Mkuu wewe baada ya kuona hivyo ulichukua hatua gani ?
Hujatuambia pia huyo mtoto alikua anaadhibiwa kwa kosa lipi ?
Japo kumuadhibu mtoto ni njia ya kumfundisha lakini Mzazi anapaswa awe na uelewa jinsi ya kumuadhibu mwanaye , sio mtoto anapigwa kama mwizi kisa anaadhibiwa .
Wazazi tuelimishane kwenye hili , Japo malezi yanatofautiana na kila mtu anaamini kivyake katika vitu kama hivyo.
Napingana na vitendo vya wazazi wanaoadhibu watoto kama wanapiga mwizi.
Hilo ndio la muhimu Mkuu , kumnusuru huyo mtoto ndio jambo la kwanza mengine yatafuata.mimi hata nisingetaka hata kujua kosa lake, ningeamua kwanza mengine baadaye.
Hapana pia ungekuwa hatiani kwani inahitaji busara kuamua mambo kama haya pia kumuelemisha mwanamama namna ya kuishi na mtoto pia matokeo ya baadae
Chanzo ni wanaumeNimeshuhudia mwanamke anamuadhibu mwanae kama nyoka, kipigo alichopigwa yule mtoto ni ajabu maana inafikia mzazi unamuumiza mtoto wa miaka mitano huu ni ukatili. Wanawake tuwe na upendo kwa wanetu jamani kwani hata sie kama tungelelewa kwa njia hiyo ya kikatili nadhani tusingefika.
We ulichukua hatua gani? Au ndio hii ya kuja kuanzisha mada?Ni wake wa kuzaa wana jamii ila kwa adhabu ile haikumstaili hata kama alikua na kosa.