Powel Mizengo
Senior Member
- Jan 20, 2014
- 126
- 24
Nina rafiki yangu ana mpenzi wake ambaye amekwisha mtolea mahali tayari kwa ajili ya kumuoa!!Huyo mwanamke yeye ni mwalimu huko Morogoro na jamaa anafanya kazi Dar es Salaam,hivyo huwa na mawasilino ya simu na mara kadhaa hutembeleana!!.Mara nyingi mwanamke amekuwa akihitaji fedha nyingi za matumizi toka kwa mwanaume ilihali nayeye anafanya kazi!!!!Lakini jamaa hua anamtumia!!!Huyu mwanamke amekuwa akihitaji kitu,anataka apate kwa wakati bila kujali kama jamaa anayo au hana!!!Kuna siku jamaa alienda kumtembelea mpenzi wake ila hakumwambia kama anakwenda!!!Alipofika hakumkuta;akampigia simu kumuuliza kuwa yupo wapi;yeye akamjibu yupo nyumbani;Jamaa akamwambia mbona nimemtuma mtu kwako na haupo!!!Ndipo jamaa akaamua kuingia chumbani na kulala mpaka asubuhi kwani funguo za chumba nayeye alikuwa nazo!!!Asubuhi jamaa akarudi zake Dar!!!Siku nyingine jamaa akaenda tena;wakati wakiwa wote chumbani,mwanamke alienda bafuni,huku sms zikawa zinaingia kwenye simu ya mwanamke!!Kwakuwa jamaa alishakuwa na mashaka na mpnz wake, ndipo alipoamua kusoma sms zote zilizokuwa zikiingia;Jamaa aliamua kuzifoward kwake;wakati mwanamke anatoka bafuni alimkuta jamaa anaendelea kusoma sms;ndipo mwanamke akaanza kumfokea jamaa yake akidai kwa nini anashika simu yake!!Hakika ulitokea ugomvi mpaka mwanamke kufikia kummwagia maji ya moto ambayo yalikuwa yakichemka jikoni kwa ajili ya maandalizi ya msosi!!Alipommwagia,akakimbia kusikojulikana!!!Jamaa wa watu alijipatia huduma ya kwanza na kulala!!ilipofika asubuhi akarudi zake Dar!!!!Sasa huyu jamaa amekuja kwangu kuniomva ushauri;Je,amtafute mpnz wake ili warudiane au aachane naye?Anajua wazi mapenzi hayashauriki lakini bado yupo njia panda kwa aliyofanyiwa ijapokuwa dhamira yake bado inamhitaji yule mwanamke!!!Naomba msaada wenu wanajamvi tuweze kumwokoa mwenzetu kwani mpaka sasa jamaa amedhohofika sana kwa mawazo!!!!