Heparin
Senior Member
- Sep 24, 2021
- 127
- 420
Nawasalimu wote kwa jina la Upendo. Amani, baraka na neema za Mwenyezi Mungu ziwe pamoja nanyi.
Kwa wakristu, hongereni kwa kuingia nusu ya pili ya mfungo wenu. Pia, nawatakia ndugu zangu waislam mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mwenyezi Mungu awakirimie Neema na azipokee sala na funga zenu.
Pasipo kuathiri imani na ibada yao kwa Mungu, nataka nitoe maoni yangu kuhusu uzembe uliopo Tanganyika Packers, kwa waumini wanaosali kwa Mtume Mwamposa.
Binafsi, sina shida yoyote na kusali kwao. Isipokuwa, kumekuwepo na tabia ya watu hawa kulala chini, kwenye uwanja wa wazi usiku kucha wakisubiri huduma hii.
Jumatatu moja Mwaka jana mwezi wa 7 wakati naanza kazi kwenye taasisi moja iliyo karibu na maeneo haya, nilishangaa kuona kusanyiko kubwa la watu waliolala chini ambao kwa hesabu ya haraka hawakuwa pungufu ya 500.
Katika kundi hilo, idadi kubwa ya watu walikuwepo ni wazee, wajawazito na wanawake wenye watoto wachanga sana. Hali hii haikuishia siku hiyo, imekuwepo hadi sasa.
Sehemu ndogo ya makundi ya watu waliolala hapo usiku wa kuamkia leo Machi 23, 2023
Mtu yeyote mwenye akili timamu hahitaji elimu ya sayari ya 5 kuona kuwa mazingira haya ni hatari kwa afya ya wahusika.
Kwa kuwa mimi ni mtu mwenye elimu ya fani fulani ya afya, inayohusika na kushughulikia wagonjwa moja kwa moja, huwa nawaza sana kila ninapoona watu hawa asubuhi. Fikiria hali ya sasa ya mvua, kisha mtazame mzee, au mwanamke mjamzito, mama mwenye mtoto mchanga au mgonjwa wa kisukari, presha au kifafa anayelala hapo usiku kucha kwa siku kadhaa akisubiria huduma.
Kibaya zaidi, sehemu za kujisaidia na kupata huduma muhimu za kibinadamu hazitoshi. Mathalani, ukipita hapo asubuhi utakuta watu wanapiga mswaki hadharani na kutema uchafu barabarani, au hata sehemu ileile ambayo huitumia kulala wakati wa usiku.
Baridi kali na vumbi ni chanzo cha magonjwa mengi hasa kwa watoto na wazee. Badala ya kupata huduma za kiroho, watu hawa wanaweza kuondoka hapo wakiwa na mzigo wa magonjwa mengine makubwa zaidi.
Naomba Serikali itazame suala hili kwa umakini. Kama imeshindwa kabisa kuweka utaratibu mzuri wa kumbana Mwamposa kwa kuwa yeye ndiye kiongozi, basi miundombinu ya eneo hili iboreshwe.
Kuacha hali hii iendelee ikiwa hivi itasababisha maafa makubwa. Uponyaji wa kiroho unapaswa kwenda pamoja na uponyaji wa kimwili.
Naomba kutoa hoja!