Mwamunyange waonye wanasiasa wasilitumie jeshi vibaya

Mwalufunamba

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
211
129
Generali Mwamunyange, binafsi ninakuamini na kukuheshimu kutokana na busara yako kubwa katika maamuzi mengi niliyosikia umekwisha kuyafanya.

Kutokana na yale yanayotokea Mtwara,na yale yaliyowisha kutokea Arusha, Mbeya na Dar es salaam nawiwa kukuomba uwaonye wanasiasa kutokulitumia jeshi kwenye matatizo wanayoyasababisha wao kwa kutokuwajibika ipasavyo na kukimbilia kulitumia jeshi letu (JWTZ) lenye kupendwa, kuheshimiwa na kujivunia kwa kila mtanzania mzalendo.

Ni ukweli usiopingika kuwa utendaji kazi wa JWTZ unahitaji msaada na faraja kubwa toka kwa watanzania wote. Ni watanzania ndiyo wanawatoa watoto wao kujiunga na jeshi letu wakijua dhahiri iko siku wanao wanaweza kwenda vitani na kurudishiwa maiti badala ya wanao kurudi kama ashujaa. Wakirudi kama ashujaa wanashangilia, lakini wakirudi kama maiti watalia na kuomboleza lakini hawatalitupia lawama jeshi. Sasa kwanini wanasiasa wavivu wawe sababu ya kuwafanya watanzania walichukie jeshi lao?

Sasa hivi JWTZ limepeleka batalioni huko DRC, bado linahitaji support toka kwa umma wa watanzania. Mlikwenda Darfur, Somalia na hata Comoro mlipatiwa support na watanzania; la Kagera hilo silizungumzii ushahidi wa ushirikiano kati ya Jeshi na wananchi ulikuwa katika kiwango kilichotukuka katika historia ya Tanganyika na Tanzania.

Gen. Mwamunyange, tumeona yakianza kuibuka mazoea ya kulitumia jeshi vibaya kwa maslahi ya wanasiasa tofauti na tulivyozoea JWTZ kuwa ndugu zetu wa kutuokoa nyakati za majanga na shida na hata pale wageni wanapotishia usalama wetu (makaburu, RENAMO, waasi wa Congo, wanajeshi-majambazi toka Burundi, na isavya Nduli Idd Amini).

Mwaka 2010, Brig.Shimbo alilitumia Jeshi kutoa vitisho kwa wananchi kwa maslahi ya Kikwete, alifanya hivyo makusudi akijua wewe uko safarini. Kwa kauli za Shimbo, uliweza kusikia ni kwa kiasi gani watanzania walilinung'unikia jambo lile, si raia wa kawaida bali hata wanajeshi wenyewe.

Mwaka 2011, unakumbuka namna ambavyo viongozi wa mkoa wa Arusha na mwanasiasa toka Dar walivyotaka jeshi litumike kupambana na wana Arusha kwa lugha ya "kuongeza nguv u".. Nashukuru hukuridhia. Lakini, pia tuliona awali yake namna Jeshi la Polisi lilivyosababisha mauaji ya raia,..mambo yalipowawia magumu wakataka msaada wa JWTZ. Mgogoro mzima kiini chake ni kutokuwajibika kisiasa kwa wanasiasa walioko madarakani.

Mkoani Mbeya, kutokuwajibika kisiasa kwa Abbas Kandoro, kulifanya mgogoro kati ya wakazi wa Mbeya (wafanyabiashara) kuingia katika mapambano kati ya Polisi na wananchi , ambayo baadaye yalipelekea wanajeshi JKT-Itende na wale wa Mbalizi kuhusishwa kuingilia kati. Jambo lile liliwafadhaisha sana wanaMbeya na hasa wale wanajeshi ambao ni wazawa wa Mbeya.

Mkoani Dar es salaam, vivyo hivyo tena. Kushindwa kwa wanasiasa kushughuikia viashiria vyote vya chokochoko za kidini na kuegemea upande fulani wa dini, ndiko kulikopelekea kuzuka mgogoro wa kidini. Na kama haitoshi kundi la wale waliolelewa kujiona kwamba lina uwezo mkubwa wakakusudia kuleta vurugu Dar kwa maandamano. Ili kunyamazisha vurugu hizo, wanasiasa wakataka jeshi la Wananchi liingilie kati. Hili lilikuwa aibu kubwa, jeshi linatumiwa kusiko stahili.

La Mtwara, linajieleza vizuri. Namna wanasiasa wanavyoshindwa kulishughulikia tatizo lililowazi, kwa maslahi yao na si ya Taifa, kisha wanakimbilia kulitaka jeshi letu la JWTZ liingilie kati, si sawa hata kidogo. Gen Mwamunyange, unakumbuka wakati tunakwenda Msumbiji mlipata msaada mkubwa wa hawa wanaMtwara, iweje leo JWTZ igeuzwe kuwa adui wa wanaMtwara.Mbona kamb zo te zilizoko Mtwara na Lindi ni maeneo ya kujivunia kwa wana kusini?

Wanajeshi ambao wazazi wao ama ndugu zao watakuja kulema zwa au kuuliwa na wanajeshi wako, tena wakiwa wanaujua ukweli na kwamba walioenda huko walikwenda kulinda maslahi ya wanasiasa walioko Dar watajisikiaje?

Gen Mwamunyange, chukua hatua kwa kuwaambia wanasiasa huko huko ndani kwamba marufuku kulitumia jeshi kwa maslahi yao. Wawajibike kisiasa. Naamini kama angekuwa Gen Waitara angegomea mchezo huu. Naomba nawelilinde jeshi letu kuchezewa. Mkuu wa wilaya, wala mkuu wa Mkoa hawana ubavu wa kulitaka JWTZ liingilie kati, yupo aliyeko Dar anayeweza kuamrisha baada ya kukujulisha wewe.
 
mkuuu umenena, natamani mwamunyange kokote alipo apate hii taarifa..na ushauri wako
 
Ndiyo maana tunashauriwa mkuu wa nchi asiwateue majaji wakuu,wala mkuu wa police,labda mgombea mwenza tu ,hakuna serikali ya kishikaji aliyowahi kufanikiwa duniani,kenya tutawaona wanazidi kusonga mbele tu,sababu katiba yao inambana Rais kujichukulia madaraka ya kuteua teua tu mtu anaempenda yeye,huyu unaempa ujumbe huu hujui ni nani kwa hao watawala unaowasema<wanasiasa> japo unailenga ccm moja kwa moja na kule ccm wanasiasa niwakuhesabu ila jua bila kuondoa huu mtandao madarakani hakuna jipya litakalo kuja tokea chini yao.
 
Itafikia kipindi ata watoto wa Shule ya msingi wakiandamana polisi wakashindwa kuwazibiti JW wataitwa!
Then itabidi mtuweke wazi kuwa JW nao NI SEHEMU YA FFU
 
inaudhi sana kubadilisha jeshi letu kuwa FFU. Binafsi nalipenada sana Jeshi la Wananchi mpaka nikamshauri mdogo wangu wa damu ajiunge jeshini na akafanya hvyo na kufanikiwa kupelekwa kambi ya Nachingwea. Nasikitika sana kuwa ni mmoja wa majeruhi wa jana kwa kazi ambayo FFU angeweza kufanya. Namtakia mdogo wangu na wenzake nafuu ya haraka.
 
Hivi katika hicho chombo, nani mwenye sauti ya mwisho? Kwa Tanzania hii, sidhani kama itakuwa kama wale wa Misri au Tunisia.
 
Haa ha ha kwan commander in chief of army hamumjui?LMAO tehtehteh
Kesi ya ngedere anapelekewa nyani?huyo ni kada tu wa green hv mmemsahau yule mwingne alipoacha alikuwa anataka kukabidhiwa jimbo?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Swali ni...'washauriwa wanashaurika?' Hukumsikia Hosea alivyoyamwaga ubalozi wa Marekani?
 
Hawezi kuwaonya kwa kuwa wanasiasa haohao ndio wamempatia huo u CDF

Wanasiasa hawakumpa Ukuu wa Majeshi. Jeshi lina utaratibu wake kuwapata wakuu wa maheshi. Mwanasiasa alipojaribu kuingilia utaratibu huo Gen. mstaafu Waitara alimgomea. Mwanasiasa anajua pale ni nguma nzito maana aliambiwa kavukavu "jeshi tuna utaratibu wetu".
 
Hapo umesema ukweli mtupu mkuu. Katika vyombo vya dola tulivyonavyo hapa nchini, ni JWTZ pekee ndilo wananchi wengi wana imani nalo angalau kwa kiwango kikubwa.

Hii tabia ya kuanza kuwatumia katika mambo ya kisiasa itawafanya wananchi waanze kulichukia kama ilivyo kwa wengine hasa jeshi la policcm.
 
Hivi katika hicho chombo, nani mwenye sauti ya mwisho? Kwa Tanzania hii, sidhani kama itakuwa kama wale wa Misri au Tunisia.

Amiri Jeshi Mkuu ananguvu ya kisiasa tu juu ya Jeshi kwasababu jeshi halitendi wala kujihusisha na siasa. Amiri Jeshi hawezi kuamrisha Jeshi kufanya kitu bila ruhusa ya Mkuu wa Majeshi. Mkuu wa Majeshi akigoma hakuna kitakachofanyika. Wakianza kushindana, ahueni ya Amiri Jeshi Mkuu ni kulivunja Jeshi.
 
Swali ni...'washauriwa wanashaurika?' Hukumsikia Hosea alivyoyamwaga ubalozi wa Marekani?

Tunayemshauri ni Gen Mwamunyange. Yeye anashaurika. Na ndiye anayetakiwa kuwaambia ukweli wanasiasa kisha anaweka msimamo,"Marufuku kulitumia Jeshi kwenye matatizo wanayoyasababisha wanasiasa."
 
Naunga mkono hoja Gen. Mwamunyange kupiga maarufuku JWTZ kutumika kisiasa!
 
Tumeona watu mbalimbali wakipoteza maisha, wengine wakiporwa malizao sambamba na Kujeruhiwa vibaya.

Jeshi lilitumwa kutuliza fujo, na kuleta amani, Lakini hali ya mtwara imekuwa tofauti sana, Hawa askari wanapora Mali za wananchi kisha kuteketeza kwa moto kasri zao. Hawafanyi lolote zaidi ya kupora Mali za watu. Inasikitisha sana kuona Mambo yamsingi kama hata viongozi wetu kushindwa kuyatafutia ufumbuzi wa busara,

Majigambo yote ya CCM mmeshindwa kuitafuta ufumbuzi?? Au Ndio mlisha iuza mtwara sasa mnajutia?

MAFISADI WACHACHE WANATAKA KUTUARIBIA NCHIYETU. KATU HATUTA YAFUMBIA MACHO MAMBO YA KIALIFU KAMA CCM INAYO FANYA UKO MTWARA.
 
Back
Top Bottom