Mwana MMU mwenzangu hili linawezekana kweli?

Mwana MMU mwenzangu hili linawezekana kweli?

yenyewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
621
Reaction score
94
Kuna jamaa yangu alikuwa na mpenz wake chuoni Mbeya, alikuwa anamtangulia mwaka mmoja.

Baada ya kumaliza chuo jamaa karud home mwanza na kumwacha mpenzi wake akiendelea na masomo ambapo nae akimaliza anaelekea kwao Iringa.

Ukizingatia jamaa bado hana kazi japo akijitahid akapata hata 10,000 anamtumia mpenzi wake aliye chuo.

Sasa jamaa yangu ana wasi wasi sana na amekuwa mtu wa kuomba ushauri kila kukicha, hana imani kama penzi lake litatunzwa kwa umbali uliopo na ukizingatia no way wanaweza kuonana kwa sasa na hawawezi kuoana kwa sababu bado hawajajipanga kimaisha.

Mwana JF mwenzangu tushirikiane kumshauri rafiki yangu kama huu uhusiano unawezekana au bora ajiengue mapema.

Asubuhi njema ndugu zangu.
 
Kama mtu anakupenda atakupenda ukiwa unacho na ukiwa huna sasa ndo ataona kama mpenzi wake mkweli au lahasha
 
mapenzi yapo na yalikuwepo na yataendelea kuwepo.....

fimbo ya mbali .........
atafute maisha na awekeze kwa future

mapenzi ya mbali yanahiaji uvumilivu na kama hamwamini ndo tress kabisa
 
Sasa hapo ushauri anaotaka nini yeye yupo mbali hana hela dah hapo pagumu.Kashaajiriwa au bado anabeba bahasha ya kaki?
 
Mwambie aache inferiority complexes zake, kama anamjua mpenz wake ni mpenda pesa ni bora kama hana pesa amuache kabla hajavunjwa moyo, kama anamjua ana mapenzi ya kweli aache kumfikiria vibaya mwisho wa siku hata akiwa busy na shule akashindwa kupokea simu yake ataona tayari anam-cheat, mwanaume jiamini.
 
atafute pesa kwanza na maisha mengine yatafuata.... uhusiano kukua na kuendelea kuwa pamoja inategemea na mapenzi ya hao wawili na uvumilivu pia
 
Mwambie aache inferiority complexes zake, kama anamjua mpenz wake ni mpenda pesa ni bora kama hana pesa amuache kabla hajavunjwa moyo, kama anamjua ana mapenzi ya kweli aache kumfikiria vibaya mwisho wa siku hata akiwa busy na shule akashindwa kupokea simu yake ataona tayari anam-cheat, mwanaume jiamini.

Asante ushauri umepokelewa
 
Mtoa mada nahisi wewe ndio uko mwanza

Afu kwa sikuizi ukiwa girlfriend usimueke kichwani Fanya kama uelewi
Kama wako wako tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom