Mwalimu Nyerere ametukanwaje hasa?

Maziwa Lala kwelikweli wewe na uanasheria wako wa kwenye JF...yaani matusi kwako ni yale ya nguoni tu...kama baba yako ni marehemu akatokea mpuuzi miaka kadhaa baadaye akasema baba yako alikuwa gaidi wewe hutaona kuwa ni matusi...acha ushabiki wa pesanane...
 
Nyerere alikuwa binadamu tuu,ukweli utabaki palepale kuwa kila binadamu hukosea na kukosolewa.
 

Nakubaliana na wewe ndugu yangu. Ila tatizo ni kuwa hawataki kujifunza hawa. Na kama unavyosikia inavyokuja kwa Muasisi wa siasa za taifa letu, kuna siku itafika kwake( sijui kama atakuwa hai au watngojea awe ameondoka). Wakati huo watasema " alichapa kazi sana, akakamata madini uwanja wa ndege, halafu wakamtenda (siyo kweli) akawa mpinzani wao. Akwaponda jukwaani na akawakumbatia sirini"! Hiyo ndiyo historia yake asipobadilika.

Kumbe inaonekana wabongo wana matatizo ya kuendekeza njaa na unafiki bila kujali wanaandika historia!
 
mkuu big up sana mkuu,nawashangaa sana ccm jk alipokuwa hai hawakutimiza wala kuyaishi yale sahihi aliyosema..walisema yamepitwa na wakati,leo ni marehemu wanajifanya kumtumia kama nukuu za biblia,wanafiki hawa tulione hili...wanatafuta tonge tu

Mbaya zaidi pamoja na uchungu wote wa kinafiki walionao juu ya mwalimu, matendo yao na maneno yao hayaonyeshi kama hata wanamjali kwa lolote!

Kipindi cha uhai wake, usingekuta viongozi wezi bado wako madarakani tena wanainuliwa mikono hadharani wanapigiwa na kampeni na Marais! Ni aibu!...Wala usingesikia mtu anakwiba mabilion benki halafu anaambiwa arudishe tu aende zake!.Eti mafisadi wanajulikana kwa majina, ushahidi upo, kuwashitaki unajiumauma.Mara umewashitaki kesi zinaendeshwa kama hawataki! Zinamaliza miaka! Mara Wananchi wamesahau, wathumiwa haoooo wanapeta uswahilini..Wala usingeona chama cha wakulima na wafanyakazi kimekuwa chama cha wafanyabiashara na majambazi, tena kienyeji!

Lakini naamini hata yeye alijua kuwa mbegu anazopanda, kuna watu watavuna! Imekuwa bahati mbaya wale watu tumekuwa sisi!

Halafu sikia walivyo wanafiki na kudai inawauma sana! Mwalimu katukanwa! Wapi? Matusi gani? Hivi katika akili ya kawaida ni nani anayepata laana? Lissu aliyesema Mwalimu alikuwa na "tabia za tofauti"? au Wao wanaodai kuwa watoto wa Mwalimu halafu wanayofanya na kusema yanamtukana mwalimu?

Siamini kama marehemu wanasikia wala kuona, lakini tuache unafiki na kulichafua jina la Mwalimu kwa kudai utakatifu wakati tunajua wazi uchafu wetu.
 

Ushabiki wa kisiasa ni kitu kibaya sana.....ni baadhi ya mambo yanayorudisha nyuma sana harakati za mageuzi nchini........


Mkuu ni uzushi gani uliouona kwenye maandishi yangu?........ukitaka kujua kuwa baadhi ya maandishi ya Lissu yalikuwa na walakini kuhusu uteuzi wa majaji.....rejea mada husika......

Nilichosisitiza kwenye post yangu huko juu ni kwamba inabidi wana JF tuwe makini wakati wa kusoma maandishi/maneno ya watu mbali mbali....hapo uzushi uko wapi?


Well, all the best na mtizamo wako........
 
Ukweli utabaki kuitwa ukweli na kamwe uongo hautoitwa ukweli,Lisu alyatoa ambayo weng huwa wanayajua ila wanakosa ujasir wakuyasema
 

Nikisema OSAMA gaidi ni tusi au sifa?
Tundu Lissu amemsifu hayati J.K.Nyerere kwamba aliongoza nchi
1.Kibabe
2.Kiujanjaujanja
3.Kidikiteta
4.Uongouongo
Sasa hizo zote ni sifa za Baba wa taifa. Tusi hapo ni lipi mbona ccm munakuwa wanafiki. hata mukisifiwa kwa natendo yenu bado munanuna!!!.
 

Kumbe watu ni wanafiki na kusikiliza propaganda bila kuchambua. hapa mtoa mada kasema tajeni matusi aliyosema Tundu dhidi ya Nyerere wote mnaishia kuanyaanya tu. basi nyinyi mnaomtuhumu ndiyo wenye matusi tena makubwa kwa sababu mnafanya mambo ya ajabu kwa kujificha katika maneno ya Mwl. na mtalaaniwa mpaka mbinguni
 

Lissu n mwanasheria anajua kitendo cha kutoa lugha inayoashiria kumdhalilisha mtu n makosa.
kumwita mtu muongo kisheria n kumdhalilisha.
kumwita mtu dikteta kisheria n makosa( defamesheni).
Kwa vile kauli kaitolea bungeni hakuna chombo chochote kitahoji kasoro bungeni tu.(kinga ya bunge kwa mbunge) .
Nje ya bunge anajua madhara yake hawezi kuyasema hayo.
Hata kama sio nyerere, sio busara kutamka" nyerere ni muongo, alizoea vya kunyonga, alitawala kijanjajanja. laghai nk" hayo sio matusi ni kashfa.
 
tundu lisu hana adabu..kichaa chake hakijapona bado
 

Tunashuhudia wanaCCM wengi humu JF pamoja na Masalia ya CHADEMA majukwaani yakiwa upande wa CCM wakitamka kuwa CHADEMA ni chama cha Kilaghai, Viongozi wa CHADEMA ni madikteta, CHADEMA ni chama cha KIHUNI sasa kama nyie mmeweza kuyasema hayo kama wewe unasema ni kosa vipi kwa upande wenu kuyatamka hayo kwa viongozi wa CHADEMA ni sahihi kwa kuwa ni nyie mmeyasema ila akitamka mwana CHADEMA kwenda upande mwingine ni kosa na tusi?
 
Mwalimu aliwahi kukiri hadharani kuwa haiwezekani kwa mtu kukaa madarakani miaka yote takribani 25 bila kufanya makosa. Na kwamba yeye siyo Mungu hivyo alifanya makosa! Na akafafanua kwamba tatizo ni watu kuacha kuenzi yale mazuri na kung'ang'ania mabaya. Mwenye clip ya hotuba ile tafadhali atuwekee hapa ili hawa wakina Tomaso wajue Nyerere hakuwa Mungu bali alikuwa muungwana anayekiri kuwa kuna mabaya alifanya wakati wa utawala wake.

Naunga mkono hoja ya mleta mada.....orodhesheni matusi aliyotukanwa Mwl Nyerere
 
sidhani kama Lisu katukana ila naona kuna upotoshwaji wa hali ya juu kwani nyerere ni binadamu lazima kuna sehemu amekosea na hatutakiwi kurudia yale yale makosa tunapoelekea kuandaa hatma ya vizazi vya leo,kesho na kijacho.
 

Umenikumbusha jambo; Mwalimu aliwahi kuwaoji wakenya-kwamba kama mtu atapita hapa na kukuambia yule bwana yule unayemuona ndo baba yako. Je, utakubari?
Mleta mada anakiu ya kujua matusi alotoa TL dhidi ya Mwl; wewe unacopy maoni ya Mtei unaweka hapa. Duh! Kaaazi ipo
 

cjui niseme ni upuuzi au nini,vitabu vya dini vinasema hakuna binadamu aliekamilika na ndo maana kuna kutubu,nimeshangaa hata yule babu anaejiita askofu halijui hilo mpaka kusema eti nyerere hakuna wa kumkosoa,eti anatarajiwa kutangazwa mtakatifu na kanisa katoliki,kama kuna mtu ana mawasiliano na yule babu hebu amwambie asome vizuri historia ya watakatifu aone walikuwa na maisha gani kabla ya kuja kubadilika na kutubu dhambi zao,wengine walikuwa wauaji,wanyang'nyi nk lakn leo hii ni watakatifu,kwa hili babu hastahili kuitwa askofu kama hata maandiko anayapotosha.
kwa mwenye akili ya kufikiri atajua pale swala sio kumtukana nyerere wala kumkosoa hapa ni agenda ya kutafuta pa kushika kwa sababu hata mfa maji haishiwi kutapatapa,kila mjumbe anaesimama analifanya hilo kama ndo kipengele cha kujadili bungeni kwa sababu binafsi nadhani wajumbe wameambiwa bila kuliweka hilo hatuna jambo jingine la kutumia kuwalaghai wananchi,na atakaekiuka hana ulaji ndo maana wanaangaika sana ili waonekane waendelee kupata fadhila.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…