Mwalimu wa dini (Ustaadhi) ahukumiwa kifungo jela baada ya kumlawiti mtoto wa kiume

Hawa watu hizi hukumu za miaka 30 ngome zinawapa kiburi,ipitishwe sheria mtu akimnajisi mwenzake ale kitanzi tu maana hii hali inatuongezea matatizo kwenye jamii.
 
aliyewaroga hawa walimu alitenda dhambi kubwa sana huyo ni mmoja kati ya walimu kenda wa kenda wenye kutenda uchafu huo nchini.
 
Nilipoona title tu nikahisi atakuwa ni mwl wa madrassa. Ndo zao tangu enzi na enzi.
13fa3b1d333ce7f5a192613c35960852.jpg
 
Huyu kaanza kuzishughulikia bikra hapa hapa na zingine 72 zinamsubiri peponi
 
Hakuna asiyekosea.
Msianze kuingiza mambo ya dini hapa.
Huyo kakosea basi muacheni ajute na sheria ifuate mkondo wake.
 
Wewe ni mjinga na zuzu kuliko wote hapa jf..
Kama ni kweli basi sawa kuadhibiwa.
Ila nilishawahi simuliwa na mtu mmoja ambaye alikua kiongozi wa dini wa upande wa pili na akasema. Hawapendezwi na mafunzo wanayopata watoto wa madrasa ambayo inapelekea kuwa na misimamo thabiti kwenye dini.
Wanachofanya sasa ni kwanza kumuandaa mzazi mmoja ambaye atakuwa tayari kwenda polisi kufungua kesi ya uzushi ya kubaka dhidi ya mwalim yoyote wa madrasa kisha anakwambia huko mbele anawaachia wao jukumu la kuweka mazingira favaourable upande wa mzazi aliyezusha mwanawe kalawatiwa.
Hivyo ndio dini ya kiislam anavyopigwa vita kwa njia mbali mbali kabisa tena kushirikiana na taasisi nyingi za uma tena nyeti.
 
TUESDAY, OCTOBER 3, 2017

Mwalimu wa madrasa jela miaka 30 kwa kulawiti
By Hadija Jumanne, Mwananchi hjumanne@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwalimu wa madrasa, Abdillah Sharifu, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka 11.

Sharifu (30), mkazi wa Gongo la Mboto eneo la Moshi Baa amehukumiwa kifungo leo Jumanne katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala.

Mshtakiwa anadaiwa kumlawiti mtoto huyo na pia kumtishia kuwa angemroga endapo angetoa taarifa kwa wazazi wake kuwa anamfanyia kitendo hicho.

Akisoma hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan amesema ameridhishwa na ushahidi wa mashahidi wanne akiwemo daktari.

"Mshtakiwa nimekutia hatiani kama ulivyoshtakiwa, ninakuhukumu kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwako na watu wengine wenye tabia mbaya kama hii," amesema.

Hakimu Hassan amesema kitendo kilichofanywa na mshtakiwa ambaye ni mwalimu wa dini ni cha kikatili.

Akipitia ushahidi wa upande wa mashtaka, hakimu Hassan amesema shahidi wa kwanza ambaye ni mtoto huyo aliieleza Mahakama kuwa mshtakiwa Februari 25 alimtaka kwenda nyumbani kwake.

Baada ya kufika nyumbani kwa mshtakiwa ambaye mke wake ana tatizo la kutoona, shahidi huyo alieleza alitakiwa kuvua nguo kitendo ambacho pia kilifanywa na Sharifu.

Shahidi huyo aliieleza Mahakama kuwa mshtakiwa alimfanyia ukatili huo, huku akimtishia kuwa iwapo angethubutu kutoa siri hiyo angemroga.

“Mara kwa mara alikuwa akinifanyia mchezo huu hadi nilipomwambia mama na kisha kwenda kufungua kesi katika kituo cha polisi Mazizini,” alisema mtoto huyo katika ushahidi alioutoa mahakamani.

Katika ushahidi wa mama mzazi wa mtoto huyo, alidai baada ya kuripoti polisi walikwenda hospitali ambako kwa mujibu wa vipimo vya daktari licha ya kutokuwa na michubuko ilionekana aliingiliwa.

Mshtakiwa alidai ana mke kipofu na kwamba, hafanyi vitendo hivyo isipokuwa alikuwa na ugomvi na mama wa mtoto huyo na ndiyo sababu ya kumfungulia kesi.

Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kuifafanulia Mahakama chanzo cha ugomvi hivyo ilitupilia mbali utetezi wake na kumtia hatiani.

Awali, Wakili wa Serikali, Grace Mwanga aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za kulawiti watoto na wanaotumia kimvuli cha nyumba za ibada kufanya ukatili.

Mshtakiwa alitenda kosa hilo, Februari 25 katika eneo la Moshi Baa, Gongo la Mboto.
Madrasa inatakiwa zivunjwe zote.
Subir nimuite huyu faiza foxy
 
Unampa mimba mwanafunzi tena pengne mmepatana unakula 30, na lijitu kma hili nalo 30? Hiv n kwamba bongo hivyo vifaa vya kunyongea hamna?
 
Back
Top Bottom