Mwamposa, ni vyema ukarekebisha baadhi ya vitu ambavyo ni kero kwa waumini wako na jamii kwa ujumla

Bado kuwafungisha msosi mpaka mfe.mwenye akili akishaona upuuz km huo ana acha kwenda hakuna mungu wa kwel kwa mwamposa
 
Mtumishi wa mungu ni vyema kuzingatia jamii na waumini wanataka nini katika maisha yao, yafuatayo ni kero nilizozibaini mimi kama miongon mwa waumini wake.

1. Ibada ndefu/ mpaka usiku inayopelekea usafiri kuwa wa shida, kumbuka waumini wengi wanategemea usafiri wa uma afu wanakaa mbali afu wana watoto na pengine hupelekea kukabwa usiku kwa waenda kwa miguu.

2.Kutokukemea dhambi, mimi ni mhudhuriaje mkubwa wa ibada kwa Mwamposa lakini skumbuk ni lini kakemea dhambi, ingawaje watu wanaenda pale wa kila aina, makahaba, malaya, wezi, mashoga n.k. Lakini mtumishi anadeal sana na kutoa baraka na upako pasipo kuhubiri amani,upendo,na maadili mema ukizingatia kuhusu jinamizi hili la ushoga, mtumishi ongelea ata hili tu kwa ufupi kanisa la mwamposa limekuwa kichaka cha watenda maovu, wanafurahia kutoongelewa. labda anahofia waumini kukimbia kanisa!?

3. Sadaka ni nyingi mmezipa majina mengi afu mnatoa baraka/upako kulingana na kipato cha mtu...yaan wewe mwenye elfu 5 unatofautishiwa baraka na yule mwenye kutoa elfu 50. Jambo hili linawafanya walio na kipato cha chini kujihisi wanyonge au kujihisi kupungukiwa na kitu..jambo hili binafsi linanikera na mnawapa adui zenu nafasi ya kupondea huduma hii.

4.Ukali(kufokewa).. mtumishi amekosa kauli ya kuwarekebisha watenda kazi wake pale wanapokosea amekuwa akiwadhalilisha kwa kuwafokea mbele za watu na mbele ya kamera kama mtumishi unapaswa kuwa mtaratibu kukemea kwa hekima kwa kutambua wengine ni watu wazima wana familia zao...utasikia toa hyu apa wekeni mtu sahihi pale...walinzi,washika maiki, camera man, wanafanya kazi kwa hofu kubwa sanaaa..waondolee hofu wafanyakazi wako!

Ni hayo tu niliyobaini mimi..naomba yeyote mwenye uwezo wa kufikisha haya ayafikishe kwa namna yyte ilee.... lakini pamojaa na hayo nimepokea muujiza kupitia ibada yake mungu ambariki na ajirekebishe ili huduma iwe rafik kwa wengi! Ahsanten na samahani kwa uandishi mbovu.
Watu tukiwa na shida tukakosa na akili tunageuka mandezi

Hivi ukiwa na akili timamu kabisa unaweza kusema Mwamposa anaendesha ibada yenye uhusiano na Mungu?

Kama kweli kuna kiama basi Mungu tuliyefundishwa kwamba ana wivu mkubwa ana kazi kubwa sana!

Binafsi hawa kina Mwamposa, Mzee wa upako, Geo Devie, Mwingira na wengine kama hao. Nadhani hawa ndo kesi study ya ukweli tuliyoletewa ya kwamba siku za mwisho kutakuwa na manabii wa uongo walioletwa na yule mwovu ibilisi.

Hawa ni kesi study ya ibilisi kabisa hivyo mtu mwenye akili timamu hawezi kushangaa kwanini mikutano yao watu wanajaa sana
 
Mwakasege miaka yote akiwa kwenye huduma mwisho ni saa 12 jioni watu wanatawanyika kwenda makwao.

Labda kama miaka hii amebadilika maana sijahudhuria miaka ya hivi karibuni.

Lakini zamani alikuwa na nidhamu kubwa ikifika saa 12 jioni watu wanatawanyika kurejea makwao.

Hata watumishi wengine ni hivyo mara nyingi.

Kabla giza kuingia saa 12 watu wanatawanyika ibada inaahirishwa.
 
Kujenga mahoteli si lazima uwe mchungaji au uwe na kanisa point hapa ni kwamba,

Kama makanisa lengo lake ni kuhubiri neno la Mungu kwa nini kuwepo na kipengele cha Sadaka?

Mungu muweza wa vyote anahitaji sadaka ya nini? Wakati yeye ana uwezo wa vyote?

Kanisa ni sehemu ya matapeli kupata pesa za wajinga wasio jitambua kwa jina la "Sadaka"

Watu mnadanganywa kwamba mtolee Mungu sadaka ,lakini hela hizo zina mnufaisha mchungaji wenu, Ninyi mkibaki na ufukara wenu.
sometimes! kukaa kimya ni hekima pia. ukisoma kumbukumbu la torati 12:5-9, malaki 3:8-12, mathayo 23:23-24. katika vitabu hapo juu, MUNGU anazungumzia kuhusu kumtolea sadaka, kupitia kuhani wake(NOTE:KUPITIA KUHANI WAKE) na faida utakayoipata wewe. kwahiyo sadaka ni agizo la MUNGU na sheria kama sheria nyingine. KUJIFUNZA ZAIDI; INGIA YOUTUBE NA UTAFUTE "ROBERT TV TANZANIA" hapo unaweza kupata maarifa za MUNGU. WATU WANGU WANAANGAMIZWA, KWA KUKOSA MAARIFA.
 
Naku uliza hivi,

Mungu muweza wa yote anahitaji sadaka ya nini? Wakati yeye anaweza yote?
 
ukisoma vitabu nilivyokuolodheshea, utapata jibu la swali lako. na kama bado kafuatilie youtube "ROBERT TV TANZANIA" Mungu kaweka sheria na kanuni kwa binadamu.
 
Kwanza, Mungu hayupo.

Pili, Hizo sheria unazo dai ziliwekwa na Mungu ni Sheria za wanadamu wachache wajanja walio unda mfumo wa kula hela za Wajinga kwa jina la Sadaka.

Tatu, Vitabu vyote vya kidini ni stori za kusadikika, Fiction stories.
 
UNAWEZA KUTHIBITISHA KUWA MUNGU HAYUPO!?
 
Na wewe unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Kitu kisicho kuwepo haki hitaji uthibitisho wa kuto kuwepo kwake kwa vile hakipo na hakijulikani.

Ukisema kitu kipo ndio unatakiwa uthibitishe kipoje.
 
Mimi ni mkristo lakini usimlalamikie mwamposa kumbuka imani haba ndio wanaoteseka ukiona mwenzio kapiga mihayo na ww tiyar unataka kupiga mihayo ukiona mwenzio kasimama anakojoa na ww mule mule unataka kukojoa vingine ni kuviacha vipite wala havikuongezei na kukupunguzia chochoye
 
Na wewe unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Kitu kisicho kuwepo haki hitaji uthibitisho wa kuto kuwepo kwake kwa vile hakipo na hakijulikani.

Ukisema kitu kipo ndio unatakiwa uthibitishe kipoje.
tunaomba na MUNGU anajibu! huo ndo uthibitisho kuwa Mungu yupo. siku ukiumwa na madaktari na waganga wakashindwa kukutibu, nitafute nikuonyeshe MUNGU. BINAFSI, MWAMPOSA NI NABII WA UWONGO. HAKUNA KUHANI WA MUNGU ASIYEHUBIRI KUWA UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA NA KUKEMEA DHAMBI. HAKUNA KUHANI WA MUNGU ANAYETOZA WATU FEDHA ILI WAPOKEE MIUJIZA YA MUNGU. YESU anasema; MMEPATA BURE, TOENI BURE.
 
Mtumishi wa mungu ni vyema kuzingatia jamii na waumini wanataka nini katika maisha yao, yafuatayo ni kero nilizozibaini mimi kama miongon mwa waumini wake.

1. Ibada ndefu/ mpaka usiku inayopelekea usafiri kuwa wa shida, kumbuka waumini wengi wanategemea usafiri wa uma afu wanakaa mbali afu wana watoto na pengine hupelekea kukabwa usiku kwa waenda kwa miguu.

2.Kutokukemea dhambi, mimi ni mhudhuriaje mkubwa wa ibada kwa Mwamposa lakini skumbuk ni lini kakemea dhambi, ingawaje watu wanaenda pale wa kila aina, makahaba, malaya, wezi, mashoga n.k. Lakini mtumishi anadeal sana na kutoa baraka na upako pasipo kuhubiri amani,upendo,na maadili mema ukizingatia kuhusu jinamizi hili la ushoga, mtumishi ongelea ata hili tu kwa ufupi kanisa la mwamposa limekuwa kichaka cha watenda maovu, wanafurahia kutoongelewa. labda anahofia waumini kukimbia kanisa!?

3. Sadaka ni nyingi mmezipa majina mengi afu mnatoa baraka/upako kulingana na kipato cha mtu...yaan wewe mwenye elfu 5 unatofautishiwa baraka na yule mwenye kutoa elfu 50. Jambo hili linawafanya walio na kipato cha chini kujihisi wanyonge au kujihisi kupungukiwa na kitu..jambo hili binafsi linanikera na mnawapa adui zenu nafasi ya kupondea huduma hii.

4.Ukali(kufokewa).. mtumishi amekosa kauli ya kuwarekebisha watenda kazi wake pale wanapokosea amekuwa akiwadhalilisha kwa kuwafokea mbele za watu na mbele ya kamera kama mtumishi unapaswa kuwa mtaratibu kukemea kwa hekima kwa kutambua wengine ni watu wazima wana familia zao...utasikia toa hyu apa wekeni mtu sahihi pale...walinzi,washika maiki, camera man, wanafanya kazi kwa hofu kubwa sanaaa..waondolee hofu wafanyakazi wako!

Ni hayo tu niliyobaini mimi..naomba yeyote mwenye uwezo wa kufikisha haya ayafikishe kwa namna yyte ilee.... lakini pamojaa na hayo nimepokea muujiza kupitia ibada yake mungu ambariki na ajirekebishe ili huduma iwe rafik kwa wengi! Ahsanten na samahani kwa uandishi mbovu.
Hiyo namba 3 ndio ulipo utapeli wa Hawa jamaa, hata Marehemu Rwakatare alikuwa nayo hii.
 
yangoswe muachie ngoswe labda kama hujui siku hizi wanahubiri mafanikio ukitaka gari Nyumba mtoto mke pisi Kali zamani walikuwa wanahubiri wokovu ndio maana walikuwa wachache makanisani na mapato yalikuwa hafifu sana
Swali kwako mkuu, iv kuhubiriwa mafanikio ni jambo baya unataka ahubiri umaskini! swala kama ni kuhubiri mafanikio mbna hata motivation speaker hawatupiwi lawama watu wanaangalia out come baada ya mahubiri yako
 
Watu tukiwa na shida tukakosa na akili tunageuka mandezi

Hivi ukiwa na akili timamu kabisa unaweza kusema Mwamposa anaendesha ibada yenye uhusiano na Mungu?

Kama kweli kuna kiama basi Mungu tuliyefundishwa kwamba ana wivu mkubwa ana kazi kubwa sana!

Binafsi hawa kina Mwamposa, Mzee wa upako, Geo Devie, Mwingira na wengine kama hao. Nadhani hawa ndo kesi study ya ukweli tuliyoletewa ya kwamba siku za mwisho kutakuwa na manabii wa uongo walioletwa na yule mwovu ibilisi.

Hawa ni kesi study ya ibilisi kabisa hivyo mtu mwenye akili timamu hawezi kushangaa kwanini mikutano yao watu wanajaa sana
kujaza watu mbna hata CCM na chadema wanajaza watu! na hujawahi lalamika mkuu
 
Naku uliza hivi,

Mungu muweza wa yote anahitaji sadaka ya nini? Wakati yeye anaweza yote?
Swali zuri, subiri atakujibu! sasa mimi nikuulize wewe unahisi mungu anahitaji nini kutoka kwako...nakazia...wajibu wako ni nini kwa mungu au mungu amekuumba ili iweje.... nasubiri majibu..kama hujui wajibu wako kwa mungu basi huna sababu ya kuwepo duniani!
 
Back
Top Bottom