Mwalimu Nyerere na ukabila


South Africa, its a different story alafu siongelei ubaguzi wa rangi wala kumkandamiza mtu sababu ya imani yake au jinsi alivyo ninachoongelea kuna watu inabidi uwaonyeshe kwamba kuna sheria na kuna state ambayo inabidi ieshimiwe, hakuna ubishi.., good example ni England sasa hivi too much usawa na political correctness imefanya hadi mtoto mdogo anahaki ambapo mzazi inabidi aangalie mara mbili kabla hajamkana.., that is political correctness going mad..., so in Iraq and Libya kama hakuna power ya kuonyesha kwamba you cant just run amok and get out scot free (kama enzi za Saddam)...., maybe all those crazy people will take advantage..., As the saying goes its like Lunatics Running the Asylum
 

pole sana...........
 

Ni vizuri tukumbushane kwamba Nyerere hakuomba uhuru kama mtu binafsi bali alifanya hivyo kwa kushirikiana na watanganyika wenzake, na kwa kweli watanganyika wengi sana walitaka wawe huru, kuna vibaraka wachache waliokuwa kwenye utumishi wa serikali ya mkoloni hawakuona haraka ya kupata uhuru.

Hatahivyo ni vizuri kukumbuka kwamba watanganyika wenyewe ndio walimchagua Nyerere awaongoze, hakujichagua mwenyewe.
Kama utasema kwamba haumeet expectations alizoongelea wakati akipigania uhuru nitakwambia hapana, tena hapana kubwa. Kuna mambo mengi sana ya maana na ya kukumbukwa Nyerere kawafanyia watanganyika na watanzania, na hata hivyo alifika mahali akaamua kwa hiari yake kung'atuka, inawezekana ni baada ya kurealise kwamba anahitajika mtu mwingine aje na mawazo yake kwa ajili ya maendeleo ya watanzania, tofauti na viongozi wengine wa kiafrika walioziletea nchi zao uhuru na kugeuza ikulu kuwa mali binafsi ya familia zao, mifano hai ipo huitaji nikutajie.
 
"Thread inazungumzia Nyerere na ukabila" Halafu kuna jamaa hapo juu asiye na matatizo ya uelewa ameandika hivi: "Nyerere alikuwa na mawazo finyu alizuia tv....!!" Naona kweli kwenye vipaumbele vyake angewawekea tv watu wa mijini wa wakati huo wafaidi maisha!!
 
Nilisikia kwamba na TV pia hakupenda watu binafsi wamiliki!Hicho kitabu kinaitwaje?!Ningefurahi kweli kukipata!!!

Ukisoma historia ya ICT katika TZ, wanasema miaka ya 70 kulikuwa na uhamasishaji mkubwa kuhusiana na matumizi ya redio hadi mashuleni. Kwahiyo sioni kama ishu ilikuwa kuzuia habari. Pia tukumbuke TV zilikuwa banned pamoja na kompyuta kwa wakati mmoja kwa watumiaji binafsi.
 


wewe kweli una matatizo ya kuelewa
nimeainisha hapo faida za tv nyingi mpaka mashuleni zinatumika
kama zanzibar waliweza kuwa na tv miaka hiyo
we unafikiri tanganyika ingeshindikana vipi????
vipaumbele vingeathiri vipi hilo?
au kipaumbele cha kuchangisha watu pesa za mbio za mwenge we ndo unaona cha maana??????

mnamsifia nyerere hata sifa ambazo sio zake

eti alijenga reli ya kati,na wakoloni waliacha reli ipi?????

kusema tv ni anasa
na magari ni anasa
namatrekta ni anasa ni mawazo finyu mno
period
 
Alichoamini kama hakikua kizuri alifanya kwa faida ya nani?!?!Nani anaejua kwa uhakika kwamba angeruhusu hayo makabila kuongoza huo “undugunization“ ungetawala?!
Umenikumbusha enzi za Gibonsi Mwaikambo aliyekuwa bosi wa benki. Fuatilia habari yake...
 

Nina wasiwasi huenda mzee wako alikuwa mhujumu uchumi kweli, miaka ya themanini dukani ana khanga ya mwatex na dola 500? alizitoa wapi dolari miaka hiyo? Halafu usiiruhusu chuki uliyonayo dhidi ya mwalimu ukasahau kwamba operesheni ya kuwakamata wahujumu uchumi ilitikisa kila kona ya nchi chini ya usimamizi makini wa Sokoine na mimi binafsi nilishuhudia hao hao wazanaki na wakurya wakisombwa kwenda kizuizini kwa tuhuma hizo hizo za uhujumu uchumi kwahiyo hakuna ukabila hapo!!
 

ukisikia ugonjwa ndo huo
yaani tanzania ilikuwa juu kwa ict wakati computer na tv zilikuwa banned????????
so radio tanzania ndio ilitufanya tuwe juu sio???????/
kipindi cha mikingamo sio?????????
 
Mie naweza kukuhakikishia Mwl Nyerere haku-meet expectations kama alizotarajia! sababu kuu ni kwamba kabla ya uhuru hakuwa na ideologies kama za Ujamaa na self reliance hata chembe maana nina uhakika hata huo uhuru wenyewe usingepatikana kuna sehemu kubwa ya wananchi waliom-support wangempinga! Ni baada ya kuona mambo yanaenda Mrama kila kitu hakiendi na at climax mutiny attempt nathani 1964 ndipo akaenda uchina akarudi na all the ideas za Ujamaa+plus dress code na pia akavunja na jeshi loote...na wafanyabiashara wakawa publicly anounced a great threat to his government alichofanya tofauti ni kuita African socialism ambayo unfortunately was never experimented anywhere ila we were made to be guinea pigs! ili kuwa a bit neutral to the cold war foes!
 

I bet u would kill to just achieve 1% of what Nyerere did!

Sijawahi kuona mwenye akili finyu akipewa "standing ovation" na bunge la SA!
 

nimegundua humu ndani
watu wa nyerere hawana cha kuzungumza
mbele ya geza ulole.
 
ukisikia ugonjwa ndo huo
yaani tanzania ilikuwa juu kwa ict wakati computer na tv zilikuwa banned????????
so radio tanzania ndio ilitufanya tuwe juu sio???????/
kipindi cha mikingamo sio?????????
hizo redio zilikuwa zinashika masafa yapi? acha uzushi wewe....!
 

Myth and speculations!
 
I bet u would kill to just achieve 1% of what Nyerere did!

Sijawahi kuona mwenye akili finyu akipewa "standing ovation" na bunge la SA!

umeona ulivyo finyu na wewe????????
kila anaepewa standing ovation ana mawazo sahihi sio???????
na kila anaekaribishwa white house je????????
we uliona ziara ya mobutu marekani???????
umewahi ona standing ovation za madikteta wengi tu?
hivi unajua hata iddi amin aliwahi kuwa mwenyekiti wa oau??????

manake nyinyi mnawa brain wash watoto eti
nyerere alikuwa mwenyekiti wa oau
ha ha haaa,so what???????hata mobutu na iddi amini aliwahi kuwa
wenyeviti wa oau.
 

Nyerere alikuwa anaamini katika itikadi ya ujamaa, na kama ilivyo itikadi nyengine, itakadi ya ujamaa ilikuwa na misingi yake na mojawapo ni serikali ama dola kuwa muhimili mkuu wa kila shughuli kuanzia shughuli za kiuchumi, huduma za jamii hadi uzalishaji.

Sasa utaona hapo kwamba hao watu wa vyama vya ushirika hakuwakandamiza kwa sababu alikuwa na chuki nao, isipokuwa ni katika kutekeleza sera za ujamaa alizokuwa akiziamini, na kwa misingi ya itikadi hiyo serikali ililazimika kuhodhi nyanja zote.

Na kwakuwa itikadi ya ujamaa imeonekana kuwa ngumu kuitekeleza kutokana na nature ya binadamu pamoja mazingira yote kama alivyoeleza hapo kabla VOR basi utaona kwamba alikuwa akifanya hivyo kwa nia jjema na kwa kusimamia itikadi aliyoiaminina wala si kwa ubinafsi.
 
nimegundua humu ndani
watu wa nyerere hawana cha kuzungumza
mbele ya geza ulole.

Naona unajitahidi kujinasibisha na geza ulole kwa kasi sana.

Rudi kule ukatetee utumbo wako, achana na geza ulole tunakwenda naye vizuri ili kufahamisha na kubadilishana uzoefu na uelewa sio wewe kila saa kurukia ncha ya mkuki wa geza ulole!!
 
wacha we itikadi za ujamaa zilikuja baada ya mambo kubuma! ukiangalia vizuri hata harakati zetu za kupigania uhuru zilitu-exclude na any sort ya totally alignment towards the two cold war players! we were so fortunate unlike the rest of African nations at the time so huwezi kusema alikuwa Mjamaa hapo kabla u r practically misrepresenting facts!
 

Mapambano ya kudai uhuru yaliongozwa na TANU chini ya uongozi wa mwalimu. Kwahiyo hoja kwamba uhuru ungekosekana sehemu kubwa ya watunwaliomsupport wangempinga ni hisia zako tu kutokana na mtazamo wako binafsi na wala hakuna uhalisia wowote.
Watanganyika waliokuwa wanadai uhuru hakuwa nyerere peke yake, ukumbuke hadi nyerere anakuja kupewa uenyekiti wa TANU alikuta tayari harakati za kudai uhuru zimeshaanza na zinazidi kupamba moto kwahiyo alichofanya yeye ni kuunganisha nguvu na watanganyika wenzake na kutokana wao kumuamini na kumpa uenyekiti wa chama basi ilibidi aongoze mapambano. Kwahiyo kama uhuru ungekosekana labda tanu ndiyo ingepingwa na si nyerere.
 

Mwita Maranya,

..binafsi naamini uamuzi wa Mwalimu wa kutaifisha shule za binafsi na madhehebu ya dini ulikuwa na makosa.

..alichopaswa kufanya Mwalimu ni kujenga shule za serikali akielekeza nguvu zaidi maeneo ambayo yalikuwa yameachwa nyuma.

..kosa lingine ni ule utaratibu wa quota system ambapo wanafunzi ambao hawakuwa qualified walipewa nafasi za kuendelea na masomo.

..nakubaliana na dhima nzima ya kutoa elimu kwa wa-Tanzania wote, lakini nadhani juhudi hazikufanyika kuhakikisha kwamba tunatoa ELIMU BORA KWA WOTE, na mipango kama quota system ilikuwa inaficha deficiencies ktk mfumo wa utoaji elimu wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

..kitu kinachosikitisha ni kwamba mpaka leo hii usawa haujapatikana na zaidi elimu yetu imeshuka kiwango kiasi cha kutisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…