Mwalimu akutwa kalala uchi kwenye kibao cha shule

Mwalimu akutwa kalala uchi kwenye kibao cha shule

Usikute ni sleepwalking tu sisi wabongo tushafikiria uchawi.

Kuna tukio mtu alienda kwa gari hadi nyumbani kwa mama mkwe wake, akawashambulia na kumuuwa mama mkwe, akapanda gari akarudi zake home kwake, kumbe alikuwa kalala muda wote huo
 
haya mambo yapo jamani kwa walimu ulizeni watu mbozi na sumbawanga kuna visa kama hivi kibao tu kwa walimu,kwa hyo mi natoa pole kwa mwalimu na wala si usanii kama wengine wanavyodai hapa
niliiona hii jana kwa kweli ilinisikitisha sana kuona hata katika karne hii ya watu tunajikunja kutafuta elimu mtu unaroga mwalimu ''shame of you'' halafu tukiandamwa na umasikini tunasema mungu hatupendi, ndugu zangu wa lindi inasikitisha sana. Yule kijana nilimuona akijieleza anaonekana he is still young anaweza hata kuachana na kazi ya ualimu na akafanya mambo mengine na akaishi lakini kajitolea kutoa alimu kwa vijana wetu, jamani tuache wafanye kazi kama mmemkamata ugoni kwa wake zenu au watoto wenu mpelekeni tu polisi sheria ichukue mkondo wake.
 
Wewe Preta Beseni mbona kubwa hivyo, hadi kwenye glasi ya maji unashangaa mamba huyo na wewe kiulaini unabebwa.
Preta hii si kweli, mimi mwenyewe wa huko huko Ukerewe lakini sijawahi kuona wala kusikia imetokea. ila habari ninazosikia zamani ilikuwepo hii mambo ya kubebwa na mamba na wala asikutafune! Unanikumbusha baba yangu wakati anajiunga Ifunda sekondari aliibiwa pocket money yake ndo akawatishia kwa stori ya mamba. Yeye alimchukua mjusi kimya kimya akamweka kwenye ndoo ya maji akawaambia wasubiri kidogo tu mjusi atabadilika kidogo kidogo kuwa mamba na atamla huyo mwizi wake! kweli yule mwizi alimrudishia ile pesa kimya kimya!!! na mimi itabidi nianze kuwa na ngao ya ukerewe kwa wezi. hahahaaa
 
nadhani sasa serikali ione namna ya kuwapatia walimu (risk/hardship allowance) na si utitility allowance.
 
Back
Top Bottom