Mwalimu Nyerere ametukanwaje hasa?

Mwalimu Nyerere ametukanwaje hasa?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Kuna uvumi (binafsi naziita propaganda) kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum na Wakili Msomi mwenzangu Tundu A.M.Lissu 'amemtukana' Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 'Matusi' husika yanadaiwa kuporomoshwa na Tundu Lissu alipokuwa akiwasilisha Maoni ya Wachache katika Kamati Nambari Nne ya Bunge.

Inasemwa kuwa Tundu Lissu amemtukana na kumdhalilisha Baba wa Taifa. Propaganda hizi zinazosambaa haraka na kwa kishindo zimemkumba hadi Mzee Edwin Mtei ambaye ni Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA. Nikumbukacho ni kuwa Lissu alipokuwa akitetea na kufafanua Maoni ya Wachache,alitoa mifano minne akiwataja watu mbalimbali wakiwemo Mwalimu Nyerere,Profesa Issa Ghulamhussein Shivji na Dr.Harrison Mwakyembe.

Kwanza,tufahamishane hasa matusi yaliyoporomoshwa na Wakili Lissu dhidi ya Mwalimu Nyerere. Tukiyajua na kutambua kuwa ni matusi na dharau kweli,tuungane kumkemea Wakili Lissu na kumuonya asirudie tena. Karibuni tutaje matusi au dharau za Wakili Tundu Lissu kwa Mwalimu Nyerere. Halafu,kwanini wengine waliotajwa hawaonekani kama wametukanwa au kudhalilishwa?
 
Last edited by a moderator:
Mi nasema mtu yeyote akikosea atakosolewa na akifanya vizuri atasifiwa na kwa mujibu wa imani yangu ni Mungu tu hakosolewi kwa sababu yeye ni PERFECT. Kutotaka Nyerere akosolewe ni kujidai eti alikuwa PERFECT katika maamuzi yote aliyofanya. Hii si Kweli lazima tubadilike tumweke binadamu yoyote kwenye mizani bila kujali umaarufu wala hekima ya kibinadamu aliyo nayo. tukijidai eti kumkosoa nyerere ni Dhambi inayostahili adhabu kubwa tutakuwa tumefisha uhuru wa fikra na hivyo kujifungia kwenye blanket la umbumbumbu wa hali ya juu. Nyerere was not God na hatakaa awe Mungu kwani kuna aliyofanya mazuri na kuna aliyokosea kama binadamu. Tumemsifia miaka yote kwa mazuri aliyofanya na kama alikosea basi anastahili kukosolewa. inakuwaje kukosoa mawazo na matendo ya nyerere eti ni MATUSI ;huu ni unafiki mkubwa wa kuzima mawazo chipukizi yenye mtazamo wa mawazo huru
 
Siko tayari kutukana, ila jua kua maneno aliyoyasema hakustahili kuyasema dhidi ya Nyerere.
 
Siko tayari kutukana, ila jua kua maneno aliyoyasema hakustahili kuyasema dhidi ya Nyerere.

Namkubali sana Nyerere, lakini hiyo haitamaanisha kuwa pale alipokosea iwe dhambi kumkosoa! Naungana na mtoa mada: kama tumeshindwa kutaja makosa ya Tundu Lissu, kama tumeshindwa kuyataja matusi aliyo tukana, basi tukae kimya. Nilichokiona mimi ni mtu kukosolewa alipokosea na mkosoaji alikuwa sahihi!

Anayetaka kueleweka aje na hoja yenye ushahidi kwamba aliyosema Lissu siyo kweli na hayakusemwa na Mwalimu, hayakufanywa na mwalimu na hayakuandikwa na mwalimu!

Napenda kusisitiza, ni katika jamii ya wendawazimu na wasanii wa kisiasa tu, ambapo watu watajidai kupenda kujali na kumtetea marehemu, huku tukishindwa kuwaheshimu wazee wetu walio hai kama kina Mzee Warioba, kina Mzee Aboud Jumbe na wengineo. Halafu tusubiri mpaka nao wafe ili tujidai tunawaheshimu. Tuache unafiki!
 
Hili muenendo wa hii semina huko Dodoma ni mwendo wa kutafuta nani kasema nini ili kuendelea kupoteza muda kwa kuwa kuna kipengele cha kuomba kuongezwa muda ili kuendelea kutafuna kodi zetu...
 
Maneno ni upanga wenye ncha mbili zinayokata pande zote. Maneno yako yanaweza kukufanya uwe na hatia na vile vile yanaweza kukuondoa kwenye tuhuma za hatia. Yote inategemea na jinsi unavyotumia maneno yako.

Sidhani kama Lisu alitumia maneno yake vizuri, na ndiyo maana nimekuwa na wasiwasi na uhakika wa maneno yote aliyowahi kutuambia kuhusu Zitto na Kitila huko nyuma.
 
Mimi ninafikiri waliomtukana Nyerere tusi kubwa ni wale walioua AZIMIO lake la ARUSHA na kuweka AZIMIO la Zanzibar badala yake. Hawa mahayawani wanatetea maslahi yao na familia zao. Walijua Azimio la Arusha lilikuwa linawabana kwa hivyo hawakuona haja ya kuwepo mjadala wa kitaifa kuhusu hilo. Lakini kwa vile wanajua Muungano wa serikali mbili ni lulu kwao kuendeleza usultani mamboleo basi ndo unaona wanahahaha kila kuchapo kutafuta vihoja mshenzi kulinda status quo. Washenzi sana hawa.
 
Wassira mwenyewe alikimbia ccm wakati wa nyerere alipokufa ndipo akarudi ccm.Tangulini Julius akachinja?amezoea vya kunyonga
 
Maneno ni upanga wenye ncha mbili zinayokata pande zote. Maneno yako yanaweza kukufanya uwe na hatia na vile vile yanaweza kukuondoa kwenye tuhuma za hatia. Yote inategemea na jinsi unavyotumia maneno yako.

Sidhani kama Lisu alitumia maneno yake vizuri, na ndiyo maana nimekuwa na wasiwasi na uhakika wa maneno yote aliyowahi kutuambia kuhusu Zitto na Kitila huko nyuma.
Hili ndilo tusi alilotukana? Na Mnafiq Mwanadiwani ndicho alichokiposti?
 
Mleta mada anataka muyataje hayo maneno nyie mnakuja na ngonjera zile zile, NAOMBA UTUAMBIE LISSU AMETUKANA VIPI AU MANENO GANI MABAYA ALIYOYATAMKA JUU YA NYERERE. kwa hiki ulichokiandika bado haujajibu swali la mleta mada
 
Hili ndilo tusi alilotukana? Na Mnafiq Mwanadiwani ndicho alichokiposti?
Na wewe una matatizo ya kujua maana na matumizi ya meneno; umetafuta majina badala ya maneno. Nitakusaidia kwa kuanza hivi: " Maneno ni upanga wenye ncha mbili zinazokata pande zote. Maneno yako yanaweza kukufanya uwe na hatia na vile vile yanaweza kukuondoa kwenye tuhuma za hatia. Yote inategemea na jinsi unavyotumia maneno yako."

Halafu nitakurahishia hivi:

MANENO yote yaliyowahi kutoka mdomoni mwa Lissu yanatakiwa yaangaliwa kwa makini, mfano yakiwa yale maneno yake dhidi ya Zitto na Kitila.
 
Kuna uvumi (binafsi naziita propaganda) kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum na Wakili Msomi mwenzangu Tundu A.M.Lissu 'amemtukana' Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 'Matusi' husika yanadaiwa kuporomoshwa na Tundu Lissu alipokuwa akiwasilisha Maoni ya Wachache katika Kamati Nambari Nne ya Bunge.

Inasemwa kuwa Tundu Lissu amemtukana na kumdhalilisha Baba wa Taifa. Propaganda hizi zinazosambaa haraka na kwa kishindo zimemkumba hadi Mzee Edwin Mtei ambaye ni Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA. Nikumbukacho ni kuwa Lissu alipokuwa akitetea na kufafanua Maoni ya Wachache,alitoa mifano minne akiwataja watu mbalimbali wakiwemo Mwalimu Nyerere,Profesa Issa Ghulamhussein Shivji na Dr.Harrison Mwakyembe.

Kwanza,tufahamishane hasa matusi yaliyoporomoshwa na Wakili Lissu dhidi ya Mwalimu Nyerere. Tukiyajua na kutambua kuwa ni matusi na dharau kweli,tuungane kumkemea Wakili Lissu na kumuonya asirudie tena. Karibuni tutaje matusi au dharau za Wakili Tundu Lissu kwa Mwalimu Nyerere. Halafu,kwanini wengine waliotajwa hawaonekani kama wametukanwa au kudhalilishwa?

Kwa akili zenu, na u CDM wenu bado mnaona kabisa Lissu alikuwa sahihi kutumia lugha zile na kumwita Mwalimu Nyerere mwongo! Kwa hiyo unataka kuwaambia watanzania kuwa mwasisi wenu wa CDM ni bongo lala kwa kuwa Lissu hakutoa tusi lolote? Kweli CDM sasa siasa zimewashinda!
 
Mleta mada anataka muyataje hayo maneno nyie mnakuja na ngonjera zile zile, NAOMBA UTUAMBIE LISSU AMETUKANA VIPI AU MANENO GANI MABAYA ALIYOYATAMKA JUU YA NYERERE. kwa hiki ulichokiandika bado haujajibu swali la mleta mada

Nitakujibu nikishakuwa na uhakika kuwa unajua maana ya "kutukana". Iwapo hujui maana ya matusi basi hakuna utakaloona tusi na itarudi tena kwenye "maneno na matumizi yake"'
 
Yani maneno ya Tusi yanaonekana kama ndiyo tusi lenyewe.....Hakuna matusi yoyote ambayo Lissu alimtukana baba wa taifa, kama yapo yawekwe bayana, yanini kuendelea kuzunguka mbuyu?
 
Nitakujibu nikishakuwa na uhakika kuwa unajua maana ya "kutukana". Iwapo hujui maana ya matusi basi hakuna utakaloona tusi na itarudi tena kwenye "maneno na matumizi yake"'
Mkuu, nukuu hayo matusi aliyotukanwa Nyerere. weka bra bra pembeni.
 
Back
Top Bottom