Mwanadamu lazima uwe Mchaguzi

Mwanadamu lazima uwe Mchaguzi

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Habarini bandugu

Hakuna mwanadamu ambaye afanyi UCHAGUZI katika maisha yake ya kila siku
wala hakuna mtu ambaye anayeweza kuchagua kile ambacho hakipendi?
Hivyo maisha ya watu wengi yamejaa uchaguzi wa kila namna wa vile watakavyo.

Je wewe unachagua nini au unapendelea kuchagua nini katika maisha yako?
wako wengine wanafanya maamuzi ya uchaguzi mbovu katika maisha yao
wengine wanachagua maisha ya kuwa vibaka, walevi wa kupindukia, watukanaji
wafanyao dhambi ya uzinzi yaani uasherati, wako wanafanya kufuru ya kujibadilisha
ngozi yao na kuweka bandia kusudi wawe wazungu, na kumbe wanajidanganya
kwani kuna madhara yake hapo baadaye yaani kupata kansa ya ngozi

Wako wengine wanafanya maamuzi mabovu ya uchaguzi wa kuwa naa wenzi wa
maisha yao , sasa hapa ndipo unajikoroga kabisa kijana Uchaguzi ambao wanafanya
vijana wengi unapelekea mahali pa mabaya na kuanza kujuta hapo baadaye
Wewe unachagua kitu usichokipenda au mtu usiyependa kisa unataka kuolewa umri
umekwenda hapo ukiwa ndani ya ndoa unaanza kusema kuwa hukupenda si ulitaka
mwenyewe na ukaona maamuzi na uchaguzi wako ni mzuri yanini unaanza kutuletea
shida
Kutaka kuoa/kuolewa utake wewe na kufanya maamuzi na uchaguzi wakuolewa/kuoa
ni wewe halafu kesi utuletee siye si ni majanga hayo.


RAFIKI FANYA UCHAGUZI WA BUSARA SASA USINGOJE KESHO FANYA LEO MAAMUZI
YA BUSARA

hebu twanga hapa uchaguzi wako unaoufanya rafiki

Wasaalaamu

Jael
 
^^
Jael lady
Ujumbe wako mzuri sana,,mimi nataka niishi peke angu bila mwenzi.Je ntakosea?
^^
 
Last edited by a moderator:
Charity begins at home!
Hujasema uchaguzi wako!!!!
 
Umenena vyema dadaangu....

Hii ni formula ambayo huwa naitumia siku zote, haijalishi kama itakula kwangu au lah!!!

Siwezi kuja kuolewa na mtu nisiyempenda kisa umri, shinikizo, show- off ama mimba. Lazima nifanye UCHAGUZI...

Na katika uchaguzi lazima nimchague nimpendaye lolest!!
 
mm napend kuchagua frien's(sna rafk wa kudumu), mshaur na mwenendo wa maisha yangu. LIFE IS BEAUTIFUL
 
Ni muhimu sana kwangu kuchagua mwenza sahihi tukayeendana kitabia na kuelewana...Na sitochagua kuolewa kwa sababu ya umri wangu au mimba...MAPENZI YA DHANI ni NO 1
 
Forever Himidini?sidhani kama ni uchaguzi mzuri huo kaka utakuwa mpweke sana!

^^
Ni historia ndefu Mapito ya mapenzi na ndoa yana mengi mimi49 how long utamsubiri wako?
^^
 
Last edited by a moderator:
Mpaka atakapopatikana na awe na ufunguo sahihi wa kuufungua huu moyo ulotiwa komeo :smile-big:

^^
Kuchanua kwa moyo wako na kuinuka kwa nuru yako ya mapenzi,ndio kutaleta ufunguo sahihi.
Urafiki usio na hila ndio utakufanya ujue ufunguo wenyewe,je huna rafiki/marafiki wenye dalili hizo?
^^
 
^^
Kuchanua kwa moyo wako na kuinuka kwa nuru yako ya mapenzi,ndio kutaleta ufunguo sahihi.
Urafiki usio na hila ndio utakufanya ujue ufunguo wenyewe,je huna rafiki/marafiki wenye dalili hizo?
^^
Ninae rafiki lkn siku zote mtu unafikiri huyu rafiki ana kila dalili ya kuwa na ufunguo wa moyo wangu wakati mwenzako hata hayupo huko kabisaaaa....
 
Ninae rafiki lkn siku zote mtu unafikiri huyu rafiki ana kila dalili ya kuwa na ufunguo wa moyo wangu wakati mwenzako hata hayupo huko kabisaaaa....

^^
Loo! Pole,ila unatakiwa uwe na subira sana ikiwa ni ivo,,mwenzio sina wa kusubiri,naopaswa kuwasindikiza kwenda wanakoenda wameenda..keep waiting mimi49
^^
 
Last edited by a moderator:
^^
Loo! Pole,ila unatakiwa uwe na subira sana ikiwa ni ivo,,mwenzio sina wa kusubiri,naopaswa kuwasindikiza kwenda wanakoenda wameenda..keep waiting mimi49
^^
Na vipi kuhusu ule usemi kwamba ukisubiri sana ndio unatupwa kwenye friends zone?Subiri subiri sana unakuta mwana si wako loh...
 
Na vipi kuhusu ule usemi kwamba ukisubiri sana ndio unatupwa kwenye friends zone?Subiri subiri sana unakuta mwana si wako loh...

^^
Naam lipo sana,,hasa ikiwa vigezo na masharti yako ni magumu kwa mwanaume kuya-archive..You have ur standards. mimi49 ufunguo wako unapatikana tu ikiwa unaujua ni upi..na unasomeka kirahisi tu
^^
 
Last edited by a moderator:
NOT EVERY BODY IS PRIVILLAGED WITH CHOICE. Some of us are just victims of circumstances. WE GOTTA DO WHAT WE GOTTA DO, WHEN WE GOTTA DO IT, NOT WHAT WE WANT TO DO OR ELSE WE FACE THE CONSEQUENCES.
 
UCHAGUZI NI UCHAAGUZI tu marafiki hata uchague vipi utamu unabaki kuwa palepale au siyo kaka Bujibuji?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom