Mwalimu J.K.Nyerere; Ghadafi Koma Damu Ya Watu Wangu Si Sawa Na Thamani Ya Mafuta Yako..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu J.K.Nyerere; Ghadafi Koma Damu Ya Watu Wangu Si Sawa Na Thamani Ya Mafuta Yako..!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAMBOTA, Oct 25, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  The Desert Fox Jenerali Ulimwengu akiwa na Ghadafi mnamo mwaka 1983 Mjini Benghazi nchini Libya

  Ndugu wana jf naomba kuuliza ....
  Kumbukumbu za kihistoria zinabainisha kuwa hata mara moja Mwalimu Nyerere hakuwahi kuwa rafiki wa Ghadafi , na baadhi ya matukio yafuatayo yanadhihirisha uhasama huo...
  1.Mnamo mwaka 1978 Ghadafi alimsadia Idd Amin dhidi ya Tanzania kwenye vita vya kagera
  2.Baada ya vita mwaka 1979 Ghadafi alitaka abadilishane mafuta kwa mateka wa kilibya waliokuwa chini ya majeshi ya Tanzania, Nyerere akamjibu kuwa damu ya watanzania kamwe haiwezi kuwa sawa na thamani ya mafuta.
  3.Baada ya azma yake ya kuiunganisha Afrika kukwama aliamua kuitisha mkutano wa machief wa kiafrika lakini hakumwalika hata chief mmoja kutoka Tanzania (kama wapo)

  SASA MASWALI YANGU NI KAMA IFUATAVYO;
  1.Ni lini Ghadafi alianza kuwa rafiki wa Tanzania?
  2.Ni kipi Ghadafi aliifanyia Tanzania? kiasi kwamba Mh BERNAND MEMBE kapata ujasiri wa kuitangazia DUNIA yale aliyokaririwa akisema kuhusiana na Ghadafi.
  3.Mwishowe nataka kufahamu Nyerere angekuwa hai, je angezungumza nini kuhusu kifo cha Ghadafi?

  NAWASILISHA WADAU!
   
 2. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #2
  Oct 25, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Huu uchambuzi wako ni mzuri. naamini Jenerali Ulimwengu atakuwa na majibu sahihi sana...
   
 3. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Aliishi kwa upanga na ameenda kwa upanga. Thats all...
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 4,000
  Trophy Points: 280
  jibu rahisi kwa kupitia Bakwata kujenga misikiti, kutoa bajeti yao na kuleta tenda na halua! hapa ukiuliza hayo utaambiwa unachuki za kidini! Ningependa wachambuzi kama wakina wakina Mohammed Said waongelee na hili pia!
   
 5. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,612
  Trophy Points: 280
  BENARD MEMBE NI BAKWATA AU MUISLAM?.mia
   
 6. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2011
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  kulitokea kaurafiki kati ya kikwete na gadafi baada ya jk kumpa gadafi umwenyekiti wa eu, sasa na kauislam jk anasympasize na marehemu sasa membe macho yake yanatazama 2015 anadhani mzee anaweza kumfikilia sasa anamfanyia kazi hiyo
   
 7. K

  KAMALELA JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 213
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  JK kampatia Ghadafi ile hotel ya BAHARI BEACH ya kifahari iliyojengwa na Mwalimu nyerere, na imefanyiwa ukarabati mkubwa sana na imependeza, Ilikuwa ifunguliwe april 2010 lakini kutokana na matatizo ya mfumo wa maji safi ikabidi wasimamishe ili watengeneze visima vya maji. uhusiano umeimarika sana wakati huu hasa baada ya ghadafi kuahidi kujenga miskiti 10 katika kila mkoa wa Tanzania...
   
 8. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Acheni Udini, Hata Watanzania Tulipigana na Uingereza Ktk Vita Kuu ya kwanza ya Dunia lakini mpaka leo ni marafiki. Je Ubalozi Wa Libya ulifunguliwa Jk alipoingia madarakani?
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  JK amekuwa madarakani muda mrefu sana mkuu wangu ila Urais kaanza juzi tu hapa baada ya nyie kumpa kula badala ya kura .Now kujibu swali lako nasema Yes alikuwa madarakani kaka .
   
 10. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,699
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  @ kambota,naombwa kujuzwa sababu ya Gadhaf kushindwa kuiunganisha Afrika ni nini?
   
 11. M

  Madaraka Amani Member

  #11
  Oct 26, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Swali kuwa ni lini mwalimu alikuwa rafiki wa Gadafi na angekuwa hai angesema nini kuhusu kifo cha Gadafi ni dalili kuwa mwandishi amekosa hoja na ni mvivu wa kufikiri. Ni mtazamo kuwa kila alilopenda Mwl. Nyerere ndilo sahihi na kila alilolichukia sio sahihi. Ni mtazamo kuwa hakuna anayeweza kuwa na maoni sahihi ila Nyerere. Mwl Nyerere alikuwa mwanadamu wa damu nyama na mifupa.

  Hakuwa malaika wala hakuwa mtume wa mwenyezi mungu. Yapo mazuri aliyoyafanya tunapongeza na kuyaenzi na yapo mabaya aliyofanya tunyamaza na kuyaepuka bila kuathiri heshima ya Mwalimu. Kutokana na hali ya Mwl Nyerere kuwa mwanadamu wa kawaida hawezi kuwa kipimo kwamba kila aliyemchukia yeye au kila aliyekuwa hana mahusiano na yeye basi ni mtu mbaya.

  Waheshimiwa tunaheshimu sana maoni yenu lakini msitulazishe kuamini mambo mengine kama tunavyoiamini Biblia. Zama za zidumu fkra za Mwentekiti (Mtu mmoja) zimepita sasa kila mwananchi afikiri na fikra zake ziangaliwe. Kama Gadafi alifanya mabaya yasemwe na kama Gadafi alifanya mazuri nayo yapongezwe.
   
 12. M

  MLEKWA Senior Member

  #12
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  membe.JPG


  Mimi kwanza si mfuasi wa Membe wala wa CCM ila kauli ya Membe imenipa hope ya ujasiri wake nakumuona Membe kama Kiongozi shupavu kama ule wakati wa Nyerere kwani alisema Tanzania ni nchi sisi hatushawishiwi kumtambua mtu yoyote kuitambua nchi kwa shinikizo la mtu au Taifa fulani tuna uhuru wetu hapa nilimuona Memmbe ni matured leader na inabidi watanzania tuanze kuomba kuwe na wagombea binafsi kuondoa hiii dhana ya kutawaliwa na vyama kwnai si kila linalosemwa na CCM ni baya wala CUF CCM au Chadema sio malaika as well Utaifa iwe ndio Mwanzo vyama baadae si hivyo tutajikuta tunatawaliwa na Dikteta na sisi kwenye mfumo wa vyama vingi.

  Pia kama nijaribu kujibu suali kama Nyerere angekua hai leo angesema ubeberu unarudi Afrika, nina uhakika hakuna Kiongozi yoyote au mwananchi mwenye akili zake timamu kuona nchi yako inapigwa mizinga kuvunjwa vunjwa kwa kisingizio cha kuwa watu fulani wawpo madarakani kwa kulinda maslahi yako.

  Gadafi amefanya makosa mengi kama Kiongozi kama Nyerere alivyofanya makosa ya kuwachukua watu kuwapeleka maporini na kuliwa na simba kwa kisingizio cha Nguvu KAZI. Kuna wazungu waliokuja Tanzania kuja kuona idea zake amabazo hakuna Muafrika aliokua na idea kama zake ila zote zilifeli na kuua uchumi wa nchi kabisa kwa kujaribu mambo bila ya kufanya reseach za kutosha.

  Nirudi kama Gadafi hakujaribu kuingilia maslahi ya nchi za mgharibi hivi karibuni barani Afrika kuzuia America na nchi za ulaya kujenga base za kijeshi kwa kuzioffer nchi masikini pesa kama zitakubali kambi za kijeshi matoekeo yake nchi hizi zilikua zinapewa misaada ya siri na Libya isikubali kujenga vituo vya kijeshi Afrika, kwani Gadafi aliona kua Wazungu mwisho wake wangeitawala Bara la Afrika kwa kutumia Kambi hizi za Kijeshi.

  Ujinga wa Gadafi ni tofauti na Nyerere kwani Neyerere alipoona mageuzi duniani yanaaza kuja aliamua kuondoka kwa hiari yake , kwa upande wa Gadafi akili zake zilikwisha anza kupotea na kuwaweka wanawe ndio washauri wakuu na kuwafanya wanawe kutoa amri zinazopingana hata na Waziri Mkuu au waziri yoyote akitoa amri ambayo haikupendeza kwa wanawe ilipingwa au wanawe kuingia mikataba ya Kimataifa bila ya seriakli kujiua umakini wake na kusikia kweney vyombo vya habari tu.

  Makosa ya Gadafi hayana tofauti sana na CCM leo Ingawa Gadafi hakuruhusu vyama ila mwishoni hakua na njia za kuweka sheria za kuwua control watu wake ndani ya serikali na matokeo yake waliweza kushirikiana kwa kulipiziana visasi na yeye gadafi na wanawe na mashemegi zake , tumeona namna Balozi za Libya dunaini moja moja zilianza kugawika zipi zinamuunga mkono Gadafi na zipi zinawaunga mkono mawaziri wake walioijiunga na Upinzani . Mgawanyiko huu ndio uliwapa wazungu mwanya ya kuifanya walivyotaka kuifanya Libya.

  Washa washa Gadafi jibu lako ni kuwa unapokua na watoto ndan iay nyumba yako watakusikiliza ukiwaambie usivute sigara ila na wewe ukiwa unaendelea kuvuta kisiri na wewe hutakua na uwezo wa kwuakataza , Gadafi kama angekaa na kuibadilisha katiba ya Libya na Kumshauri Seif Islam kuunda chama chake basi Libya ingekuwa more stable , democratic na kuheshimika duniani lakini Libya ilitaka kuwapa usahuri Waafria wakati yeye mwenyewe kwake hakuja kaasawa licha ya mapesa aliokua nayo ingawa alikua na nia mzuri hakua na mipango mizuri ya kujenga Dola yake ndio faliure yake iliomuacha kumaliza utawala wake Vibaya.
   
 13. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160

  Madaraka you said well broda, no need to add anything!!!
   
 14. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Gaddafi kwa Tnzania alikuwa rafiki mnafiki
   
 15. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Tanzania ni nchi ya ajabu sana.

  - Tulilia alipouwawa Osama, pamoja na kwamba Osama aliishambulia nchi yetu hata kabla ya kuishambulia Marekani.

  - Warwanda walipomuua Habyerimana, tukatangaza msiba wa wiki nzima, pamoja na kwamba walipokufa waTZ 2,000 kwenye Spice Islander hatukujali na badala tulifanya Miss Tanzania.

  - Wananchi wetu wanateswa Arabuni kwa ajira dhalimu, lakini balozi zetu zinawapotezea mpaka wanaokolewa na vi-NGO vya Ulaya.

  - Sasa hivi tunamlilia Ghadaffi pamoja na kwamba alishirikiana na lile joka kuu Idi Amin kuua watu wetu 1978!  BTW: Nimeipenda hiyo picha ya Jenerali akiwa ndani ya pango la huyo nyoka wa kijani.

   
 16. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vijana wa miaka ya 1978 and 1979 wanajua sana ubaya wa Gadafi na hasa wale wa mpakana Kagera
   
 17. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kama si ghadafi ile vita na idd amini ingechukua muda mfupi na kuokoa uchumi wa nchi.
  ghadafi alituumiza watanzania wote alitakiwa kama alitaka kujisafisha alete misaada inayogusa nyanja za kiuchumi si kujenga misikiti.
  na kama alikuwa mwema asingedhalilishwa hivyo,mungu ili kumwadhibu alimnyima hata akili ya kukimbia mpaka akaingiziwa miti makalioni.

  ole wao walio na akili za kighadafighadafi siku zao hazitakuwa tofauti na masaa ya mateso ya ghadafi.
   
 18. Blessingme

  Blessingme JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 250
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Well said! Cc tanzania huwa hatukumbuki wabaya wetu na kilichotendeka miaka ya nyuma, nakumbuka wakati wa kifo cha baba wa taifa 2likataa kabisa idd amin asije kweny msiba, sa mi najiuliza huyu ghadaf ambaye alikuwa suppoter wa idd amin amekuwa na wema gani kwetu had membe akulilie? Nimepoteza matumain kabisa na hii serikali! Shame on u membe!
   
 19. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Inaelekea hukusoma history secondary school au ulisoma mpaka form two kama mimi...... However, kwa kukukosoa tu, Tanzania hatujawahi kupigana vita na Mwingereza. Vita vilikuwa kati ya Mingereza na Mjerumani.
   
 20. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Tatito la Wabongo, tunaangalia swala la Gaddafi kwa kulinganisha na umaskini wetu!! Ndiyo sababu kuna watu wanashangaa kwa nini Walibya wamemkataa Gaddafi wakati alikuwa anawapa umeme bure na mikopo isiyo na riba. Kwa matatizo yetu ya umeme na maisha ya kubahatisha watu wanaona kuwa Walibya walitakiwa wamuenzi Gaddafi kumbe wanasahau kuwa Walibya walimchukia Gaddafi kwa ajili ya kuwanyima uhuru wao na kuifanya mali yao kama ni yake binafsi!!
   
Loading...