Mwana HIP HOP Langa Kileo alianza lini Hip hop. Na alifariki lini?

Na alifariki lini?
 
Hivi watu wa HIP HOP.

Mwana HIP HOP Langa Kileo alianza lini Hip hop. Na alifariki lini?

Hivi Langa alitoa Album ngapi wakati wa uhai wa uhai wake.

Tujuzane ndugu zangu.

#forgive Me.
1682501809278.png
Marehemu Langa Kileo ni mmoja wa wasanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, ambaye alifariki mnamo mwaka 2013. Ni miaka 10 imepita ya kifo cha msanii huyo na tunaweza kutazama historia ya maisha yake binafsi, muziki, mafanikio, changamoto, na umauti wake.

Langa alizaliwa mwaka 1985 jijini Dar es Salaam, Tanzania. Alikuwa mtoto wa Vanessa Kimei na Mengisen Kileo. Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Olympio na baadaye akajiunga na Sekondari ya Loyola, zote za jijini Dar es Salaam. Akiwa kidato cha pili, alihama na kwenda Kampala, Uganda, ambako alisoma katika Shule ya Vienna na baadaye Shule ya Hillside International Academy. Baada ya kumaliza masomo yake, alirejea nchini Tanzania na kujiunga na Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma, ambapo alisoma Stashahada ya Masoko.

Kuhusu muziki, Langa alikuwa mmoja wa washindani wa shindano la Coca-Cola Pop Star mwaka 2004, ambalo lilimtoa msanii mkali wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Ali Kiba. Langa alishiriki shindano hilo akiwa na wenzake wawili, Sara Kaisi 'Shaa' na Witness Mwaijaga 'Witness', na waliunda kundi lilioitwa Wakilisha. Kundi hilo lilipata umaarufu mkubwa kwa nyimbo zao mbili za 'Unaniacha Hoi' na 'Kiswanglish'. Baadaye, Shaa aliacha kundi hilo na Langa na Witness waliendelea kufanya kazi pamoja. Walitoa wimbo unaokwenda kwa jina la 'No Chorus' ambao ulifanya vizuri sana.

Baada ya hapo, Langa alitoa wimbo wake wa kwanza akiwa kama msanii binafsi, ambao ulikuwa unaitwa 'Matawi ya Juu'. Wimbo huo uliingizwa katika mashindano ya MTV Base na baadaye ukashinda tuzo ya Kisima nchini Kenya. Langa pia alifanya kazi na wasanii wengine wa muziki wa hip hop nchini Tanzania kama vile Fid Q, na pia alifanya kazi na wasanii wa nje ya nchi kama kundi la Necessary Noise, Naaziz, na Wyre (Kevin Wyre).

Marehemu Langa alipitia changamoto nyingi katika maisha yake, ikiwa ni pamoja na kushindwa kuuza albamu yake ya 'Langa' baada ya kukataliwa na wasambazaji. Hii ilisababisha kuporomoka kwa maisha yake ya kimuziki na hatimaye kuingia katika maisha ya uteja wa madawa ya kulevya. Hata hivyo, baada ya jitihada za familia yake, aliweza kuondoka katika maisha hayo na kuendelea na kazi yake ya muziki. Aliachia nyimbo zingine kama vile 'Bombokiata' na 'Mteja Aliyepata Nafuu'.

Langa alifariki dunia kwa sababu ya Malaria kali iliyomshika, na alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi. Kifo chake kilishtua wengi, lakini kumbukumbu yake itaendelea kuishi kupitia muziki wake.

Kwa hakika, Langa Kileo alikuwa msanii wa kipekee na mwenye talanta kubwa katika muziki wa hip hop nchini Tanzania. Tunamkumbuka kwa mengi, ikiwa ni pamoja na mchango wake katika muziki na changamoto alizopitia katika maisha yake. Amani iwe juu ya roho yake.

Chanzo: facebook
 
Hua siingii kati naegemea ukuta, nakamatia viuno vilibyolegea mfupa...Mchunge mke, nasumu kama nge, niko full ka ikulu sipigi kazi za nnje.
Simsumbui mtu mimi na starehe zangu, maisha yenyewe mafupi sijui tarehe yangu!

Ukinicheki msafi, nchokoze uone moto
Sitokei masaki, natokea King'oko (King'ori Arusha?)
Demu siku moja mm simpigi lita, sijui amenyonya wangapi dakika zilizopita
Sipendi kulazimisha kama demu hataki,
Akikataa basi mwache apoteze bahati
 
Sitokei masaki, natokea King'oki (King'ori Arusha?)
Demu siku moja mm simpigi lita, sijui amenyonya wangapi dakika zilizopita
Sipendi kulazimisha kama demu hataki,
Akikataa basi mwache apoteze bahati
Jina la ngoma mkuu..
 
King'oko....Mikocheni
 
Hua siingii kati naegemea ukuta, nakamatia viuno vilibyolegea mfupa...Mchunge mke, nasumu kama nge, niko full ka ikulu sipigi kazi za nnje.
Simsumbui mtu mimi na starehe zangu, maisha yenyewe mafupi sijui tarehe yangu!

Ukinicheki msafi, nchokoze uone moto
Sitokei masaki, natokea King'oko (King'ori Arusha?)
Demu siku moja mm simpigi lita, sijui amenyonya wangapi dakika zilizopita
Sipendi kulazimisha kama demu hataki,
Akikataa basi mwache apoteze bahati
sio Arusha,aliirusha king'oko regent estate maskani kwao!

mbona jamaa hajawahi hata ishi huko king'ori!

ukitaka kuipata king'oko crew pina/kikosi cha mizinga kawachalazia sana kwenye pini lake la beef feat kimya from Kenya.
 
Ila baaday alikubali... kuna ngoma inaitwa Kifo, Jela, Umma au taasisi humo amefunguka vya kutosha
Dogo alikuwa talented sana,kuchwani alikuwa vzr....kasoma shule nzuri
Hiyo Vienna, kampala si masihara ujue
Makundi tu yalimuingiza kingi+ kuiga umbeleee
Alafu kuna wakati alipiga kazi barick gold,sema hakuweza kutulia kutokana na mambo fulani
Nahisi hata ndugu walikuja kujua too late, ila wangemuwahi mwanzoni wangemuokoa
Kuna wakati alihisi kutengwa,kukimbiwa na washkaji kutokana na hali yake,alikuwa anaenda resi sana

Wakati nlikuwa nakunywa sana PR CAMP BAR nyuma ya mwanamboka
Mimi binafsi nlishawahi kumface mzee kileo yule mzee owner,amchukue langa ampe mishe yyt pale kumuweka bize,maana alishakuwa junki badaye kweli mzee akamvuta pale akawa anazuga ila mbeleni km alizinguana na babu yk huyo
Inasikitisha sana kuona jinsi mwana alivyopotea gafla tu
RIP langa

Ova
 
Hua siingii kati naegemea ukuta, nakamatia viuno vilibyolegea mfupa...Mchunge mke, nasumu kama nge, niko full ka ikulu sipigi kazi za nnje.
Simsumbui mtu mimi na starehe zangu, maisha yenyewe mafupi sijui tarehe yangu!

Ukinicheki msafi, nchokoze uone moto
Sitokei masaki, natokea King'oko (King'ori Arusha?)
Demu siku moja mm simpigi lita, sijui amenyonya wangapi dakika zilizopita
Sipendi kulazimisha kama demu hataki,
Akikataa basi mwache apoteze bahati
King'oko ilikua camp Yao enzi hizo kina langa na baadhi ya wasaniii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom