VoiceOfReason
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,194
- 1,375
Ukweli ni kwamba Nyerere alikuwa dikteta kwa definition ya udikteta ya Ulaya Magharibi (by then). Ila kwa viwango vya Africa kwa wakati huo Nyerere alikuwa nafuu sana kulinganisha na viongozi wengine Madkiteta wa Africa ambao walikuwa wakiwaua wapinzani wao kwa maelfu. Nyerere alikuwa akiwanyima uhuru wapinzani wake kwa kuwapeleka huko vijijini na hawakutakiwa kufika mjini kujua nini kinaendelea. Mfano Kasanga Tumbo na Mzee Mapalala! Alikuwa Dikteta ila alikuwa si muuaji kama madikteta wengine wa Afrika wa enzi zake.
Mkuu nami nilikuwepo na nipo hadi sasa. Pamoja na kuwasweka ndani watu lakini Nyerere alikuwa akipendwa na wengi. Huwezi kupendwa na kila mtu lazima wawepo wengine ambao hawakupendi lakini kwa ujumla ni kwamba alikuwa anapendwa. Kuhusu kukoswa koswa kupinduliwa ukilinganisha na Marais wengine utakuwa hutendi haki kwa kuwa kwenye miaka ya 90s Africa ilianza kunusa demokrasia ukilinganisha na miaka ya 60s na 70s ambapo demokrasia kwa Africa ilikuwa ndoto. Kipindi baada ya uhuru kwa nchi nyingi Africa kilitawaliwa na ubabe pamoja na udikteta kwa hiyo waroho wa Madaraka waliona hakuna njia nyingine ya kuchukua hatamu za uongozi zaidi ya kutumia mtutu wa bunduki. Miaka baada ya uhuru kulikuwa hakuna chaguzi za ushindani africa, vyama vingi vya siasa vilipigwa marufuku.
Kuhusu mada ni kwamba Nyerere hakuwa mkabila wa waziwazi lakini alikuwa na vimelea vya ukabila. Hakupenda Makabila kama Wachaga ambao wengi waliosomeshwa kupitia KNCU, Wahaya kupitia KCU pamoja na Wanyakyusa (ambao sijui walipata wapi bahati ya kusoma) waje kuchukua uongozi wa juu wa nchi kwa kuwa wangekuwa na solidarity na kupeana madaraka na kuyapuuza makabila mengine kama wakurya ambao elimu yao ilikuwa chini sana baada ya wakoloni kuwaona kuwa wanaweza tu kufungua bunduki na kupiga na wala siyo kufungua kurasa za vitabu.
Nilisikia kwamba na TV pia hakupenda watu binafsi wamiliki!Hicho kitabu kinaitwaje?!Ningefurahi kweli kukipata!!!kuna story ameandika edwin mteikwenye kitabu chake ukiisomana ukisikia uvumi kuwa alikuwa na matatizo ya kama ugonjwa hivi wa mentall hivi unaweza connect the dotsmfano nyerere alikuwa impulsive sanaanalipuka lipuka mno....kwenye kitabu mtei anasema aliwapeleka wazungu wa imf ikulu,nyerere badala hata ya kuwasikilza na kukataa,akasusa kuonana nao.wakati mwanzo alikubali waje ikulu.yaani aibu tupu,mtei akamkuta nyerere yuko nje ya ikulu kanuna hataki hata kuongea...na ukichanganya na jinsi zoezi la vijiji vya ujamaa lilivyopelekwayaani watu walihamishwa wakapelekwa kwenye mapori waanzishe hivyo vijiji wengine wakaliwa na simbana ukiangalia mfano sera yake ya marufuku magari,ni baiskeli tuunaweza ona
Alichoamini kama hakikua kizuri alifanya kwa faida ya nani?!?!Nani anaejua kwa uhakika kwamba angeruhusu hayo makabila kuongoza huo undugunization ungetawala?!Nadhani tusiangalie aliyoyasema bali aliyoyafanya na impact zake; na tujiulize isingekuwa hivyo tungekuwa wapi......Baadhi ya makabila sababu ya undugunization yangekuwa juu zaidi hata kushinda ilivyo sasa, therefore kuleta matabaka makubwa, (Chagga, Haya to name just a Few)Maybe baada ya kuona wenzetu wa mikoa ya Mara n.k. (kulingana na what is even happening now) ilikuwa ni vema waingie kwenye jeshi to utilize their fighting spiritKwahiyo kwa kutumia tactics na kuona culture and strengths za kila kabila directly or indirectly aliwabana au kuwaachia katika nyanja tofauti..., sio kwamba ni mkabila bali ni kwa kufanya kile alichoamini be it good or bad...
kwenye kitabu mtei anasema aliwapeleka wazungu wa imf ikulu,
nyerere badala hata ya kuwasikilza na kukataa,akasusa kuonana nao.
wakati mwanzo alikubali waje ikulu.
yaani aibu tupu,mtei akamkuta nyerere yuko nje ya ikulu kanuna hataki hata kuongea...
Sina haja ya kubishana kuhusu nyerere, lakini wewe mwenyewe jijibu kuhusu hayo makabila uliyoyataja, Jee, ndio hao hao? halafu ongeza waislaam ambao aliwafunga masheikh wao wakubwa woote, hakuna sheikh wa kiislaam aliyekuwa maarufu ambae hajaonja joto la chuki za nyerere. Ukisha waongeza hao na wafuasi wao, ongeza na watu kama Mwamwindi walikuwa wangapi? halafu ongeza wafuasi wakina Kambona, Kasela Bantu, Bibi Titi na waliokama hao, ukipata jibu. Utajaza mwenyewe.
Nilisikia kwamba na TV pia hakupenda watu binafsi wamiliki!Hicho kitabu kinaitwaje?!Ningefurahi kweli kukipata!!!
Alichoamini kama hakikua kizuri alifanya kwa faida ya nani?!?!Nani anaejua kwa uhakika kwamba angeruhusu hayo makabila kuongoza huo "undugunization" ungetawala?!
Mkuu nami nilikuwepo na nipo hadi sasa. Pamoja na kuwasweka ndani watu lakini Nyerere alikuwa akipendwa na wengi. Huwezi kupendwa na kila mtu lazima wawepo wengine ambao hawakupendi lakini kwa ujumla ni kwamba alikuwa anapendwa. Kuhusu kukoswa koswa kupinduliwa ukilinganisha na Marais wengine utakuwa hutendi haki kwa kuwa kwenye miaka ya 90s Africa ilianza kunusa demokrasia ukilinganisha na miaka ya 60s na 70s ambapo demokrasia kwa Africa ilikuwa ndoto. Kipindi baada ya uhuru kwa nchi nyingi Africa kilitawaliwa na ubabe pamoja na udikteta kwa hiyo waroho wa Madaraka waliona hakuna njia nyingine ya kuchukua hatamu za uongozi zaidi ya kutumia mtutu wa bunduki. Miaka baada ya uhuru kulikuwa hakuna chaguzi za ushindani africa, vyama vingi vya siasa vilipigwa marufuku.
Kuhusu mada ni kwamba Nyerere hakuwa mkabila wa waziwazi lakini alikuwa na vimelea vya ukabila. Hakupenda Makabila kama Wachaga ambao wengi waliosomeshwa kupitia KNCU, Wahaya kupitia KCU pamoja na Wanyakyusa (ambao sijui walipata wapi bahati ya kusoma) waje kuchukua uongozi wa juu wa nchi kwa kuwa wangekuwa na solidarity na kupeana madaraka na kuyapuuza makabila mengine kama wakurya ambao elimu yao ilikuwa chini sana baada ya wakoloni kuwaona kuwa wanaweza tu kufungua bunduki na kupiga na wala siyo kufungua kurasa za vitabu.
Zomba. Hata Sheikh Yahya na AMNUT, Sheikh Nurdin Hussein (Mwenyezi Mungu Awarehemu) na wengine wengi wanayajua machungu ya Nyerere. Mada iliyokuwa mezani ni ukabila nami nimechangia kwenye ukabila siyo udini manake ukiongelea masheikh unaongelea udini. Kama ni mada ya udini basi iwekwe tuiongelee.
Sindio aliodhani wataiweza kazi!?Angerudi aone ni kwa kiasi gani alidanganyika/jidanganya!!!Aisee nyie watu hapo juu............Hebu mwacheni mzee wa watu apumzike kwa amani.....Nyerere baba wa taifa langu............. The African Hero.............RIP mzee wangu. Usifufuke manake ukifufuka ukakuta waliyoyafanya hawa watu uliowaachia hii nchi, hakika utakufa tena! Ubazazi, ubaradhuli na wizi mtupu!
Hahahha....mi nilivyosikia ni kwamba hakutaka watuwawe na tv ili wasijue yanayoendelea nje ya sehemu walipo...sasa yeye kwasababu anayo anakuja kuwadanganya ana maono haya na yale kuhusu ulimwengu unapoelekea.Siku ya pili watu wakisikia zile habari kwenye redio au sijui kwenye magazeti basi wanazidi kumwamini maana anajua mambo!!!Ntakitafuta!!!yaani nyerere mawazo yake yalikuwa finyu mpaka na yeye yamem costkutokuwepo kwa tv matokeo yake hotuba zake za tv zipo mbili tu....na zilichukuliwa akiwa sio rais...na ni itv na channel ten tu ndo wanazo....zingine nzuri hazipo kwenye tvkitabu ni historia ya edwin mtei kimezinduliwa hivi karibuniwaulize watu wa chadema watakupa
Nimekusoma na nimekuelewa!Swali...kama alichokua hataki ni walionacho kuongezewa niambie nini haswa kinachoendelea Tanzania karne hii?!Na je leo hii ukiambiwa kwamba haya makabila makubwa yakichukua nchi yatawekana sana madarakani ila maendeleo yatakuwepo (maisha mazuri kwa kila mTanzania kama wanavyosema wanamagamba) utaona bora tutawaliwe na mchanganyiko usio na muelekeo au kundi moja linalojua nini linafanya?!?!Nadhani kuna tofauti kati ya mtu anapokupa sumu akidhani kwamba anakupa dawa na yule anayekupa sumu ili akuuwe.., wa kwanza hata kama anafanya baya anadhani anafanya zuri..., Kuhusu nani anadhani for sure.... history can tell us ndio sababu mpaka sasa watu wengi wanadhani kwamba mmasai ndio mlinzi mzuri au mkurya ndio mwanajeshi mzuri, ni kutokana na culture na historia za makabila. Kuhusu undugunization huo upo mpaka sasa and by then kuna makabila machache ambayo ndio yalikuwa na wasomi na wajuaji so give them power kungekuwa na uwezekano mkubwa wa mwenye nacho kuongezewa na asiyenacho kunyanganywa so maybe he was just putting a level playing field.A good leader ni yule anayefanya what he believes in he just takes action, hakuna kubahatisha..., saying that sio kwamba nasema the guy was an Angel la Hasha., lakini alifanya what he really thought was good kuliko viongozi wa sasa ambao wanatupeleka shimoni huku wakijua.
Afadhali umeanza kwa kucheka kwa kuwa unajua kabisa kuwa hayo ni maneno ya mtaani kama yale ya hadithi ya "Kawawa funika kikombe". Lizzy darling, acha kusikiliza maneno ya vijiweni!Hahahha....mi nilivyosikia ni kwamba hakutaka watuwawe na tv ili wasijue yanayoendelea nje ya sehemu walipo...sasa yeye kwasababu anayo anakuja kuwadanganya ana maono haya na yale kuhusu ulimwengu unapoelekea.Siku ya pili watu wakisikia zile habari kwenye redio au sijui kwenye magazeti basi wanazidi kumwamini maana anajua mambo!!!Ntakitafuta!!!
Habari zenu jamani?!
Naomba nianze kwa kusema ukweli kwamba mimi sikuwepo kipindi cha utawala wa Mwl na hata alipofariki nilikua mdogo sana hivyo sikuwahi kujua kwanini watu wengi walikua wanampenda sana huku bado kukiwa na mambo mengi hasi yanayosemwa juu yake.Nafurahi kwamba mwaka huu nimeweza kutumia muda wangu kiasi nikasoma vitabu kadhaa kumhusu...makusanyo ya hotuba zake pamoja na vitabu alivyoandika mwenyewe.Kutokana na niliyoyasoma niliridhika kwamba sifa zote anastahili...pia kukosolewa maana yeye kama mtu mwingine yeyote yule makosa hatuwezi tuyakwepa.
Katika vitu ambavyo Mwl alivisimamia haswa ni usawa.Hakutaka kabila moja lijione/jisikie liko juu ya jingine na kutengeneza matabaka.Sasa swali langu nnaloomba mnisaidie ni hili....ule msemo au sijui niyaite madai ya kwamba Mwl aliwahi kusema makabila fulani hayafai kupewa uongozi wa juu wa nchi ni wa kweli au ni propaganda za waliomchukia?!Nauliza hivi kwasababu niliyoyasoma juu yake hayaendani kabisa na madai haya...na wala haileti maana kusikia kwamba aliyepigania usawa ndie aliyekua wa kwanza kutengeneza matabaka lilipokuja swala la uongozi!!!
Naomba majibu kama yapo yawe na vielelezo na yasiwe maneno ya kusikika na kufikirika tu ili tusiojua tujifunze kitu.
Asanteni!
Nadhani kuna tofauti kati ya mtu anapokupa sumu akidhani kwamba anakupa dawa na yule anayekupa sumu ili akuuwe.., wa kwanza hata kama anafanya baya anadhani anafanya zuri..., Kuhusu nani anadhani for sure.... history can tell us ndio sababu mpaka sasa watu wengi wanadhani kwamba mmasai ndio mlinzi mzuri au mkurya ndio mwanajeshi mzuri, ni kutokana na culture na historia za makabila. Kuhusu undugunization huo upo mpaka sasa and by then kuna makabila machache ambayo ndio yalikuwa na wasomi na wajuaji so give them power kungekuwa na uwezekano mkubwa wa mwenye nacho kuongezewa na asiyenacho kunyanganywa so maybe he was just putting a level playing field.
A good leader ni yule anayefanya what he believes in he just takes action, hakuna kubahatisha..., saying that sio kwamba nasema the guy was an Angel la Hasha., lakini alifanya what he really thought was good kuliko viongozi wa sasa ambao wanatupeleka shimoni huku wakijua.