Changalucha
JF-Expert Member
- Oct 19, 2011
- 508
- 595
Apumzike kwa amani Mwalimu kijana. Hoja yangu ni kuhusu aina ya uandishi kutoka chanzo cha uzi huu (Nipashe) hasa kuhusiana na chanzo cha kifo " kunyweshwa sumu" na dawa anayotaja mwandishi kuwa mhanga alinyweshwa kuwa ni " Asphxia Due Mothorax".Mwalimu Nocka Mwaisango (28) wa Shule ya Sekondari Kibwe, jijini Dodoma, amefariki dunia baada ya kunyweshwa sumu na watu wasiofahamika.
Alikufa wakati akitokea mkoani Dodoma kwenda kijijini kwao mtaa wa Mtakuja, Mbalizi Wilaya ya Mbeya Vijijini kwa lengo la kumuoa mchumba wake wa muda mrefu.
Baba mzazi wa mwalimu huyo, Oddy Mwaisango, alisema alipigiwa simu Desemba 20, mwaka jana na mtoto wake huyo kuwa anatarajia kwenda Mbeya kwa mapumziko ya sikukuu na kwamba atatumia mapumziko hayo kumuoa mchumba wake wa muda mrefu.
Alisema baada ya kupigwa simu hiyo, alishangaa kuona muda mrefu unapita bila kumuona na wiki moja baadaye alipigiwa simu na watu wasiofahamika waliotumia namba ya simu ya mtoto wake wakisema kuwa wanamshikilia kwa kazi maalum.
Alisema baada ya kauli hiyo aliamua kwenda Kituo cha Polisi Mbalizi, kuripoti tukio hilo.
Alisema siku iliyofuata mama yake alienda Dodoma katika shule aliyokuwa akifundisha kukutana na Mwalimu Mkuu ambaye alimjibu kuwa mtoto wake hakumuaga alipoondoka.
Alisema, ilibidi aende kuripoti Polisi Dodoma na Kitengo cha Uchunguzi wa Mawasiliano mkoani humo kiligundua kuwa mwalimu huyo yuko mkoani Morogoro.
“Ilibidi mama yake asafiri hadi Morogoro na aliripoti kituo cha polisi na kukabidhiwa mtu wa uchunguzi wa mitandao ndipo katika kuchunguza wakabaini wahalifu hao na mwalimu huyo wako mkoani humo, lakini ghafla wakawa hawaonekani kwenye mtandao,” alisimulia.
Alisema baadaye wahalifu hao walimpigia simu (baba) wakihitaji Sh. 5,000,000 kama kikombozi, lakini kwa sababu hakuwa na fedha aliwatumia Sh. 500,000 ili wamwachie.
Aliongeza kuwa siku iliyofuata mtoto wake aliwapigia simu mwenyewe na kuwaambia kuwa yuko kituo cha daladala cha Tazara Mbeya na walipoenda kumfuata walikuta hajitambui.
Aidha, alisema waliamua kumkimbiza hospitali ya Ifisi iliyoko Wilaya ya Mbalizi na baadaye walimhamishia Hospitali ya Rufani Mbeya.
Alisema akiwa wodini aliongezewa maji ya kutosha, lakini alikuwa analalamika kuumizwa kwenye koo na kifuani na katika uchunguzi wa madaktari ilibainika amenyweshwa sumu.
Alisema siku iliyofuata mwalimu huyo alifariki akiwa hajawataja waliomfanyia unyama huo huku chanzo cha kifo kikitajwa kuwa ni dawa aina ya ‘Asphxia Due Mothorax’ aliyonyweshwa.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibwe, Dodoma, Mwasiti Msokola, alikiri kupata taarifa za kifo cha mwalimu wake na kwamba suala hilo linashughulikiwa na mkurugenzi ambaye ndiye mwajiri wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Chanzo:Nipashe
Nashawishika kuwa huenda mwandishi wa taarifa hii hakufanya ufuatiliaji na utafiti wa kutosha na hata pengine hakuwaona madaktari ili watoe ufafanuzi wa chanzo cha kifo hicho bali amesoma cheti cha kifo tu.Cha kusikitisha hata mhariri wake naye hakuwa makini.
"Asphxia" (mara nyingine huandikwa Asphyxia)ni hali ya kupungua au kuishiwa kiasi kikubwa cha hewa ya oksjeni mwilini inayoambatana na ongezeko la hewa ya kaboni monoksaidi na kusababisha mtu anayepata hali hiyo kuzirai ama kifo. Hali hii husababishwa na kupaliwa/kukabwa koo, kuzama majini, shock ya umeme ama kuvuta hewa yenye sumu au kujeruhiwa (injury). "Pneumothorax" ni hali inayotokea wakati hewa ama gesi nyingine (air or other gas) inapovujia kwenye nafasi kati ya mapafu na kuta za kifua na huweza kusababishwa na maradhi, ama majeraha kwenye tishu za mapafu, ama mipasuko kwenye kuta za kifua.
Chanzo cha kifo kinaweza kuwa ni Asphixia (Kuishiwa oksjeni mwilini) kulikosababishwa na majeraha kifuani (Pneumothorax) (Asphxia due to pneumothorax).