Mwalimu amkung’uta makonde Mwalimu Mkuu

Mwalimu amkung’uta makonde Mwalimu Mkuu

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,699
Reaction score
2,261
Maabara.jpg

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitarungu Wilayani Serengeti, Thomas Marwa ametwangwa makonde na mwalimu mwenzake akiwa ofisini kwake.

Tukio hilo lilisababisha masomo na shughuli zingine kusimama shuleni hapo kwa muda ili kuweza kuupatia suluhu ugomvi huo.

Akizungumza kuhusu ugomvi huo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Thomas Marwa amesema kuwa, ameshambuliwa na mwalimu mwenzake Yaredi Amos kwa tuhuma kuwa anamfuatilia fuatilia kuhusu uwajibikaji wake katika majukumu yake.

“Nikiwa ofisini naendelea na majukumu yangu, ghafla mwalimu Amos aliingia Ofisini kwangu na kuanza kunishambulia kwa ngumi usoni, akihoji barua niliyomuandikia kuhusu uwajibikaji wake kazini,”amesema Marwa

Hata hivyo, kwa upande wake Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Serengeti, Juma Hamsini amesema kuwa amepokea taarifa tukio hilo na kuagiza hatua za kisheria na kinidhamu zichuliwe dhidi ya mwalimu huyo.

Chanzo: Dar24
 
Kwa jinsi Viongozi wanavyopenda Sifa awamu hii usipokuwa na stamala lazima urushe Ngumi tu!
 
Kuna walimu wakuu wanazingua kinyama, so hii kitu mi sitomlaumu ticha aliye amua kuwa 'Francis Cheka'
 
Sitak kuuliza wala kujua, naamin mwl mkuu ndo kiherehere, with refference kwa walimu wakuu weng hasa wakizaman pamoja na kiki za viongoz weng wa awam hii
 
walimu wakuu na waratibu ni vibaraka wa wakoloni weusi.... nami nilishamkwida mmoja za uso. bahati nzuri na magu alimpitia kwa cheti cha "steshenare".
 
Back
Top Bottom