Mwalimu aliyetekwa afariki kwa kunyweshwa sumu

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,008
Reaction score
63,990
Mwalimu Nocka Mwaisango (28) wa Shule ya Sekondari Kibwe, jijini Dodoma, amefariki dunia baada ya kunyweshwa sumu na watu wasiofahamika.

Alikufa wakati akitokea mkoani Dodoma kwenda kijijini kwao mtaa wa Mtakuja, Mbalizi Wilaya ya Mbeya Vijijini kwa lengo la kumuoa mchumba wake wa muda mrefu.

Baba mzazi wa mwalimu huyo, Oddy Mwaisango, alisema alipigiwa simu Desemba 20, mwaka jana na mtoto wake huyo kuwa anatarajia kwenda Mbeya kwa mapumziko ya sikukuu na kwamba atatumia mapumziko hayo kumuoa mchumba wake wa muda mrefu.

Alisema baada ya kupigwa simu hiyo, alishangaa kuona muda mrefu unapita bila kumuona na wiki moja baadaye alipigiwa simu na watu wasiofahamika waliotumia namba ya simu ya mtoto wake wakisema kuwa wanamshikilia kwa kazi maalum.

Alisema baada ya kauli hiyo aliamua kwenda Kituo cha Polisi Mbalizi, kuripoti tukio hilo.

Alisema siku iliyofuata mama yake alienda Dodoma katika shule aliyokuwa akifundisha kukutana na Mwalimu Mkuu ambaye alimjibu kuwa mtoto wake hakumuaga alipoondoka.

Alisema, ilibidi aende kuripoti Polisi Dodoma na Kitengo cha Uchunguzi wa Mawasiliano mkoani humo kiligundua kuwa mwalimu huyo yuko mkoani Morogoro.

“Ilibidi mama yake asafiri hadi Morogoro na aliripoti kituo cha polisi na kukabidhiwa mtu wa uchunguzi wa mitandao ndipo katika kuchunguza wakabaini wahalifu hao na mwalimu huyo wako mkoani humo, lakini ghafla wakawa hawaonekani kwenye mtandao,” alisimulia.

Alisema baadaye wahalifu hao walimpigia simu (baba) wakihitaji Sh. 5,000,000 kama kikombozi, lakini kwa sababu hakuwa na fedha aliwatumia Sh. 500,000 ili wamwachie.

Aliongeza kuwa siku iliyofuata mtoto wake aliwapigia simu mwenyewe na kuwaambia kuwa yuko kituo cha daladala cha Tazara Mbeya na walipoenda kumfuata walikuta hajitambui.

Aidha, alisema waliamua kumkimbiza hospitali ya Ifisi iliyoko Wilaya ya Mbalizi na baadaye walimhamishia Hospitali ya Rufani Mbeya.

Alisema akiwa wodini aliongezewa maji ya kutosha, lakini alikuwa analalamika kuumizwa kwenye koo na kifuani na katika uchunguzi wa madaktari ilibainika amenyweshwa sumu.

Alisema siku iliyofuata mwalimu huyo alifariki akiwa hajawataja waliomfanyia unyama huo huku chanzo cha kifo kikitajwa kuwa ni dawa aina ya ‘Asphxia Due Mothorax’ aliyonyweshwa.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibwe, Dodoma, Mwasiti Msokola, alikiri kupata taarifa za kifo cha mwalimu wake na kwamba suala hilo linashughulikiwa na mkurugenzi ambaye ndiye mwajiri wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Chanzo:Nipashe
 
ninaamini kamanda muroto lazima atawakamata hao waahalifu na atawaletabela ya camera kila mtanzania awaone
Unaongea kuhusu nini Mkuu? Mzazi kaenda Ku report kituo cha Police Dodoma, Wataalam wanaohusika na Kesi za Mtandao wakamwambia Mzazi kuwa mwanae yupo MOROGORO, anafika Morogoro na kwenda Ku report tena kituo cha Police MOROGORO.....inawezekana muda uliopotea ni takribani Siku 2, toka Mzazi wa kiume a report tukio Mbeya, mpaka Wataalam wa Morogoro kumkosa Mwalimu kwenye System inaweza kuwa zaidi ya 4...!

Lakini tunaambiwa Walinzi wetu wanafanya kazi kwa ushiriano, tumeona watu wakifanya makosa mkoa mwingine na kukimbilia mkoa mwingine, haraka sana wanakamatwa na kurudishwa kule makosa yalipotendeka.....mbona kwa hili ni Wazazi ndo walikua wanazunguka mkoa mmoja mpaka mwingine?

Watekaji wenyewe wanaonekana hawakua na plan nzuri, kama taarifa za Mbeya zingefanyiwa Kazi kwa wakati, bila kumsubiri Mama aende Dodoma then MOROGORO, Waharifu wale wangetiwa mikononi muda mrefu tu!
 
Mwalimu Nocka Mwaisango (28) wa Shule ya Sekondari Kibwe, jijini Dodoma, amefariki dunia baada ya kunyweshwa sumu na watu wasiofahamika.

Alikufa wakati akitokea mkoani Dodoma kwenda kijijini kwao mtaa wa Mtakuja, Mbalizi Wilaya ya Mbeya Vijijini kwa lengo la kumuoa mchumba wake wa muda mrefu.

Baba mzazi wa mwalimu huyo, Oddy Mwaisango, alisema alipigiwa simu Desemba 20, mwaka jana na mtoto wake huyo kuwa anatarajia kwenda Mbeya kwa mapumziko ya sikukuu na kwamba atatumia mapumziko hayo kumuoa mchumba wake wa muda mrefu.

Alisema baada ya kupigwa simu hiyo, alishangaa kuona muda mrefu unapita bila kumuona na wiki moja baadaye alipigiwa simu na watu wasiofahamika waliotumia namba ya simu ya mtoto wake wakisema kuwa wanamshikilia kwa kazi maalum.

Alisema baada ya kauli hiyo aliamua kwenda Kituo cha Polisi Mbalizi, kuripoti tukio hilo.

Alisema siku iliyofuata mama yake alienda Dodoma katika shule aliyokuwa akifundisha kukutana na Mwalimu Mkuu ambaye alimjibu kuwa mtoto wake hakumuaga alipoondoka.

Alisema, ilibidi aende kuripoti Polisi Dodoma na Kitengo cha Uchunguzi wa Mawasiliano mkoani humo kiligundua kuwa mwalimu huyo yuko mkoani Morogoro.

“Ilibidi mama yake asafiri hadi Morogoro na aliripoti kituo cha polisi na kukabidhiwa mtu wa uchunguzi wa mitandao ndipo katika kuchunguza wakabaini wahalifu hao na mwalimu huyo wako mkoani humo, lakini ghafla wakawa hawaonekani kwenye mtandao,” alisimulia.

Alisema baadaye wahalifu hao walimpigia simu (baba) wakihitaji Sh. 5,000,000 kama kikombozi, lakini kwa sababu hakuwa na fedha aliwatumia Sh. 500,000 ili wamwachie.

Aliongeza kuwa siku iliyofuata mtoto wake aliwapigia simu mwenyewe na kuwaambia kuwa yuko kituo cha daladala cha Tazara Mbeya na walipoenda kumfuata walikuta hajitambui.

Aidha, alisema waliamua kumkimbiza hospitali ya Ifisi iliyoko Wilaya ya Mbalizi na baadaye walimhamishia Hospitali ya Rufani Mbeya.
Alisema akiwa wodini aliongezewa maji ya kutosha, lakini alikuwa analalamika kuumizwa kwenye koo na kifuani na katika uchunguzi wa madaktari ilibainika amenyweshwa sumu.

Alisema siku iliyofuata mwalimu huyo alifariki akiwa hajawataja waliomfanyia unyama huo huku chanzo cha kifo kikitajwa kuwa ni dawa aina ya ‘Asphxia Due Mothorax’ aliyonyweshwa.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibwe, Dodoma, Mwasiti Msokola, alikiri kupata taarifa za kifo cha mwalimu wake na kwamba suala hilo linashughulikiwa na mkurugenzi ambaye ndiye mwajiri wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Chanzo:Nipashe
Huenda alikuwa mwana cdm
 
Unaishi Mbeya.

Unaripoti Kituo cha Dom.

Dom wanakurusha Moro.

Unafika Moro unaanza kuripoti upya.

Kompyuta, Simu, Fax, police database ni ya kazi gani?

Tuweke namna ambayo huyu mama angeripoti tukio akiwa Mbeya, watu wa Mbeya, wawasiliane na wa Dom, wa Dom wafuatilie wamkose shule wajue yupo Moro.
Hawa wa Dom wawasiliane na wa Moro.

Siku zote nasema hatuna sera nzuri ya kudeal na watekaji (pengine ipo ila sijui) negotiation zote ilibidi ziendeshwe na askari siyo hao wazazi hadi wakatuma Laki 5.
Ok imetumwa, askari wanajua pesa imeenda kwa nani? Wana mpango gani?

Magaidi na watekaji hua hawagewi ransom kwakua ukiwapa huo mchezo unaupalilia. Jeshi letu lijikaze jamani. Rais alisema vyeo havitategemea elimu ila kiukweli dunia ya sasa inahitaji elimu kuliko uwezo wa kupasua tofali kwa kichwa.
 
hao waliofanya hivyo ni kuchoma sindano ya sumu ambayo itawapa maumivu makali sana kwa siku tano mfululizo halafu watibiwe
 
Back
Top Bottom