DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mwanafunzi wa darasa la saba (13) shule ya Msingi Ngarenaro Jijini Arusha amefungwa na mnyororo na kufungwa kwenye dawati Darasani na Mwalimu mkuu wa shule hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa kuwa ni mtoro.
Wakizungumza wazazi wameleza kuwa walipigiwa simu na mlinzi wa shule aliyekuwa zamu mchana kwamba mtoto wao amefungiwa darasani na Mwalimu mkuu hivyo waende wakamsaidie kwasababu anakohoa sana na hana msaada
Baada ya Time TV kufika shuleni hapo ilishuhudia mwanafunzi huyo akiwa kwenye dawati na raia waliokuwepo walitamani kumsaidia lakini mlinzi aliyekuwa zamu usiku huo alikuwa amefunga geti kwa kile alichoeleza kuwa kufanya hivyo ni magizo ya boss wake ambaye ni mkuu wa shule hiyo.
Baada ya tukio hilo taarifa zilitolewa na alifika mkuu wa kituo cha polisi ngarenaro na baadhi wa walinzi wakaruka geti kwa na Kwenda kuingia darasani na kuvunja mnyororo huo ili kumsaidia mwanafunzi huyo.
Hata hivyo mlinzi wa shule hiyo amekiri kuwa shuleni hapo wanafunzi huwa wanafungwa nyororo na Mwalimu mkuu kama ni watoro na kulala darasani mpaka asubuhi huku wamavaliwa nyororo ikiwa imefungwa na kufuli ambapo kazi yao ni kulinda kutokana na maelekezo ya Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bwana Mussa