani umri huu sidhani kama anaweza kuwa na na visasi na mtu yoyote, hao wauaji wanyongwe tu na hakuna hukumu njingine itawafaa, nahisi hao wametumwa tu na ukiangalia unaweza kuta kuna mgogoro wa uhalali/umiliki wa wazazi juu ya huyo binti. RIP Doris
 
This is too much.....Maisha ya Doris yalikuwa na maana kubwa kwa wazazi wake, ndugu zake na taifa kwa ujumla....
...chanzo cha mauaji haya kikijulikana tujuzane, japo hakuna sababu yoyote ya maana ya kupoteza maisha ya binti huyu....damu ya doris si tu inalia mbele za MUNGU kwa ajili ya wauaji wake lakini pia inaleta laana ktk taifa

mix with yours

 
Inasikitisha sana, wakikamatwa wakabidhiwe kwa wananchi nao wawamalize, hawafai kukaa jela hao
 
Masikini mtoto Doris
Mungu ailaze roho ya marehemu peponi...Amina
 
Habari hii imenisikitisha sana... Heading yake kwenye gazeti mojawapo la leo SIJAIPENDA KABISA...
 
Kwa kweli kama wauwaji wanakamatwa wanastahili mauaji mbele za umati,ni ajabu mtoto wa hivi kuuawa kimafia namna hii

May Lord rest her soul in peace!
 
Taratibu mambo yanayotokea nchi za mbali yanaanza kutokea nyumbani kwetu. i miss them days, when i played inncocently, laughing and jumping kama kitoto cha ndama, worrying abt nothing! maskini watoto wangu...:A S 12:
 
r.i.p dorris. unaweza ukakuta bifu ni mzazi/wazazi na watu wengine. either wamedhulumiana au wameleteana fitina kazini.
 
R.I.P. Doris,huenda ni visasi vya wazazi.Huu ni unyama wa hali ya juu sana.
 
Inasikitisha na kutia simanzi kubwa sana ktk taifa letu Tanzania. Hayo majamaa nayo yauliwe hvyo2 kwn aliye ua kwa upanga naye auawe vivyo hivyo. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMINA!!!
 
Jamani! Mungu atusamehe. Kwanza mtoto mwenyewe ana miaka 12! yaani hapo sioni kama kawakosea nini mtoto mdogo wa umri huo. RIP Doris na poleni wafiwa wote
 
Haki za binadamu wanapinga binadamu kunyongwa lakini kwa mauaji ya namna hii jamani!!!
 
Nimeumia sana, mtoto malaika kwani kakosa nini jamani, hamna hata huruma. EE MUNGU mlipie kwa kuwa ulisema ".............. kisasi ni juu yangu .........."
 
Dah, tunakoenda watanzania ni kubaya sana mana uyo mtoto jamani ana kosa gani? ngoja tusubiri vyombo vya dola vifanye kazi yake labda tutaja pata ukweli wa jambo lenyewe
 
Back
Top Bottom