The Desert Fox Jenerali Ulimwengu akiwa na Ghadafi mnamo mwaka 1983 Mjini Benghazi nchini Libya
Ndugu wana jf naomba kuuliza ....
Kumbukumbu za kihistoria zinabainisha kuwa hata mara moja Mwalimu Nyerere hakuwahi kuwa rafiki wa Ghadafi , na baadhi ya matukio yafuatayo yanadhihirisha uhasama huo...
1.Mnamo mwaka 1978 Ghadafi alimsadia Idd Amin dhidi ya Tanzania kwenye vita vya kagera
2.Baada ya vita mwaka 1979 Ghadafi alitaka abadilishane mafuta kwa mateka wa kilibya waliokuwa chini ya majeshi ya Tanzania, Nyerere akamjibu kuwa damu ya watanzania kamwe haiwezi kuwa sawa na thamani ya mafuta.
3.Baada ya azma yake ya kuiunganisha Afrika kukwama aliamua kuitisha mkutano wa machief wa kiafrika lakini hakumwalika hata chief mmoja kutoka Tanzania (kama wapo)
SASA MASWALI YANGU NI KAMA IFUATAVYO;
1.Ni lini Ghadafi alianza kuwa rafiki wa Tanzania?
2.Ni kipi Ghadafi aliifanyia Tanzania? kiasi kwamba Mh BERNAND MEMBE kapata ujasiri wa kuitangazia DUNIA yale aliyokaririwa akisema kuhusiana na Ghadafi.
3.Mwishowe nataka kufahamu Nyerere angekuwa hai, je angezungumza nini kuhusu kifo cha Ghadafi?
NAWASILISHA WADAU!