Mkuu story yako ni short chasis.
Hujaelezea uhalisia wa huyo amma. Je ni mjane? Au ameachika?
Na wewe hujaelezea historia yako ya kimapenzi kabla hujakutana na huyu mama.
Je ulikuwa kwenye mahusiano wakati unakutana na huyu mama? Au umeachika?
Na pia hujaelezea tofauti ya umri uliopo kati yako na huyo mama. Amekuzidi au umemzidi au mnalingana?
Na pia hujaelezea mipango halisi ya hayo mapenzi yenu, je mnataka kuishi kama mke na mume au mnaendekeza tamaa zenu tu kwa sasa au mwenzetu umekumbwa na tamaa ya utajiri wa mama kwa sababu anazo hela?
Na je, suala la kuhamia kwake despite kwamba huyo mama ana umri unadhani ndo suluhu ya mapenzi yenu au mwenzetu umeshatiwa limbwata kwa hiyo umejikuta umetia timu kwa 'mama' kimazingaombwe?
Na je, hili suala lenu mshalifanya kuwa 'official' kwa ngazi ya ndugu, viongozi wenu wa kiroho na kadhalika au mmeamua kuvunja tu amri ya "msijamiiane na kuzini"?
Nna maswali mengi ila naona umenichanganya zaidi.
Anyway..........