Ni juzi tu hapo umetoka kuachia uzi ukisema ulimwengu huu ni mzuri kuishi na kushangazwa na Atheists jinsi wasivyokuwa convinced na uzuri huo kiasi cha kuamini uwepo wa Mungu
Leo tena unakuja kuonesha matatizo ya ulimwengu huu tena kwa mifano iliyo hai (Turkey na Syria)
Sasa tushike lipi?
Majanga yanayotesa watu hayapaswi kuwepo kwenye kazi iliyofanywa na Mungu mwenye upendo woteNinapozungumzia uzuri wa dunia ninamaana ya maumbile yake na vilivyomo, maumbile yake.na vilivyomo ni ishara tosha kwamba yupo aliyeiumba hii dunia naye ndiye tunamuita Mungu, au a conscious disciplined being, Super being nk.
Ninapozungumzia mambo yanayotokea duniani (mambo hasa yanayomsibu mtu) ni lazima uyaweke katika mafungu mawili;
1-- Mambo yote ya raha, faraja, mafanikio nk.
2-- Mambo shida, majanga, misiba nk.
Mambo hayo mawili hayaondoi nafasi ya dunia kuumbwa bali mambo hayo ni sehemu ya taratibu za Mungu kuwafanya watu wamjue Mungu, mfano; tuapopata faraja, raha nk huo ni wakati wetu wa kumshukuru na kumkumbuka Mungu tunapofanya hivyo ndivyo Mungu anatuongezea faraja zaidi.
Upande wa.majanga ni kwamba; Watu wskati mwingine tunapokuwa kwenye faraja huwa tunajisahau kumkumbuka Mungu hivyo wakati mwingine Mungu hutumia njia kali au adhabu kali au kutupa mtihani ambao kwao tuweze kumkumbuka kwa faida yetu, hivyo yale unayoyaona majanga, shida nk huwa katika muundo huo kwani Mungu ndiye aliyetuumba hivyo anazijua nafsi zetu kuliko jinsi sisi tunavyozijua nafsi zetu.
Kifupi ndivyo hivyo.
Majanga yanayotesa watu hayapaswi kuwepo kwenye kazi iliyofanywa na Mungu mwenye upendo wote
Anavyokupa hiyo mitihani ili akupime anataka kugundua nini ambacho hakijui ilihali yeye ni mjuzi wa yote?Hayo unayoyaona ni mateso kutoka kwa Mungu yanaweza kuwa ni ama mtihani au adhabu, mtihani ni kuwapima watu je watamtegemea Yeye katika shida, adhabu ni kuwaadhibu wakosefu baada ya wao kumsahau na kutenda maovu nk, mara nyingi Mungu huwa haadhibu (watu) mtu kabla ya kumuonya/kumpa ishara ya onyo na huo ndio upendo wake kwa binadamu, mfano adhabu ni sawa na wewe kumnywesha mwanao dawa chungu ili apone maradhi, huo ni upendo.
Kifupi ni kwamba tumo ndani ya "banda" ni lazima tutii na tufuate sheria za bandani, hatuna njia sisi tunamilikiwa na Mungu.