Twilumba
JF-Expert Member
- Dec 5, 2010
- 11,542
- 12,404
WanaJf Habari za Mchana kutwa!
Nilihudhuria Sherehe za Mei Mosi, mahala furani kimsingi hapo ilikuwa ni maadhimisho ki-wilaya.
Walimu walikuwa wamepangwa kutumbuiza kwa Mashairi na Ngonjera ki ukweli niliona ubunifu wa walimu wale kwa jinsi walivyopangilia yale mashairi.
Lakini ghafla niliingiwa na huzuni baada ya Beti Mbili za Shairi lile kuweka bayana kuwa kuna gap kubwa sana kati ya walimu na watumishi wa idara ya afya wahudumu wa sekta ya afya na wauguzi.
Ilimiia majonzi jinsi walimu wale walivyoliweka lalamiko hili kiushairi ni kama walikuwa nalia na kujuta kwa nini wamekuwa walimu.
Mathalani wansema mwalimu aliyehitimu Ngazi ya Cheti analipwa Ngazi ya Mshahara TGTS B/1 -Sh 210,000 wakati Mhitimu wa Cheti cha Uhudumu wa Afya (Medical attendant) analipwa ngazi ya Mshahara TGHS B/1- shilingi 415,000 ikiwa na maana kuna tofauti ya shilingi 205,000/=!
Swali langu hapa ni kwa nini hawa wote mwalimu na mhudumu wa Afya wasilipwe kiwango sawa maana mwalimu na mhudumu wa Afya kwa kweli naona wote ugumu wa kazi unafanana!
Je serikali haijaona kama kuna ulazima wa kuondoa gap hili ambalo pengine linachangia kudumaza kiwango cha Elimu Nchini?
NAOMBA KUWASILISHA KWA MJADALA!